Wakati Bunge likielekea ukingoni, Watanzania wengi wanaowasiliana nasi wamekuwa wakiuliza siku ambayo Waziri Mkuu atamaliza kihoro chao kwa kutoa taarifa kuhusu masuala kadhaa muhimu ambayo tumeahidiwa kuwa yatawasilishwa katika kipindi cha hivi karibuni.
Mshawasha huo wa wananchi mbalimbali ambao idadi yao ni kubwa, ndio ambao umetulazimisha kurejea tena na kuikumbusha serikali kuhusu kile wanachokitarajia kutoka kwao.
Miongoni mwa mambo hayo makubwa yanayosubiriwa ni pamoja na utekelezaji wa Azimio la Bunge lililotokana na Ripoti ya Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza utata katika mkataba wa Richmond.
Uzito wa jambo wala hauhitaji maelezo marefu kwani hata Spika wa Bunge wakati akizungumza na wakuu na wahariri wa vyombo vya habari kabla ya Bunge hili kuanza alizungumzia umuhimu wa suala hilo na namna Bunge linavyosubiri kwa hamu ripoti ya utekelezaji kutoka serikalini.
Lakini katika hayo na mengine yote, mtu mwenye kazi nzito atakuwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda, ambaye ndiye kiongozi wa shughuli za serikali bungeni.
Pinda katika hili, yeye ndiye atakayepaswa kutoa ripoti kuhusu utekelezaji wa ripoti hiyo ya Richmond ambayo ilishindwa kukamilika katika Bunge lililopita hata baada ya yeye mwenyewe kuunda kamati yake kufuatilia suala hili.
Mbali ya jambo hili, Pinda atakuwa na dhamana nzito ya kuhakikisha kuwa, anafanikiwa kutimiza baadhi ya ahadi nzito alizopata kuzitoa kuhusu maamuzi ya kiserikali au masuala yanayohusu Bunge.
Kwa mfano, Pinda atalazimika kuwathibitishia Watanzania kwamba kauli aliyoitoa wakati alipokutana na wahariri katika mkutano wake wa kwanza aliofanya nao inathibitishwa.
Naamini wahariri na Watanzania wanakumbuka namna Pinda alivyoahidi kwamba serikali haitakuwa na mzaha wa kuwaacha viongozi ambao watakiuka misingi na maadili ya uongozi.
Katika hili alisema wao serikalini, hawatakuwa tayari tena kuwavumilia viongozi watakaoirejesha nyuma serikali na akatumia maneno makali akisema; ‘tutakufa na mtu’.
Kauli hiyo nzito ya Pinda kwa kiwango kikubwa ilifufua matumaini makubwa ambayo wananchi wanayo kwa serikali ambayo mbali ya Richmond itapaswa pia kutoa maelezo ya namna itakavyotekeleza na kuziba nyufa zilizotokana na kashfa ya EPA iliyoigharimu serikali shilingi zipatazo milioni 133.
Kwa sababu hiyo basi, ni imani yetu kwamba, Pinda ataweza kulieleza Bunge na Watanzania ni kitu gani hasa wamekigundua kuhusu Richmond na hatua ambazo zimechukuliwa au zitachukuliwa dhidi ya baadhi ya viongozi.
Ili kuwarejeshea wananchi imani, Pinda atapaswa kulieleza Bunge na Watanzania hatima ya watendaji kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Dk. Edward Hosseah, ambao bado wanaendelea na kazi hata baada ya kutakiwa kuwajibishwa.
Katika hili serikali itapaswa kutoa ufafanuzi ni kitu gani hasa kilitokea hata kusababisha watu hao pengine waonekane wasio na hatia yoyote kinyume cha kile kilichozungumzwa bungeni.
Hata hivyo wakati serikali ikitoa maelezo yoyote, itapaswa kuangalia na kukumbusha matukio ambayo yalisababisha baadhi ya watendaji serikalini watajwe na watakiwe kuwajibishwa.
