Tarishi Hauwawi

August 21, 2008

JK ANGURUMA BUNGENI NA KUWEKA MAMBO SAWA

Filed under: habari ndio hiyo — tarishi @ 10:15 pm
President Jakaya Kikwete arrives at the National Assembly to address legislators and the Nation.

President Jakaya Kikwete arrives at the National Assembly to address legislators and the Nation.

Baada ya kutembelea tovuti zote za Tanzania nimegundua ni www.dailynews-tsn.com ambayo imeweza kukidhi sehemu ya kiu ya wananchi kujua Raisa Kikwete anazungumza nini huko Bungeni Dodoma. Na hii imekuja kwa msaada wa blogu ya issamichuzi.blogspot.com ambayo imeelekeza mamilioni ya wasomaji wake kwenda kuona video za hotuba hiyo iliyokuwa ikisubiriwa kwa udi na uvumba na wa-Tanzania wote

Advertisements

August 18, 2008

Mwakyembe awasha moto Zanzibar

Filed under: habari ndio hiyo — tarishi @ 6:50 am
Mh. Harrison Mwakyembe akiwa na Mh. Hawa Ghasia

Mh. Harrison Mwakyembe akiwa na Mh. Hawa Ghasia

   
*SMZ yataka aombe radhi wananchi
*Mwenyewe asema:Sitabadili kauli
*Hati za Muungano sasa zatoa jibuNa Waandishi Wetu Zanzibar, Dar

KAULI iliyotolewa bungeni wiki hii na Mbunge wa Kyela (CCM), Dkt. Harrison Mwakyembe kuwa mawaziri wa Zanzibar wanaoendelea kudai Zanzibar ni nchi ni watovu wa nidhamu, imezidi kuwasha moto na sasa S.M.Z imetoa tamko rasmi ikimtaka mbunge huyo si tu awaombe radhi mawaziri bali pia wananchi wote wa visiwa hivyo.

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) katika ‘kupambana’ na mbunge huyo pia sasa imeibua jipya ikisema kauli ya Dkt. Mwakyembe ni sawa na uchochezi na kejeli.

Msimamo huo rasmi wa SMZ umetolewa jana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Kiongozi. Bw. Hamza Hassan Juma aliyeweka bayana kuwa anawasilisha tamko la Serikali, alipozungumza na waandishi wa habari.

“Mheshimiwa Mwakyembe tunamheshimu sana kama ni mwanasheria…..lakini inaonesha wazi amekiuka maadili kwani matamshi aliyotoa ni kejeli kubwa kwa mawaziri wa SMZ na kusisitiza Serikali haiwezi kukaa kimya katika suala hilo,” alisema.

Hamza ambaye ni mjumbe wa Baraza la Wawakilishi kutoka jimbo la Kwamtipura, alisema mawaziri wa SMZ kamwe hawawajibiki kwa Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda wala Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“SMZ haiwajibiki kwa Bunge…hapa kipo chombo chake cha kutunga sheria-Baraza la Wawakilishi….wadhifa wa Pinda sawa sawa na wa Waziri Kiongozi Shamsi Nahodha,” aliongeza Bw. Hamza.

Akichangia hotuba ya Wizara ya Sheria na Katiba katikati mwa wiki hii, Dkt. Mwakyembe ambaye ni mtaalamu wa sheria za katiba aliyehitimu shahada yake ya Udaktari wa Falsafa (Ph. D) kutoka Chuo Kikuu cha Hamburg, Ujerumani, alisema kitendo cha baadhi ya mawaziri wa Zanzibar kupingana na Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda ni kejeli dhidi ya kanuni ya kikatiba ya uwajibikaji wa pamoja wa mawaziri.

Naibu Waziri Kiongozi wa Zanzibar, Bw. Ali Juma Shamhuna, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Bw. Idd Pandu Hassan, baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Bunge la Muungano ni miongoni mwa wanasiasa wa Zanzibar waliokuwa wakilumbana na Bw. Pinda wakisisitiza kuwa Zanzibar ni nchi inayojitegemea.

Dkt. Mwakyembe ambaye kati ya mwaka 2001 na 2005 alikuwa mshauri wa sheria wa Chama cha Mapinduzi (CCM) NA Kamishina visiwani Zanzibar akisaidia kujenga utawala bora na kuimarisha katiba, katika mchango wake huo bungeni, alitaka viongozi hao wa Zanzibar wachukuliwe hatua kwa kubishana hadharani na Waziri Mkuu wa Muungano.

Hamza akizungumzia kauli hizo za Dkt. Mwakyembe, aliongeza kuwa wameamua kumtaka Mbunge huyo si tu kuwaomba radhi mawaziri wa Zanzibar bali kufanya hivyo kwa wananchi wote wa visiwa hivyo.

Alipoulizwa, Dkt. Mwakyembe alijibu kwa kifupi, akionekana kupuuza shinikizo hizo kwa kusisitiza kuwa hatafuta kauli yake aliyoitoa Bungeni.

Naye Naibu Spika wa Bunge, Bibi Anne Makinda alipoulizwa kuhusu kanuni za Bunge zinasemaje kuhusu shinikizo anazopewa Dkt. Mwakyembe, alimtaka mwandishi azitafute ili ajionee mwenyewe.

Kisheria, kauli inayozungumzwa Bungeni ina kinga ya kutohojiwa katika chombo chochote cha kisheria hata hivyo uamuzi wa Spika katika shauri la Reginald Mengi na Mbunge Adam Malima, pamoja na kusisitizia kinga hiyo ulielezwa kuwa mwananchi wa kawaida aliyeumizwa na kauli iliyotolewa bungeni, anaweza kuwasilisha malalamiko yake kwa Spika.

Katika hatua nyingine, wakati sakata hilo likichukua sura mpya, uchunguzi wa Majira Jumapili, umebaini kuwa pamoja na wanasiasa wa Zanzibar kushupalia kuwa visiwa hivyo ni nchi, Hati za Muungano ambazo gazeti hili limefanikiwa kuziona, zinasisitiza kuwa April 26, 1964 iliundwa nchi moja ya muungano.

Kwa mujibu wa hati hizo ambazo kwa sasa ni sehemu ya sheria iitwayo ‘The Union Between Tanganyika and Zanzibar Act (no. 22) 1964, kifungu cha 4, kinatamka bayana kuwa nchi iliyoundwa ni moja.

Kifungu hicho kinasema: ” Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, zitaungana na kuunda nchi moja; Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar’.”Baadaye jina la jamhuri hiyo lilibadilishwa na kuitwa Tanzania.

Uchunguzi zaidi umebaini kuwa utata wa Zanzibar kuwa nchi au la pia ulishatatuliwa na Mahakama ya Rufani katika hukumu yake ya Novemba 21, 2000 katika kesi ya S.M.Z. vs. Machano Khamis Ali & Others (Criminal Application no. 8 of 2000), ambapo Jaji Augustino Ramadhani katika sehemu ya hukumu hiyo alisema:

“Ni vyema tukabaini ibara hiyo (ya 103 ya katiba ya Muungano) inabainisha wazi kuwepo kwa kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na si Kiongozi wa Nchi ya Zanzibar ingawa Kiongozi huyo wa Serikali ya Mapinduzi anaitwa Rais.

“…Hili linafupisha mjadala na kufikisha hoja ya dhahiri kuwa Zanzibar si nchi, si tu kwa mujibu wa sheria za kimataifa bali pia hata kwa mujibu wa katiba ya Muungano.”

Raza, NRA ndio wakereketwa zaidi wa utaifa wa Zanzibar?

Filed under: habari — tarishi @ 6:11 am
Bendera ya 'Taifa' la Zanzibar

Bendera ya 'Taifa' la Zanzibar

Raza, NRA ndio wakereketwa zaidi wa utaifa wa Zanzibar?
Na Theodatus Muchunguzi  MOJA ya matukio makubwa ya kisiasa yaliyotawala nchini ni shinikizo la maandamano tuliyoelezwa kuwa yaliandaliwa na Chama cha National Reconstruction Alliance (NRA) Zanzibar kwa ajili ya kupinga kauli iliyotolewa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuwa Zanzibar si nchi, bali sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Maandamano hayo awali yaliruhusiwa na polisi, lakini baadaye yalizuiliwa na kusababisha malalamiko kutoka kwa viongozi wa NRA Zanzibar, makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), akiwamo mfanyabiashara maarufu, Mohamed Raza, ambaye ni Mshauri wa zamani wa Rais wa Zanzibar, Dk Salmin Amour, kuhusu mambo ya Michezo pomoja na Wazanzibari wengine.

Inasemekana malalamiko dhidi ya Jeshi la Polisi yalitokana na hasara ambayo waandaaji wa maandamano hayo waliipata. Hasara hizo ni pamoja na kuandaliwa kwa fulana zilizokuwa zimeandikwa maneno ya kudai Zanzibar.

Kuna mambo yanayopaswa kuhojiwa kuhusu nani hasa aliyekuwa nyuma ya maandalizi ya maandamano hayo. Nasema hivyo kwa sababu itakumbukwa kuwa NRA ni miongoni mwa vyama vichanga; nikimaanisha kwamba nguvu yake katika siasa za Tanzania bara na Visiwani si kubwa.

