Tarishi Hauwawi

August 15, 2008

‘Dereva wa Wangwe’ aendelea kusota rumande

Filed under: habari — tarishi @ 11:32 am

MSHITAKIWA Deus Mallya (27), anayetuhumiwa kusababisha kifo cha Mbunge wa Tarime, Chacha Wangwe, amekosa dhamana baada ya wadhamini kutotokea mahakamani jana.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Dodoma, Mosses Mzuna, Mallya alishindwa kupata dhamana jana baada ya kutokuwapo kwa wadhamini wa kufanikisha hilo. Dhamana hiyo kwa mshitakiwa huyo ni Sh milioni tano.

Baada ya kukosekana kwa wadhamini, Mallya alirudishwa rumande hadi Agosti 28, mwaka huu wakati kesi yake itakapotajwa tena.

Awali, Mwendesha Mashitaka, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP), Policarp Urio, alisema upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na kwamba dhamana iko wazi.

Awali, Mallya alifikishwa mahakamani hapo Agosti mosi, mwaka huu, akikabiliwa na mashitaka mawili ya kuendesha gari bila leseni na kuendesha kwa hatari na kusababisha kifo cha Wangwe katika eneo la Pandambili wilayani Kongwa Mkoa wa Dodoma, usiku wa Julai 28, mwaka huu.

No Comments Yet »

No comments yet.

RSS feed for comments on this post. TrackBack URI

Leave a comment

Blog at WordPress.com.