Kwa maneno rahisi kabisa ni kwamba, Pinda atapaswa kulinda hadhi yake yeye binafsi, ya serikali na pengine ya Rais Kikwete, ambaye wakati alipoingia madarakani aliwaonya watendaji kuwa makini akisema iwapo mawaziri watakumbwa na fedheha, basi nao watarajie kukumbwa na fagio litakalotokana na matukio ya namna hiyo.
Ndugu zangu Watanzania .Tunaishi kwenye nyakati za hatari za kutisha. Kila siku kuna sauti nyingi sana zinakuja masikioni mwetu.Watu wanotuzunguka wanatuleta sauti nyingi sana. Vyombo tunavovitumia majumbani vinatoa sauti nasauti hizo tunazifuata. Television ,redio, na vinginevyo vingi. Iko sauti inayosema skutafuta fedha nyingi na Wengi wetu tunadhani fedha itatufanya kila kitu kiwe shwari hivyo, tunajitahidi sana tuzipate maana tunaamini tizipata tutakuwa na amani. Ukitaka kujua angalia mtu mwenye fedha anavoishi . Ataukuwa na walinzi wa mchana na usiku na ataona hawatoshi .Anaanza kufuga mbwa mmoja hata kama dhehebu lake haliruhusu kufuga mbwa. Baadaye mbwa mmoja hatoshi ataongeza wengine na wengine. Baadaye mbwa na walinzi hawatoshi atatafuta bastola na baadaye atataka na bunduki hata hivyo hataridhika baadaye mitambo ya umeme na bado hana amani. Hii ndiyo hali halisis. Unanunua gari jipya unajion a wa kisasa unaweka kishoka muda si mrefu anakuja mwingine na gari model mpay zaidi unarudisha mkono ndani. Na Yule aliyeleta mpya kabisa muda si mrefu anakuja mwenzie ambaye anayo wanaita latest . Kishoka kinafichwa ndani.
Waganga wanatoa offer kwa wateja wake kuwaahidi kuwa matajiri endapo watapeleka viungo vikiwa na damu fresh ambayo haijakauka. Hii ni sadaka ya shetani . Wanadhaniwatapata amani endapo watapata veo au madaraka au mali nyingi.
Tukitazama ndugu zangu Watanzania kuna watu katika jamii yetu inatembea siku nzima kwa miguu kutafuta maji ya bwawa yaliyotokana na mvua iliyonyesha. Watoto wanatembea masaa mawili hadi matatu kufika shuleni na kurudi masaa mawili . Hivyo hivyo kuna Watanzania ambao mpaka sasa toroli au mkokoteni wa Miti au mbao ni tekinoljia mpya sana kwao labda hana ndoto lini itafikia muda wa uwezo wa kuipata toroli au mkokoteni
Ukitazama shule za sekondari na vyuo hazina huduma na hata huo mfumo wa mkopo haujakaa sawasawa. Lakini pia ukitazama upande mwingine kuna jitahada za mtu mmoja mmoja na hata serikali za kupata mapato. Ukitazama fedha zilozotumika huko kwa wanaoitwa Mafisadi, Marichond tunayajua na tusiyoyajua ni mengi kweli kweli. Lakini jambo la kuninshangaza ni jinsi tunavyothamini mawazo na rasilimali zetu. Ni Ziko sauti nyingi zinaingia masikioni mwetu tunavyoweza kupambanua na kufanya uchaguzi unaofaa. Tulipotaka kuuza mashirika na mggodi yetu tulifanya haraka sana na hizo fedha hatujui namna ya kuzitumia .Tunachagua kusikia na kutii kila sauti inayoingi masikioni mwetu.