Chama hicho hakina hata kiti cha ubunge Tanzania Bara na hakijawahi kufanya vizuri katika chaguzi zote za mwaka 1995, 2000 na 2005. Safu ya uongozi na mtandao wa wanachama na wafuasi wa chama hicho ni mambo ambayo hayaeleweki vizuri.

Kwa Zanzibar, NRA hakina ngome yoyote kwa kuwa siasa za Zanzibar hakuna asiyezifahamu kwamba ni vyama viwili tu vya CCM na Chama cha wananchi (CUF) vyenye mitandao na ngome za wanachama na wafuasi, viti vya ubunge na uwakilishi pamoja na safu za uongozi madhubuti na zinazoeleweka vizuri.

Ujasiri wa NRA wa kuandaa maandamano ya Wazanzibari eti kudai nchi haukuhojiwa na mtu yeyote vikiwemo vyombo vya habari, lakini lilikuwa ni suala muhimu kulihoji kwa kuzingatia kuwa chama kichanga kama hicho, tena huko Zanzibar kuwa na ubavu wa kuandaa maandamano ya kitaifa ya kudai Zanzibar.

Baadhi ya maswali ni je, NRA ambacho ni miongoni mwa vyama vya siasa 18 nchini vyenye usajili wa kudumu lakini hakipokei ruzuku yoyote kutoka serikalini kutokana na kutokuwa na viti vya ubunge kilipata wapi fedha za kuandaa maandamano hayo ya kudai Zanzibar?

Kitu kingine ambacho kinashangaza na kinahitaji majibu ni je, baadhi ya wanachama na makada wa chama tawala CCM walijihusishaje na maandamano hayo, achilia mbali kauli zao za kupingana na Pinda kuhusiana na suala la hadhi ya Zanzibar?

Raza, ambaye katika siku za karibuni amekuwa mstari wa mbele kutoa kauli mbalimbali za kupingana na kauli ya Pinda kuhusiana na hadhi ya Zanzibar, baada ya maandamano hayo yanayoitwa ya NRA kufutwa na Jeshi la Polisi, aliitisha mkutano wa waandishi wa habari siku hiyo Jumapili na kutoa kauli za kuchochea kuvunjika kwa Muungano, akidai kuwa Zanzibar inamezwa katika Muungano huo.

Raza alikaririwa na vyombo vya habari akiwataka Wabunge wa kutoka Zanzibar warejee makwao kwa madai kuwa hawaiwakilishi Zanzibar kama nchi. Pia aliwataka wafanyakazi wa taasisi za Muungano zilizopo Tanzania Bara wakiiwakilisha Zanzibar katika serikali ya Muungano kuwa wanapaswa kurudi kwao kwa kuwa Zanzibar sio nchi.

Alikwenda mbali zaidi kwa kudai kuwa Wazanzibari wote kwa sasa ni wahaini na wataendelea kuwa wahaini hadi suala hili litakapopatiwa ufumbuzi; akiwa na maana kuwa mtu anayesema Zanzibar ni nchi anachukuliwa kuwa ni mhaini. Raza pia alidai kwamba, vikao vilivyokaa kuidhinisha kwamba Zanzibar si nchi havikuwa halali kwa kuwa havikupata ridhaa ya Wazanzibari!

Kauli hizo za Raza zinazua maswali mengi. Moja, ni kuwa ilikuwaje Raza akajitokeza kulishambulia Jeshi la polisi kwa kuyapiga marufuku maandamano hayo? Pili, ni kwa nini Raza alijitokeza siku hiyo hiyo ambayo maandamano hayo yalikuwa yamepangwa kufanyika?

Baadhi ya wasomaji walionitumia ujumbe mfupi wa simu wakidai kuwa baadhi ya makada wa CCM na vyama vingine vya siasa walikuwa nyuma ya maandalizi ya maandamano hayo ya NRA. Wengine walikwenda mbali kwa kudai kuwa ajenda kuhusu suala la hadhi ya Zanzibar imewaunganisha Wazanzibari wote bila kujali itikadi zao za kisiasa.

Wakati mjadala kuhusu hadhi ya Zanzibar ulipoanza baada ya kauli ya Pinda bungeni mjini Dodoma, serikali ya Jamhuri ya Muungano na CCM zilijiweka pembeni kukwepa malumbano na ilifikia wakati vyombo vya habari na wanasiasa kuhoji sababu za ukimya huo wa kushindwa kulitolea tamko kama chama au kauli ya rais Jakaya Kikwete.

Muda mchache kabla ya Jumapili ambayo maandamano hayo yalipangwa kufanyika, mwanasiasa mmoja mkongwe nchini kutoka CCM aliniambia kuwa: ”Kama serikali itaruhusu maandamano ya kudai Zanzibar yakafanyika, hizo zitakuwa dalili tosha za kuthibitisha kuwa mwisho wa Muungamo umefika”.

Baadaye niliposikia habari za kupigwa marufuku kwa maandamano hayo, nilipata hisia kuwa pengine watu wenye busara wamewashauri viongozi wetu kuchukua hatua hiyo, ambayo kwa wenye uwezo wa kupima mambo na kuyatafakari watakubaliana nami kuwa ingeleta athari.

Kila mtu ana haki ya kuelezea hisia na kutoa maoni yake, lakini maandamano hayo tunayoambiwa kuwa yaliandaliwa na NRA kwa ajili ya Wazanzibari kudai nchi yao yaliandaliwa bila kusubiri ahadi iliyotolewa na serikali kwamba wataalamu wa sheria wa pande zote wangekaa na kupitia mambo, zikiwemo tafsiri za kisheria zinayoonekana kusababisha utata katika suala zima la Muungano.

Ni kweli kabisa kwamba kwa kiwango kikubwa serikali zote mbili zilichelewa sana kukaa pamoja kubainisha na kujadili baadhi ya kasoro za msingi, ambazo kwa zaidi ya miaka 40 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zimekuwa zikizua utata.

Huu ndio wakati ambao agizo la Rais Jakaya Kikwete linapaswa kuwataka Waziri Mkuu na Waziri Kingozi wa Zanzibar kukutana na kujadili namna ya kumaliza kasoro zilizoko katika Muungano. Aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa na waziri Kiongozi, Shamsi Vuai Nahodha, walijitahidi kuanza mchakato huo lakini matunda yake hayakuonekana.

Kwa kuwa Rais Kikwete hivi karibuni alipounda upya Baraza la Mawaziri alimpa Makamu wa Rais, Dk Ali Mohamed Shein kusimamia mchakato huo, kuna matumaini makubwa ya kuondoa kasoro hizo ili kuepukana na uwezekano wa upande mmoja kukosa uvumilifu na kuona njia ya mkato ni kudai nchi kwa maandamano, ingawa hatua hiyo tafsiri yake ni uhaini.

Kauli za Raza za kuwataka Wazanzibari kuususia muungano hazijengi taifa bali zinachochea kulibomoa kwa kuwa leo hii Wazanzibari wakijitoa katika Muungano, kesho Wapemba watadai Pemba yao. Mashambulizi ya wiki iliyopita ya Russia dhidi ya Georgia iliyojitoa katika muungano wa Urusi ya zamani lakini baadaye jimbo la Ossetia nalo likajitoa Georgia ni fundisho tosha kwetu.

Kero za muungano zinawaathiri Watanzania wote na siyo upande mmoja. Kwa hiyo inashangaza sana kuona Raza na NRA wakijifanya kuwa ndiyo wakereketwa wakubwa wa hadhi na utaifa wa Zanzibar kuliko raia wengine.

Baruapepe: theodatusm@yahoo.com

Simu: 0737-038475

Kipi kitaanza, Zanzibar kujitoa Muungano au Pemba kujitenga na Unguja?

Filed under: habari — tarishi @ 6:05 am

Na Makene Tumaini

MWANAMUZIKI nguli wa muziki wa reggae kutoka Afrika Kusini, Lucky Dube, alipata kuimba katika moja ya nyimbo zake kuwa, ‘If you follow politician, you will never come far,’ kwamba ukiwasikiliza na kuwafuata wanasiasa hautafika mbali. Watakuacha solemba tu. Kwa maana ya kwamba wanasiasa si watu wa kuaminika sana, wakati wote.

Kwa mfuatiliaji wa masuala ya siasa, sehemu yoyote hapa duniani, achilia mbali Tanzania, anaweza kuwa na mifano mingi tu, kuweza kuelezea na kulithibitisha hili. Wazo hili linaweza kuungwa mkono na hoja nyingine kwamba katika siasa hakuna rafiki wala adui wa kudumu.

Adui yako mkubwa leo anaweza kuwa rafiki yako mkubwa kesho na kinyume chake. Ndiyo maana mtu hapaswi kushangaa leo Wamarekani wakimsaka rafiki na kipenzi chao hapo zamani – Osama Bin Laden. Haishangazi kusikia kuwa Jonas Savimbi aliuawa baada tu ya waliokuwa wakimpa kiburi, kumsaliti kwa serikali ya Angola, si wengine nao ni hao hao Marekani.

Mlolongo unaweza kuwa mrefu, usishangae pia unapomuona ghafla, Muammar Gaddafi, rais aliyekuwa akihesabika kuwa mmoja wa adui wa nchi ya Marekani na washirika wake wa Ulaya, sasa ni mtu wao wa karibu.

Hiyo ndiyo siasa. Lakini pia hayo ni ya Musa (ughaibuni), ya Firauni (hapa nyumbani), pia yanaweza kukumbukwa na kuonekana. Wapo akina Leo Lekamwa na Augustine Mrema. Tunaweza kuwakumbuka watu kama Masumbuko Lamwai na Tambwe Hiza, tukiwataja kwa uchache tu. Historia inaonesha hivyo, haijafutika.

Halafu kuna hili na Zanzibar kuwa ni nchi au la, nalo limetufikisha katika uhalisia wa wanasiasa wetu na siasa kwa jumla. Suala limezua suala, kila mwenye uwezo wa kusema ameshasema na kunukuliwa na vyombo vya habari.

Mara nyingi kwa watu wafuatiliaji wa ‘mtifuko’ wa kisiasa Tanzania, hasa unapohusisha masuala ya Muungano kuna watu ambao hawawezi kujiuzia kulisema.

Haliwezi kupita jambo la nafasi ya Zanzibar katika Tanzania usiwasikie watu kama akina Raza, Maalim Seif Sharif Hamad na wengine (kwa siku za hivi karibuni wanavuma pia akina Shamuhuna.

Wote waliotarajiwa kupaza sauti zao katika suala hilo, ambalo chimbuko lake ni kauli ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakati akitoa hotuba ya majumuisho ya Ofisi yake, wameshafanya hivyo.

Hilo limesababisha kuwa na ‘Muungano usio rasmi’ kati ya mahasimu wakubwa wa siasa za Zanzibar – CCM na CUF. Hiyo ndio siasa.

Jamaa sasa wanaonekana kuwa ni kitu kimoja, mtu akihisi kuwa kwa sasa hawa jamaa wanaweza hata wakakutana kwa siri na kupanga mikakati ya kuibuka na hoja za pamoja, hata kama wasipotaka kuonesha hivyo hadharani, atakuwa hakosei.

Kwamba wahafidhina na wanamageuzi wanaweza kukaa meza moja kwa suala hili na mwisho wa siku wakaongea lugha moja, ni suala ambalo linaweza kusubiri muda tu kwa jinsi wanasiasa wetu wanavyoendesha mambo kwa kubahatisha, bila kuwa na mpangilio.

Halafu, wanasiasa walivyo watu wa ajabu wenye kutaka kulazimisha kidole cha shahada kiwe sawa na cha kati kwa urefu na ukubwa. Katika hili la Zanzibar yameingizwa mambo mengi ambayo hapo awali hayakufikiriwa.

Wahusika (wanasiasa) wote wanaorusha hoja zao, vijembe vyao, jeuri yao na kupima mbavu zao katika ulingo wa siasa, hasa wakijaribu kupinga hoja ya Pinda, kwa hoja za nguvu (badala ya nguvu ya hoja). Hawataki kuwaeleza wasikilizaji wao kuwa kati ya dola, nchi, taifa kipi hasa kinagomba hapa.

Mwanasiasa yeyote makini hasa kutoka chama makini chenye kuwa na washauri wa masuala ya sheria na katiba, bila shaka angelitazamiwa kuja na hoja iliyotokana na tafakuri jadidi.

Angechambua hoja, kupitia misingi yote na hatimaye kufikia hitimisho murua, lenye mantiki na linaloeleweka akiwaacha watu wakiwa wameelewa.

Kama mtu wa kawaida hawaelezwi masuala ya namna hii kwa ufasaha bila kuangalia mtaji wa kisiasa, tunaweza kuwa na uhakika kabisa hata tuliowasikia majuzi wakiwa wamehamasika (au kuhamasishwa?) kuandamana eti kumpinga Waziri Mkuu, wakiulizwa mmoja mmoja nini hasa kilichowafanya kutaka kubeba mabango, wachache mno watakaoweza kukuambia kitu chenye mantiki kuonesha kuwa wanajua wanachokitaka.

Wanasiasa kama akina Raza, Maalim Seif au Shamuhuna (kuwataja kwa uchache), ndio wenye kuweza kuwafikia kwa urahisi zaidi wananchi wao, kuliko akina Profesa Shivji, Haroub Athuman au Mwesiga Baregu na wataalamu wengine ambao wamekuwa wakijaribu kuzielezea zana zote hizo za taifa, nchi au dola.

Wengine wanasema kuwa wanapanga kuzunguka kote visiwani eti kuzidi kuwahamasisha Wazanzibari waendelee kusimama kidete kutetea ‘nchi’ yao.

Lakini hamadi ni iliyo kibindoni, wanatafuta kuungwa mkono katika upande ambao tayari wameshachukua msimamo bila kujali kama utakuwa na maslahi kwa wananchi wote.

Unapomsikia kiongozi wa serikali, akiwa pia na kofia ya uanasiasa, anatoa kauli kumjibu mkubwa wake kuwa hizi si zama za kutishana na kubembelezana kuhusu Muungano, anafaa kutazamwa kwa macho makini.

Kwani wakati Pinda akiibua hoja ile alimtisha mtu? Mbona alipata kurudia kwa masikitiko akisema alimaanisha nini. Lakini hawa tunaowasikia wakitema cheche, hata hawafafanui msingi na maana hasa ya madai yao, tujichunge nao.

Wanaompinga Pinda, iwe vibarazani, mikutanoni, maofisini na hata katika kumbi kubwa za kuheshimika kama Baraza la Wawakilishi, wangesubiri wanasheria wafanye kazi zao kama Waziri Mkuu alivyoelekeza, wangeonekana wanabembeleza?

Maneno yasiyokuwa na mpangilio baadhi yao yamewabubujika. Badala ya kueleza suala, wanaishia ‘kutukana’, kukejeli, kurusha vijembe, kukebehi na hata kutumia ujuzi wa maneno ya Kiswahili yasiyokuwa na tija yoyote katika ujenzi wa hoja ya suala zima.

Shamuhuna amewahi kukaririwa akiibua hoja tata wakati watu walipokuwa wakisema suluhisho la mpasuko wa kisiasa Zanzibar ni serikali ya mseto. Ilibidi CCM watoe kauli kuwa hayo yalikuwa ni maoni yake binafsi. Lakini kwa hili la sasa, hatujasikia ikisemwa hivyo na chama hicho.

Kutokana na ukimya wa sasa hasa kutoka kwa watu tuliotarajia wawakemee na kuzisukumizia mbali kauli za akina Shamuhuna, tunashawishika kuamini kuwa safari hii kauli hii si ya kwake binafsi, inasukumwa au anasukumwa na wengine wengi nyuma yake.

Na kwa kuwa Shamuhuna si mtu mdogo katika CCM na serikali ya Mapinduzi Zanzibar, ukiachilia mbali Raza ambaye hatujui alitumia nguvu inayotokana na wadhifa upi kumbeza Tambwe, ukiongeza na ukimya wa ‘mabosi’, tunashindwa pia kujizuia kuamini kuwa huo ndio msimamo atakaokwenda nao katika meza ya majadiliano, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar.

Maalim Seif nafikiri katika hili atapaswa kuwaeleza vizuri Watanzania. Kwa sababu mbali na kushangilia hukumu ile kesi ya uhaini ya akina Machano na wenzake mwaka 2000, hivi majuzi kanukuliwa akimsihi Rais Karume atangaze mgogoro wa kikatiba katika Muungano.

Katika mkutano huo wa Kibanda Maiti, kama alivyonukuliwa, Maalim Seif alitumia muda wake akimsifia Mzee Karume, kuwa alikuwa imara asiyepata kuyumbishwa.

Kwa kauli ya namna hiyo tunaweza kusema kuwa Maalim Seif alikuwa akimkubali Karume baba. Lakini wa sasa, hajawahi kutamka hivyo.

Lakini ni Maalim Seif huyo huyo ambaye hajapata kumtambua Karume kama rais wa Zanzibar, kwa misingi ya kwamba alimnyang’anya tonge mdomoni.

Katika hili, ni vyema vyama vyote vinavyosema kuwa vinalilia ‘haki’ au ‘hadhi’ ya Zanzibar viwe na msimamo madhubuti katika makabrasha yao, kama ni katika ilani au katiba zao.

Lakini ili kuonesha kuwa wanarukia mambo, ukitazama katiba zao, itakuwa ni bahati ya mtende kukuta ‘hadhi’ ya Zanzibar imeelezwaje, kama ni dola, nchi, taifa, mkoa, au vyovyote vile. Huko ni kubahatisha mambo.

Sasa CUF imepata changamoto kubwa kutoka kwa mmoja wa wawakilishi wake, aliyeamua kujitolea kumfunga paka kengele.

Bila kutafuna maneno kasema sasa ni muda mwafaka wa chama hicho kuitambua serikali ya Rais Karume. Hakuna haja ya kuendelea kutoitambua serikali kwa muda wote huu na wakati huo huo hali halisi ikionesha kuwa wako pamoja.