Kila sauti inayoingia amsikioni mwetu laziam tutii. sikia na kutiii , Ikitoka sauti kutoka huku tunatii ikitoka sauti kutoka kule tunatii. Ikija sauti ya ushirikina na uchawi inayotuambia kuwa tutakuwwa matajiri au tutapanda veo kama tukitii tunaifuata. Sauti ya kutumia fedha Tukiangalia fedha za serikali katika mambo amabayo siyo muhimu . Sasa iko sauti inayosikika ya kupanda chuki katika jamii ya Watanzania kuona dini moja ina haki kuliko zingine . Sauti hiyo inakuja pole pole kama vunza ikishaigia chuki itazaa mauti. Na hiyo sauti tumeikariribisha.Chuki ni rahisi kuingia lakini kuitoa ni haiwezekani. Nakumbuka wakati rusha ilpokuwa bado chini sana kama hakuna tulianzisha kitengo cha kuzuia. Mwasisi wa nchi hii Marehemu aliyekuwa rais wa kwanza Mwalimu Julias Kenyere alisema ikiingia rushwa ilkuwa vigumu kuindoa. Hapa tunakabiliwa na mambo megni sana hatujamaliza madai ya wanafunzi wa Shule za msingi, sekondari, vyuo. Mbaya zaidi sasa maoeneo ya shule yanauziwa watu binafsi kutaja mfano Shule ya sekondari ya Arusha na ni ya Serikali kiwanja kimemegwa na kuuziwa mtu binafsi. Ukitazama upande mwingine bado ipo sauti ya wananchi na sauti za Richmond, Wafisadi , Kuna Richmond na wafisadi wengi sana sauti zake zinatuchnganya . Tena ziko sauti inayolia juu ya damu inayomwagwa isiyo na hatia ya Albino , watoto na watu wazima wanauwawa kwa kutolewa sadaka kwa imani za uchawi. Sasa tuna sauti inaingia ya OIC,na Mahakama ya kadhi.
Jambo linalonishangaza ni jisi tunavyopokea sauti hizi na ushawish wa mtu mmoja navoweza kuwaingia watu wakukubaliana na sauti yoyote na ikafanya kazi katika jamii inayoishi katika mwaka wa 2008,
Mtazamo wangu ni kwamba sis tulio wengi miili yetu inaishi katika mwaka 2008 likini mawazo yetu na akili zetu hazijafika mwaka 2008 bado zipo katika miaka ya 1980 wachache sana wamefika 1990 na wachache zaidi wamefikia 2000. Hivyo tunajifariki tu kwa sababu ya mavazi tunayovaa. Yanayotokana na usherehere sherehere.
Tuwe waangalifu na sauti zinazoingia masikioni mwetu
Comment by Albert Sindato — October 27, 2008 @ 12:04 pm |
Ndugu Mhariri nichaposhie maoni yangu hayaNdugu zangu Watanzania .Tunaishi kwenye nyakati za hatari za kutisha. Kila siku kuna sauti nyingi sana zinakuja masikioni mwetu.Watu wanotuzunguka wanatuleta sauti nyingi sana. Vyombo tunavovitumia majumbani vinatoa sauti nasauti hizo tunazifuata. Television ,redio, na vinginevyo vingi. Iko sauti inayosema skutafuta fedha nyingi na Wengi wetu tunadhani fedha itatufanya kila kitu kiwe shwari hivyo, tunajitahidi sana tuzipate maana tunaamini tizipata tutakuwa na amani. Ukitaka kujua angalia mtu mwenye fedha anavoishi . Ataukuwa na walinzi wa mchana na usiku na ataona hawatoshi .Anaanza kufuga mbwa mmoja hata kama dhehebu lake haliruhusu kufuga mbwa. Baadaye mbwa mmoja hatoshi ataongeza wengine na wengine. Baadaye mbwa na walinzi hawatoshi atatafuta bastola na baadaye atataka na bunduki hata hivyo hataridhika baadaye mitambo ya umeme na bado hana amani. Hii ndiyo hali halisis. Unanunua gari jipya unajion a wa kisasa unaweka kishoka muda si mrefu anakuja mwingine na gari model mpay zaidi unarudisha mkono ndani. Na Yule aliyeleta mpya kabisa muda si mrefu anakuja mwenzie ambaye anayo wanaita latest . Kishoka kinafichwa ndani.
Waganga wanatoa offer kwa wateja wake kuwaahidi kuwa matajiri endapo watapeleka viungo vikiwa na damu fresh ambayo haijakauka. Hii ni sadaka ya shetani . Wanadhaniwatapata amani endapo watapata veo au madaraka au mali nyingi.