Lakini katika harakati zao za kudai nchi yao, ni vizuri baadhi yetu tukaelezwa waziwazi, kuwa ni kipi wanasiasa wetu wanataka kitangulie, kumeguka kwa Muungano au kujitenga kwa Pemba na Unguja.

Kwa sababu kumekuwapo na maneno mengi hasa baada ya kuzorota (au kukwama) kwa mazungumzo ya muafaka kuwa ni bora Pemba akajitegemea, kwani imekuwa ikitengwa katika serikali ya sasa ya Karume.

Sasa hao hao ambao tumepata kuwasikia wakipaza sauti zao wakitaka Pemba iwe na serikali yake, tunawasikia wakitaka Zanzibar isibabaishwe katika Muungano na kwamba inaweza kujitoa. Wana ajenda gani hawa? Kwamba wanajua wakifanikiwa kuuvunja Muungano itakuwa rahisi kwao kukitenganisha kisiwa cha Pemba?

makene_84@yahoo.com 0713 58 44 82

August 15, 2008

Mbowe afanyia sherehe kifo cha Wangwe

Filed under: habari ndio hiyo — tarishi @ 1:03 pm

Mwenyekiti wa Chadema Mh. Freeman Mbowe

Mwenyekiti wa Chadema Mh. Freeman Mbowe

Na Tarishi, magazeti

 

 

 

MWENYEKITI wa CHADEMA, Bw. Freeman Mbowe, anadaiwa kufanya hafla kubwa Afrika Kusini saa chache baada ya kupata taarifa za kifo cha Makamu wake, marehemu Chacha Wangwe.Habari zilizopatikana kutoka hoteli ya Garden Court jijini Johanesburg ilikoifanyika hafla hiyo Julai 29 mwaka huu, zilisema baada ya Mwenyekiti Mbowe kupokea taarifa za msiba, alifanya hafla ya kuwaaga wajumbe aliokuwa nao huko ili arejee nchini kwa mazishi.

“Kwanza taarifa ilipopatikana, hakututangazia mpaka tulipopata kutoka kwa vyanzo vyetu vingine ndipo tukathibitisha naye…akatuandalia hafla jioni ya siku hiyo,” kilidai chanzo cha habari hii.

Kilidai kuwa kilishangaa kuona katika mazingira yale ya majonzi, kuandaliwa hafla kubwa namna ile.

“Tulishangaa na kumuuliza kwa nini hafla ile, akatujibu kuwa alikuwa akituaga, kwani anarudi nchini kushiriki mazishi ya marehemu Wangwe,” kiliongeza chanzo hicho.

Kilidai kuwa hata wajumbe wa vyama vya siasa waliokuwa nchini humo kuhudhuria semina ya vyama vyenye wabunge Afrika, walipotaka kumchangia rambirambi, hakutaka kuipokea na badala yake kuwaambia kila mmoja ataje kiwango naye atawalipia.

“Tulitaka kumchangia fedha za rambirambi mwenzetu huyo, lakini hakuonesha nia ya kuzipokea na badala yake akatuambia kila mmoja ataje kiwango chake naye akifika Tanzania ataziwasilisha msibani,” kilidai chanzo hicho.

Wajumbe tisa kutoka Tanzania walikuwa wakiongozwa na Bw. Mbowe katika semina hiyo ya siku nne ya kujifunza jinsi Tume Huru ya Uchaguzi inavyofanya kazi nchini Afrika Kusini.

Chanzo hicho cha habari kilisema semina hiyo ilikuwa ni kwa ajili ya makatibu na naibu makatibu wa vyama vya siasa nchini, lakini walishangaa kumwona Mwenyekiti wa CHADEMA naye akishiriki.

“Yawezekana alialikwa, lakini mbona wenyeviti wenzake hawakualikwa, tulijiuliza sana lakini tukaacha mambo yaendelee hivyo hivyo,” kilidai chanzo hicho.

Pia wanasiasa hao walikutana na viongozi wa chama tawala cha Afrika Kusini cha African National Congress (ANC).

Wajumbe waliohudhuria semina hiyo ni wawili kutoka CHADEMA, wawili CCM, mmoja mmoja CUF, TLP, Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Tume ya Haki za Binadamu na Mkurugenzi wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD).

Bw. Mbowe alipoulizwa kuhusiana na madai ya kuwaandalia tafrija baadhi ya watu aliokuwa akihudhuria nao mkutano huo, kabla ya kurejea Dar es Salaam kuhudhuria msiba wa marehemu Wangwe, alijibu:

“Hao waliokuambia ni akina nani! Waambie wakuthibitishie maana siwezi kuingia kwenye malumbano ya mambo ambayo hayakuwapo.”

Alipoulizwa ilikuwaje akahudhuria mkutano huo wakati ulikuwa ni kwa ajili ya makatibu wakuu na manaibu wao kutoka vyama vyenye wabunge, Bw. Mbowe alisema alipewa mwaliko wa kuhudhuria mkutano huo.

“Mimi nilialikwa na watu TCD kuhudhuria mkutano huo,” alisisitiza Bw. Mbowe alipozungumza na gazeti hili kwa njia ya simu.

Akizungumzia madai kuwa alikataa michango waliyotaka kutoa baadhi ya washiriki aliokuwa nao kwa ajili ya rambirambi na badala yake kudaiwa kuwataka watoe ahadi zao na akifika Dar es Salaam atawatolea, Bw. Mbowe alijibu:

“Wewe zungumza na vyanzo vyako hivyo vikuthibitishie  kama hayo yalitokea.”

Bw. Mbowe alimtaka mwandishi wa habari hizi kuwauliza watu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) au CCM au TCD kama kweli hayo yalitokea au la kwa sababu nao walihudhuria mkutano huo.

 

Chacha Wangwe aibuka toka kuzimu

Filed under: habari ndio hiyo — tarishi @ 12:15 pm

Hayati Chacha Wangwe

Hayati Chacha Wangwe

JARIDA LA CHACHA ZAKAYO WANGWE MBUNGE WA TARIME CHADEMA

 

 

 

Utangulizi:

 

Jarida hili la Mheshimiwa Chacha Zakayo Wangwe lina sehemu tatu.  Sehemu ya kwanza litaweka bayana na kufafanua sababu za mimi kuchafuliwa kisiasa na baadhai ya viongozi wa ngazi za juu za Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, na sehemu ya pili itaonyesha baadhi ya maswali ya msingi niliyopata kuuliza Bungeni na majibu yake na sehemu ya tatu itakuwa na michango mbalimbali niliyopata kuchangia kwa muda wa miezi miaka miwili na nusu.

 

Lengo hasa la Jarida hili ni kumwelewesha Mtanzania na hususan MWANADEMOKRASIA juu ya tuhuma zilizoelekezwa kwangu kwa lengo la kunichafua kisiasa huku viongozi wa CHADEMA wakidai kukisafisha chama jambo ambalo si kweli na ni kampeni chafu zilizoandaliwa na baadhi ya viongozi wa Chama na kuwarubuni wajumbe 31 wasiokuwa wanademokrasia na kunipaka matope ya siasa zao zisizo na hata chembe ya Demokrasia.

 

Nasema hivi nikijua wazi kwamba, CHADEMA kama chama kinaendeshwa kwa katiba na kwa wakati huo huo kikiwa kinaendeshwa kidikteta na kauli za NDIYO MZEE.  Ninajua wazi kwamba, viongozi wa sasa wa chama changu wanatofautiana sana na viongozi wa mwanzo wakati CHADEMA ikianzishwa kwani wanatofautiana kiitikadi, kisera na hata kimtazamo.  Kwa mfano, mzee Mtei alikuwa akikieneza chama hasa vijijini miaka ya 95 kwa kutumia magari chakavu na alifanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwashawishi wananchi na wakijua kuwa CHADEMA si chama cha mjini, na hapa ndipo mwanzo wa CHADEMA kuwa Chama Tawala kule Tarime hadi sasa.  Ila katika uongozi huu wa kizazi kipya basi kila kitu kinaenda kwa kauli za “Mheshimiwa Mwenyekiti kasema” na matumizi mabaya huku ufisadi ukikitafuna chama kwa matumizi hewa na kwa kigezo kuwa eti wanajilipa madeni ya Kampeni.  Nililia sana juu ya matumizi ya helkopta katika kampeni lakini nikaanza kuonekana kuwa mini ni mbaya.  Binafsi sikuona sababu za Chama kutumia helkopta ilhali bado wanachama wa vijijini hawakijui chama wala sera zake huku viongozi wa wilaya na mikoa wakishindwa hata kutoa durufu (photocopy) za viepeperushi vya chama kwa kukosa ruzuku.  Hii si sawa.

 

SEHEMU YA KWANZA

 

Sababu za baadhi ya Viongozi wa CHADEMA kuamua kunichafua kisiasa.

 

          Baadhi ya Kampeni za chini chini dhidi yangu, tarehe 28 na 29 Juni 2008 katika kikao cha Kamati Kuu kilichofanyika Dodoma ambacho kiluhudhuriwa na wajumbe 31 kiliridhia mimi kuondolewa kwenye wadhifa niliokuwa nao ndani ya chama kama Makamu Mwenyekiti kwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutuhumiwa kuwa navujisha siri za chama kwa CCM.  Binafsi kwangu kama mwanasiasa wa kiwango cha juu ni pigo kubwa sana kisiasa kuchafuliwa na watu 31 tu ndani ya chama.  Ninachokiamini hapa ni kwamba, kutokana na msimamo wangu wa siku nyingi hata kabla sijawa makamu mwenyekiti CHADEMA, ndiyo sababu rasmi ya kupigiwa kampeni na baadaye kura za kutokuwa na imani na mimi kwa taarifa nilizo nazo ni kwamba anaandaliwa Dr. Slaa kushika nafasi hiyo.  Hapa ikumbukwe kuwa Mke wa Dr. Slaa ni diwani kupitia CCM hivyo kuna uwezekano wa sera za chama zikavuja kupitia Mama huyu katika njia mbalimbali.

 

Ofisi ya Katibu Mkuu (Ofisi ya Slaa) ndiyo ya kwanza kunituhumu kuwa nawaingilia majukumu yao katika suala zima la matumizi mabovu ya fedha za ruzuku ya chama.  Chama hupata zaidi ya milioni 60 kila mwezi.  Ni fedha nyingi sana kukijenga chama kama zikipata mipango mizuri na kuachana na matumizi mabovu kama matumizi ya helkopta kwenye kampeni kama ilivyotokea kwenye chaguzi zetu pamoja na baadhiya viongozi kudai kuwa wanajilipa madeni waliokikopesha chama wakati wa kampeni za 2005.

 

Mhe. Philemon Ndesamburo Mbunge wa Moshi Mjini inadaiwa kuwa anakidai chama milioni 100 alizokopesha wakati wa kampeni za 2005.

 

          Mhe. Philemon Ndesamburo Mbunge wa Moshi Mjini inadaiwa kuwa anakidai chama milioni 100 alizokopesha wakati wa kampeni za 2005, Freeman Mboe ambaye hadi sasa ni Mwenyekiti wa chama changu katika ngazi ya Taifa naye kwa taarifa nilizo nazo ni kwamba kila mwezi hulipwa shilingi milioni 10 ili kufidia fedha anazodai kukikopesha chama ambazo ni zaidi ya milioni 500 katika kampeni hizo hizo na hadi sasa anaendelea kukidai chama mamilioni ya shilingi.

 

          Mimi nilipoonyesha wasiwasi juu ya madeni haya yasiyoisha, ikaundwa tume ya kampeni za kutokuwa na imani na mimi.  Binafsi sijui kama viongozi wanaojiita makini kama kina Dr. Slaa na Kabwe Zitto wangeweza kuusimamia ufisadi mkubwa kama huu ndani ya chama huku wakiwa mstari wa mbele kuwafichua mafisadi Serikalini.  Au ni kawaida kuwa Mganga hajigangi?  CHADEMA kuna ufisadi wa aina nyingi sana kuanzia uchapaji bendera hadi manunuzi ya vifaa vya chama!

 

          Katika ofisi ya Vijana nako kunanuka ufisadi kwani ni vijana wachache sana ambao hupata nafasi ya kwenda nje ilhali mikoani nako kuna vijana wanaohitaji kujifunza.  Ofisi hii ina watu maalumu wa kwenda kwenye Semina na Matamasha mbalimbali.  Na watu hao hupangwa na John Mnyika.

 

          Pamoja na hayo, Kurugenzi hii inayoendeshwa na John Mnyika imekuwa ikifanya hesabu za “Mbili mara Mbili toa nne”.  Nakumbuka matamasha mbalimbali yaliyowahi kuratibiwa na Kurugenzi hii kwa kutumia fedha za chama yamekuwa hayana maslahi yoyote kwa chama ….labda kwake mwenyewe kwani itakumbukwa kwamba Kurugenzi ilizindua mfuko ulioitwa Tumaini jipya Septemba 16, 2007 katika hafla ya wafanyakazi vijana na akaunti ya Tumaini Jipya 01810301 NBC ilifunguliwa.  Jumla ya shilingi milioni 6,176,500 zimekusanywa na shilingi milioni 6,064,300 zimetumika kwa shughuli mbalimbali za vijana ikiwemo gharama za hafla yenyewe.  Hafla nyingine kama hiyo ilifanyika Arusha.

 

          Hafla hii ilifanyika tarehe 29 Machi, 2008 The New Polygon Triangel Arusha na kuhudhuriwa na washiriki 67 mgeni rasmi akiwa Mhe. Mzee Edwin Mtei.  Jumla ya shilingi milioni 2,300,700 zilikusanywa na shilingi milioni 1,885,000.  Zimetumika kwa shughuli mbalimbali za vijana ikiwemo gharama za hafla yenyewe.  Sasa najiuliza, kulikua na mantiki gani ya kutumia fedha za chama kiasi cha shilingi 6,064,300 na kukusanya shilingi 6,176,500/=?  Ni faida ya shilingi ngapi ilipatikana kama ameamua kukiingiza chama katika kufanya biashara ya matamasha?

 

          Jingine, tangu nimekuwa mbunge Chadema na Baadaye Makamu Mwenyekiti sijawahi kuandaliwa safari za kibunge ama za kukiwakilisha chama ilhali kuna watu wasio na uwezo kiakili, kifikra na hata nafasi za uongozi lakini waliandaliwa safari za nje.  Chama kimefikia hatua ya kuwakilishwa kimataifa na watu wasio na vigezo kwa ajili ya utawala mbovu!  Siandiki haya kwa kuwa nimeondolewa katika uongozi, hapana!  Hizi ni harakati zangu za muda mrefu juu ya utawala bora.  Tazama, wafuatao wamewahi kusafiri katika mataifa mbalimbali kwa shughuli mbalimbali kukiwakilisha chama.  Mhe. Suzan Lymo (Mb. Viti maalumu) Cape Towan, Afrika Kusini kwa Mkutano wa Interparliamentary Union.  Susan pia amesafiri kwenda USA kwa High Level meeting ya HIV/AIDs mwezi June, 2008.  Mhe. Zitto Kabwe, (Mb) alisafiri kwenda Berlin mara mbili – Mhe. Zitto pia alisafiri kwenda Marekeani kwa wiki 3 kwa mwaliko wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani pamoja na Wabunge vijana toka dunia nzima ambako walipata nafasi ya kutembelea majimbo mbalimbali ya Marekani.  Mhe. Mhonga Said (Mb – Viti maalum)  alisafiri kwenda Burundi kwa Mkutano wa Nchi za Maziwa Makuu.  Mhe. Dr. Slaa amesafiri kwenda Johannesburg, Windhoek na Manzini Swaziland kwa vikao vya Kamati na Bunge la SADC.  Dr. Slaa ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya InterParliamentary Cooperation Committee ya Bunge la SADC.  Mhe. Maulida Komu (Mb. Viti Maalumu)  alisafiri kwenda Nairobi na pia Finland.  Mhe. Ndesamburo (Mb) alisafiri kwenda Australia kama Commissioner wa Bunge.

 

          Wafuatao walisafiri kichama;  Mhe. Mhonga Said (Mb – Viti Maalum), Maulida Komu (Mb – Viti Maalum), Suzan Kiwanga (Afisa Msaifizi Idara ya Uchaguzi na Kampeni) na John Mnyika Mkurugenzi wa Idara ya Vijana) walisafiri kwenda Norway na Sweden.  Anthony Komu (Mkurugenzi wa Fedha na Utawala)  alisafiri kwenda Norway kwa mwaliko wa Centre Party, Mhe. Balozi Ngaiza (Mjumbe wa heshma wa kamati kuu wa kuteuliwa na Mwenyekiti), John Mnyika (Mkurugenzi katika Ofisi ya Vijana), John Mrema (Afisa katika Kurugenzi ya Halmashauri na Bunge), walisafiri kwenda Windhoek Namibia kwa Mkutano wa Dua, na Mhe. Kimesera (Katibu Mtendaji wa kuteuliwa na Mwenyekiti), Suzan Lymo (Mb) Viti maalum, na John Mrema walisafiri kwenda Kampala, Uganda kwa Mkutano wa Dua.

 

          Ndugu Regia Mtema (Afisa katika Kurugenzi ya Vijana) alisafiri kwenda Malawi kwa Mkutano wa NIMD.  Mama Naomi Kaihula (Mkurugenzi katika Idara ya Wanawake) na Regia Mtema walisafiri kwenda Finland kwa mwaliko wa Shirika la Demo Finland.  Johna Mrema, Msafiri Mtemelwa na Happiness Mwaipopo (Sina hakika kama ni Mwanachama) walisafiri kwenda London/Uingereza kwa mwaliko wa Conservative Party/WFD wakati wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.  Mhe. Benson Kigaila (Mkurugenzi wa Oganaizesheni na Mafunzo) alienda Zimbabwe katika uchaguzi uliofanyika 27 June, 2008 kupita Ofisi ya Msajili wa Vyama.