Tukitazama ndugu zangu Watanzania kuna watu katika jamii yetu inatembea siku nzima kwa miguu kutafuta maji ya bwawa yaliyotokana na mvua iliyonyesha. Watoto wanatembea masaa mawili hadi matatu kufika shuleni na kurudi masaa mawili . Hivyo hivyo kuna Watanzania ambao mpaka sasa toroli au mkokoteni wa Miti au mbao ni tekinoljia mpya sana kwao labda hana ndoto lini itafikia muda wa uwezo wa kuipata toroli au mkokoteni
Ukitazama shule za sekondari na vyuo hazina huduma na hata huo mfumo wa mkopo haujakaa sawasawa. Lakini pia ukitazama upande mwingine kuna jitahada za mtu mmoja mmoja na hata serikali za kupata mapato. Ukitazama fedha zilozotumika huko kwa wanaoitwa Mafisadi, Marichond tunayajua na tusiyoyajua ni mengi kweli kweli. Lakini jambo la kuninshangaza ni jinsi tunavyothamini mawazo na rasilimali zetu. Ni Ziko sauti nyingi zinaingia masikioni mwetu tunavyoweza kupambanua na kufanya uchaguzi unaofaa. Tulipotaka kuuza mashirika na mggodi yetu tulifanya haraka sana na hizo fedha hatujui namna ya kuzitumia .Tunachagua kusikia na kutii kila sauti inayoingi masikioni mwetu.
Kila sauti inayoingia amsikioni mwetu laziam tutii. sikia na kutiii , Ikitoka sauti kutoka huku tunatii ikitoka sauti kutoka kule tunatii. Ikija sauti ya ushirikina na uchawi inayotuambia kuwa tutakuwwa matajiri au tutapanda veo kama tukitii tunaifuata. Sauti ya kutumia fedha Tukiangalia fedha za serikali katika mambo amabayo siyo muhimu . Sasa iko sauti inayosikika ya kupanda chuki katika jamii ya Watanzania kuona dini moja ina haki kuliko zingine . Sauti hiyo inakuja pole pole kama vunza ikishaigia chuki itazaa mauti. Na hiyo sauti tumeikariribisha.Chuki ni rahisi kuingia lakini kuitoa ni haiwezekani. Nakumbuka wakati rusha ilpokuwa bado chini sana kama hakuna tulianzisha kitengo cha kuzuia. Mwasisi wa nchi hii Marehemu aliyekuwa rais wa kwanza Mwalimu Julias Kenyere alisema ikiingia rushwa ilkuwa vigumu kuindoa. Hapa tunakabiliwa na mambo megni sana hatujamaliza madai ya wanafunzi wa Shule za msingi, sekondari, vyuo. Mbaya zaidi sasa maoeneo ya shule yanauziwa watu binafsi kutaja mfano Shule ya sekondari ya Arusha na ni ya Serikali kiwanja kimemegwa na kuuziwa mtu binafsi. Ukitazama upande mwingine bado ipo sauti ya wananchi na sauti za Richmond, Wafisadi , Kuna Richmond na wafisadi wengi sana sauti zake zinatuchnganya . Tena ziko sauti inayolia juu ya damu inayomwagwa isiyo na hatia ya Albino , watoto na watu wazima wanauwawa kwa kutolewa sadaka kwa imani za uchawi. Sasa tuna sauti inaingia ya OIC,na Mahakama ya kadhi.
Jambo linalonishangaza ni jisi tunavyopokea sauti hizi na ushawish wa mtu mmoja navoweza kuwaingia watu wakukubaliana na sauti yoyote na ikafanya kazi katika jamii inayoishi katika mwaka wa 2008,
Mtazamo wangu ni kwamba sis tulio wengi miili yetu inaishi katika mwaka 2008 likini mawazo yetu na akili zetu hazijafika mwaka 2008 bado zipo katika miaka ya 1980 wachache sana wamefika 1990 na wachache zaidi wamefikia 2000. Hivyo tunajifariki tu kwa sababu ya mavazi tunayovaa. Yanayotokana na usherehere sherehere.
Tuwe waangalifu na sauti zinazoingia masikioni mwetu
Albert Sindato
Comment by Albert Sindato — October 27, 2008 @ 12:08 pm |