 

          Suala la ukabila ni jambo ambalo halihitaji kupingwa kwani asilimia karibu 85 ya viongozi wa CHADEMA wametoka katika mikoa ya Kilimanjaro na Arusha pamoja na kwamba baada ya mimi kulishupalia jambo hili wameanza kubadilisha majina.

 

          Wapo wanachama kama mimi ambao nao wakipewa nafasi za uongozi ndani ya chama hiki watafanya vizuri zaidi ya hawa na wengine ambao ni Jobless!  Pengine niweke wazi hapa kuwa, mimi ni kiongozi shupavu nisiye kuwa na hata chembe ya woga katika kuteta na kusimamia haki za mwanachama wa CHADEMA tena nisiyependa siasa za kisanii.  Ukweli huu ndio uliowafanya kina Mbowe, Slaa kuwa mstari wa mbele katika kupiga kampeni na baadaye kura ya kutokuwa na Imani na mimi.  Binafsi naamini katika chama cha siasa mtu muhimu ni Mwanachama na si Mwenyekiti au Katibu.  Hapa mimi siandiki maneneo haya kukufanya udhani kuwa nataka kuwa king’ang’anizi kwenye wadhifa niliovuliwa, la hasha bali napenda upate picha halilisi ya uendeshwaji wa Siasa ya CHADEMA na kisha uweze kugundua uhalisia wa mgogoro ulivyo.  Viongozi wa CHADEMA Makao Makuu wamening’oa kutoka katika wadhifa niliokuwa nao kwa sababu zao binafsi na si sababu za chama kama chama, na wanajitahidi kuzunguka mikoani kwa siri kuendelea kunichafua kisiasa kuwa sifai.  Kweli sifai kwa wafuja ruzuku ya chama, kweli sifai kwa mafisadi ndani ya chama ila nafaa kukiendesha chama katika ngazi ya taifa katika nafasi yoyote na siku zote.  Nafaa kwa sababu nimefukuzwa kwa kusema ukweli hivyo nikageuka mwiba kati kati ya majipu, nikatolewa.  Ndiyo, nafaa kwa sababu siko tayari kufanya kazi na watu waliozoea kukaa ofisini kama mafaili!  Nafaa kwa sababu mimi ni mpambanaji, kamanda shujaa niliye tayari kuwajibishwa kwa ajili ya kuwatetea WANADEMOKRASIA hususan WANACHADEMA nchi nzima.

 

          Kuliendesha Taifa kama Tanzania hakuhitaji siasa za kisanii, fitina, na chuki.  Kinachotakiwa ni nani abadilike alete mabadiliko katika siasa ili aweze kukabidhiwa dola na alete mabadiliko.  Wananchi wamechoshwa na siasa zetu ndio maana wanaziita siasa za kisanii.  Wanahitaji mabadiliko.  CHADEMA maana yake ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo, lakini huku wanakoelekea tayari uongozi wa Mbowe na Slaa wameiondosha Demokrasia kwa kunitoa katika wadhifa wa umakamu Mwenyekiti kwa kupiga kampeni ndogo ya wajumbe 31 tu! Tena huku wakinituhumu kuwa navujisha siri za chama!!.  Dhahama kama hii siwezi kuivumilia hata kidogo na ni wazi kuwa hata wanachama wetu hawajafurahishwa na jambo hili.  Mimi nilipokuwa kwenye ngazi hiyo ndipo fedha zilipoanza kupelekwa mikoani kwa viwango halali, ndipo ukarabati wa Makao Makuu ulifanyika.  Niweke wazi hapa kuwa, jambo lililonifanya niandike jarida hili si kuwashawishi Freeman Mbowe na Slaa kunirudisha kwenye nafasi waliyonitoa kwa matusi, la hasha!  Lengo ni kuweka wazi kwa wanachama wajue aina ya uongozi uliopo Makao Makuu ya Chama. Kama ni suala la mimi kurudi katika nafasi hiyo ni mimi mwenyewe nikiamua na kwa kutumia Demokrasia.  Ikumbukwe kuwa, Freeman ndiye aliyesema kuwa hataki kufanya kazi na mimi na kutokana na UMANGIMEZA na Kauli za NDIYO MZEE akapata kuungwa mkono na wajumbe 31 tu!  Baada tu ya mimi kutangazwa kuwa nimetolewa kwenye wadhifa niliokuwa nao nilipata simu nyingi sana za wanachama na hata baadhi ya watendaji Makao Makuu wakiniambia kuwa kama Mbowe hayuko tayari kufanya kazi na mimi, wao bado wananihitaji katika Uongozi Taifa.  Kuna mila ya kichagga kuwa, katika eneo la kazi/biashara, ukimuona anayekusababisha ukose maslahi Fulani unatakiwa kumuondoa kwa gharama yoyote! Na hili ndilo lililojiri kwangu na mwenyekiti wangu.

 

Aluta Continue…………………..

 

Wangwe Chacha Zakayo,

Mbunge wa Tarime-CHADEMA

 

 

KAULI YANGU KWA MSOMAJI

 

          Awali ya yote, nasikitika sana kwa maamuzi yaliyofikiwa na wajumbe 31 kule Dodoma aidha, kwa hasira, chuki au majungu na kuamua kuniondoa katika wadhifa niliokuwa nao wa Makamu Mwenyekiti Tanzania Bara wakitumia kivuli cha Katiba ya Chama.  Pili nimezidi kuumia zaidi pale nilipotuhumiwa kuwa eti navujisha siri za Chama kwa CCM!  Niliwapa siku Arobaini (40) kuwaza kuthibitisha juu ya tuhuma hizo lakini wameshindwa hadi leo! Inamaanisha kuwa walitumia tuhuma hizo ili kunitoa kati yao ili nisiendelee kutetea ahadi za wanachama wa CHADEMA na nisiendelee kupinga ubadhirifu wa fedha za chama.  Pengine kutokana na hasira, chuki na majungu hayo hayo wakaamua kuzidi kunichafualia jina katika mkutano uliofanyika Tanga kwa kunisema kuwa mimi ni mhuni.  Hapa sintakuwa na huruma wala urafiki na yeyote aliye mstari wa mbele kunichafua kisiasa nitahakikisha nawafungulia mashtaka na waweze kuthibitisha tuhuma hizo.  Mpendwa msomaji, pamoja na hayo ni vyema ukumbuke kuwa, uongozi wa CHADEMA Taifa umeshindwa kukieneza chama hadi vijijini.  Ni kwa ajili ya majungu haya haya!.

 

          Kimsingi, tusiposhikamana kwa sauti moja, lengo moja na kwa msimamo, ni dhahiri kuwa chama cha mapinduzi kitaendelea kushika Dola hadi Ukamilifu wa Dahari!  Chama kisipokuwa madhubuti hakitaweza kushika Dola hakiwezi kuaminika na Wananchi.  CHADEMA tufike mahali tugeuke, tujue tuna lengo la kuiongoza Tanzania na si vinginevyo.  Badala ya kulewa katika kuwafichua mafisadi.  Tumejisahau!.

 

          Naamini kuwa, nguvu za umma ndiyo nguvu inayoweza kuleta mabadiliko ya kweli.

 

          Naamini kuwa, katika chama chochote cha siasa, mwanachama ndiye bora kuliko Kiongozi.

 

          Naamini kuwa msingi bora wa chama hujengwa na watu makini.

 

          Naamini pia baada ya kusoma Jarida hili ukiwa kama mwanachama au Mwanademokrasia utaungana nami katika kupiga vita UFISADI ndani ya CHADEMA.

 

Sakata ya EPA yaelekea kuichanganya serikali

Filed under: habari — tarishi @ 12:01 pm
Na Ramadhan Semtawa 

UCHUNGUZI wa sakata la ufisadi wa zaidi ya Sh 133 bilioni katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), sasa unaichanganya serikali, huku Ikulu na wajumbe wa tume ya Rais ya Uchunguzi wa suala hilo kila mmoja akikwepa kusema lolote.

 

Hali imezidi kuwa tete kutokana na kuwapo kwa taarifa za kukanganya juu ya fedha iliyookolewa na wamiliki halisi wa kampuni 22 zilizochotewa fedha hizo ni nani.

 

Kuna utata pia kwamba, hatua zinazopendekezwa na kuchukuliwa na timu ya uchunguzi, ni ngumu kutekelezwa na huenda sasa serikali inataka kuvuta muda ili suala hilo lipoteze nguvu.

 

Tayari Timu iliyoongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johson Mwanyika, imekwishakamilisha kazi yake na kuandika ripoti zaidi ya siku 21 sasa, lakini habari zinasema kwamba, bado hawajapata muda wa kuiwasilisha kwa Rais Ikulu.

 

Si Ikulu ambao wako tayari kusema lolote juu ya ripoti hiyo wala wajumbe wa timu hiyo.

 

Wajumbe wengine wa timu hiyo ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hosea na Inspekta Jenerali wa Polisi, Said Mwema.

 

Taarifa kutoka vyanzo huru vya habari ndani ya serikali, zinasema hadi sasa, Rais Jakaya Kikwete, anafikiria matokeo ya maamuzi ambayo atachukua baada ya ripoti ya timu aliyounda kutolewa.

 

Kwa mujibu wa taarifa hizo, Rais ana mambo mawili makubwa anayoangalia, moja ni kuona namna gani matokeo ya maamuzi atakayochukua yatakubalika kwa wafadhili ambao wanasubiri kwa hamu kabla ya kuruhusu kutolewa kwa fedha za kusaidia bajeti ya serikali ya mwaka wa fedha 2008/09 walizoahidi.

 

Wafadhili walitoa ahadi ya fedha hizo kiasi cha asilimia 40 cha bajeti ya Sh7.2 trilioni kwa mwaka huu wa fedha, kwa masharti kwamba, fedha halisi zitatolewa kutegemeana na jinsi serikali itakavyoshughulikia mafisadi waliotajwa kwenye ripoti ya Ukaguzi wa EPA iliyofanywa na Kampuni ya Ernst & Young. Msaada huo wa fedha ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

 

Kundi jingine lenye matarajio kama wafadhili, ni wananchi ambao tangu taarifa za ufisadi wa EPA zifichuliwe wamekuwa wakisubiri kwa hamu hatua zitakazochukuliwa hasa baada ya Rais Kikwete mwenyewe kusema kupitia Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo kwamba, walioiba fedha hizo ni lazima wazirejeshe na ikibidi watafilisiwa.

 

Rais Kikwete akitafakari cha kufanya juu ya makundi hayo mawili, yaani wafadhili wanaompa fedha na wananchi ambao walimpa kura zaidi ya asilimia 80 wakionyesha imani kubwa kwake, makundi haya yakifanana kwa matumaini, kwani wanataka mafisadi waadhibiwe, kuna kundi la tatu ambalo ni watu wanaohusika na EPA, wengi wao wakielezwa kuwa karibu ama na watendaji serikalini au chama tawala.

 

Utata mkubwa zaidi wa EPA umeendelea kutanda hasa kutokana na taarifa kwamba, akaunti ya siri ya fedha za EPA ndani ya BoT bado imebaki na fedha kidogo zisizozidi Sh64 bilioni, kiasi ambacho ni chini ya nusu ya fedha zote zilizochotwa kifisadi ambazo ni Sh133 bilioni.

 

Luhanjo alipoulizwa kulikoni hadi sasa serikali imeota matende kuhusu ripoti ya EPA, hakuonekana kufurahishwa na maswali hayo na alitaka Ikulu kutokuulizwa swali hilo, badala yake alisema, suala hilo liko kwa timu ya Rais ambayo mwenyekiti wake ni Mwanyika.

 

Katibu Mkuu Kiongozi Luhanjo, alipoulizwa zaidi kwamba, kumekuwa na taarifa tata kutoka Ikulu, ambayo moja ni ile ya Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu kusema kwamba, muda wa timu hiyo umeongezwa, alijibu: “Hunielewi, leo siwezi kuzungumza na wewe kuhusu EPA, uliza timu.”

 

Kwa upande wake Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndulu, alipoulizwa jijini Dar es Salaam jana, alisema hadi sasa akaunti ya EPA ni siri.

 

Profesa Ndulu alisema, BoT haiwezi kutangaza siri za mteja wake na kuongeza pia kwamba, suala la EPA lipo chini ya timu maalumu, hivyo benki hiyo isingeweza kusema lolote.

 

“Nafikiri subiri timu iseme, sisi tuna akaunti nyingi za serikali, sasa kutaja ipi ni EPA ni kiasi gani cha fedha si sahihi, ni siri, nafikiri subiri timu ifanye kazi kisha itatoa taarifa,” alisema Profesa Ndulu.

 

Hata hivyo, Mwanyika wiki moja iliyopita aliliambia gazeti hili mjini Dodoma kwamba, kwa sasa asingeweza kusema chochote kuhusu EPA.

 

IGP Mwema alipopigiwa simu jana alielezwa kuwa katika mkutano huku simu ya Dk Hosea ikiwa haipatikani.

 

Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, wiki iliyopita wakati akizungumza na mwandishi wa habari hii akiwa bungeni, alisema uchunguzi wa EPA ulikuwa ukiendelea vizuri, lakini akamtaka mwandishi awasiliane na Mwanyika.

 

Wakati kukiwa na mkanganyiko huo, taarifa hizo kutoka duru za serikali zinaeleza kwamba, Rais anaweza kukabidhiwa ripoti hiyo wakati wowote.

 

Hata hivyo, changamoto kubwa kwa Rais Kikwete kwa sasa juu ya EPA ni jinsi ya kuchukua maamuzi, kwani anachelea kama asipowakuna wafadhili na wananchi, serikali yake inaweza kujikuta katika wakati mgumu.

 

Kwa mujibu wa taarifa hizo, Rais pia anafikiria matokeo ya maamuzi ambayo yanaweza kuwa mazito kwa wahusika, ambao baadhi ni watu wake wa karibu na walisaidia kuchangia kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005.

 

Timu ya kuchunguza ufisadi wa zaidi ya Sh 133 uliofanywa na makampuni 22, ilitangazwa na Ikulu kupitia Luhanjo, hapo Januari tisa na kuelezwa kwamba, ilipewa miezi sita, iwe imerejesha fedha hizo taslim au kukamata mali, hata hivyo, hadi sasa hakuna taarifa zozote rasmi kutoka serikalini kuhusu matokeo ya uchunguzi huo.

 

Timu hiyo ilipata kuzungumza na waandishi wa habari mara moja tu, na tangu wakati huo imekuwa ikiendesha uchunguzi wake kwa siri, licha ya Rais alipoiteua kuitaka kutoa taarifa kwa umma mara kwa mara. Haijulikani kama baadaye Rais alibadili mfumo wake wa utendaji kazi kuwa wazi hadi wa siri.

Tahariri Mtanzania Daima leo

Filed under: habari — tarishi @ 11:49 am

 

 

Bado twamsubiri Pinda
MKUTANO wa 12 wa Bunge la Bajeti unaendelea na kimsingi uko katika hatua zake za mwisho mwisho.

Wakati Bunge likielekea ukingoni, Watanzania wengi wanaowasiliana nasi wamekuwa wakiuliza siku ambayo Waziri Mkuu atamaliza kihoro chao kwa kutoa taarifa kuhusu masuala kadhaa muhimu ambayo tumeahidiwa kuwa yatawasilishwa katika kipindi cha hivi karibuni.

Mshawasha huo wa wananchi mbalimbali ambao idadi yao ni kubwa, ndio ambao umetulazimisha kurejea tena na kuikumbusha serikali kuhusu kile wanachokitarajia kutoka kwao.

Miongoni mwa mambo hayo makubwa yanayosubiriwa ni pamoja na utekelezaji wa Azimio la Bunge lililotokana na Ripoti ya Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza utata katika mkataba wa Richmond.

Uzito wa jambo wala hauhitaji maelezo marefu kwani hata Spika wa Bunge wakati akizungumza na wakuu na wahariri wa vyombo vya habari kabla ya Bunge hili kuanza alizungumzia umuhimu wa suala hilo na namna Bunge linavyosubiri kwa hamu ripoti ya utekelezaji kutoka serikalini.

Lakini katika hayo na mengine yote, mtu mwenye kazi nzito atakuwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda, ambaye ndiye kiongozi wa shughuli za serikali bungeni.

Pinda katika hili, yeye ndiye atakayepaswa kutoa ripoti kuhusu utekelezaji wa ripoti hiyo ya Richmond ambayo ilishindwa kukamilika katika Bunge lililopita hata baada ya yeye mwenyewe kuunda kamati yake kufuatilia suala hili.

Mbali ya jambo hili, Pinda atakuwa na dhamana nzito ya kuhakikisha kuwa, anafanikiwa kutimiza baadhi ya ahadi nzito alizopata kuzitoa kuhusu maamuzi ya kiserikali au masuala yanayohusu Bunge.

Kwa mfano, Pinda atalazimika kuwathibitishia Watanzania kwamba kauli aliyoitoa wakati alipokutana na wahariri katika mkutano wake wa kwanza aliofanya nao inathibitishwa.

Naamini wahariri na Watanzania wanakumbuka namna Pinda alivyoahidi kwamba serikali haitakuwa na mzaha wa kuwaacha viongozi ambao watakiuka misingi na maadili ya uongozi.

Katika hili alisema wao serikalini, hawatakuwa tayari tena kuwavumilia viongozi watakaoirejesha nyuma serikali na akatumia maneno makali akisema; ‘tutakufa na mtu’.

Kauli hiyo nzito ya Pinda kwa kiwango kikubwa ilifufua matumaini makubwa ambayo wananchi wanayo kwa serikali ambayo mbali ya Richmond itapaswa pia kutoa maelezo ya namna itakavyotekeleza na kuziba nyufa zilizotokana na kashfa ya EPA iliyoigharimu serikali shilingi zipatazo milioni 133.

Kwa sababu hiyo basi, ni imani yetu kwamba, Pinda ataweza kulieleza Bunge na Watanzania ni kitu gani hasa wamekigundua kuhusu Richmond na hatua ambazo zimechukuliwa au zitachukuliwa dhidi ya baadhi ya viongozi.

Ili kuwarejeshea wananchi imani, Pinda atapaswa kulieleza Bunge na Watanzania hatima ya watendaji kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Dk. Edward Hosseah, ambao bado wanaendelea na kazi hata baada ya kutakiwa kuwajibishwa.

Katika hili serikali itapaswa kutoa ufafanuzi ni kitu gani hasa kilitokea hata kusababisha watu hao pengine waonekane wasio na hatia yoyote kinyume cha kile kilichozungumzwa bungeni.

Hata hivyo wakati serikali ikitoa maelezo yoyote, itapaswa kuangalia na kukumbusha matukio ambayo yalisababisha baadhi ya watendaji serikalini watajwe na watakiwe kuwajibishwa.

Kwa maneno rahisi kabisa ni kwamba, Pinda atapaswa kulinda hadhi yake yeye binafsi, ya serikali na pengine ya Rais Kikwete, ambaye wakati alipoingia madarakani aliwaonya watendaji kuwa makini akisema iwapo mawaziri watakumbwa na fedheha, basi nao watarajie kukumbwa na fagio litakalotokana na matukio ya namna hiyo.

mwakyembe awaondolea uvivu wah. visiwani

Filed under: habari — tarishi @ 11:44 am

MBUNGE wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe (CCM), ameitaka serikali kutoa adhabu kali kwa Naibu Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Ali Juma Shamuhuna na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Ali Pandu Hassan, kwa kuonyesha utovu wa nidhamu kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

Mwakyembe alitaka viongozi hao waadhibiwe kutokana na matamshi waliyoyatoa ndani ya Baraza la Wawakilishi hivi karibuni wakipinga kauli ya waziri mkuu kuhusu hadhi ya Zanzibar katika muungano.

Tamko hilo la Mwakyembe ambaye katika siku za hivi karibuni amepata umaarufu mkubwa kutokana na ripoti ya kamati teule aliyoiongoza kuchunguza kashfa ya Richomond, alionya kuwa endapo viongozi hao hawataadhibiwa, basi ipo siku wanaweza kufikia hatua ya kumnyoshea kidole machoni, Rais wa Jamhuri ya Muungano.

Mwakyembe ambaye alikuwa akizungumza wakati wa kipindi cha maswali ya ana kwa ana kwa waziri mkuu, bungeni mjini Dodoma, alisema kitendo cha mawaziri hao wawili kumpinga hadharani Pinda si tu kwamba ni utovu wa nidhamu, bali pia  kinakwenda kinyume cha agizo lake la kuwataka wanasheria wakuu wa muungano na yule wa Zanzibar kulishughulikia suala hilo linalohusu hadhi ya visiwa hivyo katika muungano.

“Kilichotokea Zanzibar kwa viongozi hao ni utovu wa nidhamu na wanapaswa kuadhibiwa na wasipoadhibiwa, kuna siku watamnyoshea kidole rais mpaka machoni,” alisema Mwakyembe na kushangiliwa na wabunge.

Mbali ya kushangiliwa, wabunge wawili, John Malecela (Mtera – CCM), na Zitto Kabwe (Kigoma Kaskazini – Chadema), waliinuka katika viti vyao na kwenda kumpa mkono wa pongezi Mwakyembe mara baada ya kumaliza swali lake.

Katika hali inayoweza kuonyesha kumuunga mkono Mwakyembe, Mbunge wa Muleba Kusini, Wilson Masilingi (CCM), naye alisema suala hilo lililoanzia bungeni, linapaswa kuwa fundisho kwa Watanzania ambao wanapaswa kumwomba Mungu.

Akielezea kile kilichotokea hata kusababisha Pinda kutoa matamshi hayo, Masilingi alisema waziri mkuu alikuwa ndiye aliyechokozwa na mbunge, ingawa yeye ndiye akaanza kuandamwa baadaye.

“Waziri Mkuu alichokozwa na mbunge mmoja, lakini kesi ikawa ya waziri mkuu. Maandamano yameandaliwa kumpinga bila sababu ya msingi,” alisema Masilingi.

Kabla Masilingi hajamaliza kuzungumza, alisimama Mbunge wa Dimani Zanzibar, Hafidh Tahir (CCM), aliyetaka mwongozo wa Spika, akitaka amzuie Masilingi kuendelea na kauli yake, kwa kuwa tayari Spika mwenyewe ameshatamka kuwa suala hilo linashughulikiwa na wabunge waache kuendelea kujadili na kuliuliza bungeni.

Hata hivyo, Spika alimjibu kwa kusema kuwa: “Bado namsikiliza Masilingi anakwenda wapi, lakini kauli yangu isipotoshwe, kama anatoa ufafanuzi wa kikatiba anaruhusiwa,” alisema.

Kauli hiyo ya Spika ilimfanya Masilingi aendelee kuchangia na kusema kuwa waziri mkuu anapaswa kuungwa mkono kwa nguvu zote, kwani yuko sahihi.

Mbunge mwingine wa Kibakwe, George Simbachawene, (CCM), alipotaka kuzungumzia hoja ya Zanzibar ni nchi au la, Spika alimzuia.

Hoja hiyo ya hadhi ya Zanzibar, ilianzia bungeni wakati Waziri Mkuu, Pinda alipokuwa akijibu swali kuhusu nafasi ya Zanzibar, na akajibu kuwa si nchi, akitumia Katiba ya Jamhuri ya Muungano.

Kauli hiyo ilizua malumbano miongoni mwa Wazanzibari wa makundi tofauti ya kisiasa na kijamii, walioungana kutetea hadhi ya Zanzibar kuwa ni nchi, huku wakiungwa mkono na viongozi wao.

Malumbano kuhusu suala hilo sasa hivi yamefikia hatua ya kuwashawishi watu kuanza kutoa lugha za kuashiria mwelekeo mbaya wa muungano uliodumu kwa miaka 44.

Utata wa malazi wanafunzi mlimani upo pale pale

Filed under: habari ndio hiyo — tarishi @ 11:41 am

Mwanzoni mwa mwezi ujao wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ambao wengi wao wanachukua masomo ya shahada ya uzamili waliokuwa wakiishi katika hosteli za Ubungo wanatakiwa wawe wamehama katika majengo ya hosteli hizo.

Wanafunzi hao takribani 220 wanaondoka katika majengo hayo kupisha walimu wao ambao wameshaanza kupatiwa vyumba viwili kwa kila mwalimu mmoja katika majengo hayo yenye vyumba 36 kwa kila jengo. Majengo hayo ni matatu.

Nilipofanya mahojiano na Ofisa Uhusiano wa chuo hicho cha elimu ya juu nchini, alinieleza lengo la kubadilisha matumizi hayo ni kuwasaidia walimu wao ambao kwa sasa wanakabiliwa na upungufu wa nyumba.

Uamuzi huo kwa upande mmoja ni mzuri unaoonyesha chuo kinawajali walimu wake lakini nikiangalia suala hilo kwa upana zaidi naomba kutofautiana na uongozi wa chuo hicho kwa kufikia uamuzi huo ninaouona unaweza kuwa na hasara zaidi ya faida.

Itambulike kuwa chuo hicho kinapokea wanafunzi wapya zaidi ya 5,000 kila mwaka wakiwamo 3,000 wanaosomea katika kampasi kuu ya chuo hicho. Wanafunzi hao wengi wanatoka mikoa mbalimbali ya Tanzania na wakifika Dar es Salaam wanakuwa wageni.

Kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi wanaosoma chuoni hapo ambao idadi yake inatarajiwa kuendelea kuongezeka katika siku zijazo haiendi sambamba na uwezo wa malazi. Sasa hivi tunaelezwa kuna upungufu wa hosteli za wanafunzi wanaosoma chuoni hapo licha ya kuwapo baadhi ndani ya kampasi kuu na kule Mabibo.

Ikiwa leo uongozi wa chuo unaona busara kuongeza uhaba huo wa hosteli za wanafunzi kwa kuwaangalia zaidi walimu wao ni wazi ni uamuzi wa kibinafsi.
Uongozi wa chuo unaweza kusema si kazi yao kuangalia malazi ya wanafunzi lakini kulingana na mazingira halisi ya hapa kwetu ni wajibu wao kuhakikisha wanafunzi, hasa wanaotoka nje ya Dar es Salaam, wanakuwa na uhakika wa malazi katika kipindi chote cha masomo na si mwaka wa kwanza pekee.

Uamuzi huo wa kubadilisha matumizi ya hosteli hizo tayari umeongeza tatizo la wanafunzi takriban 220 kukosa malazi katika kipindi cha masomo kinachoanza Septemba na tatizo hili limekuwa likikua kutokana na uamuzi wa chuo kubadilisha matumizi ya hosteli za wanafunzi kama ilivyowahi kutokea kubadilishwa matumizi kwa hosteli za Kijitonyama.

Naamini kutatua tatizo la nyumba kwa walimu ni rahisi kuliko kuwapatia malazi wanafunzi kwani wao wakipatiwa posho za nyumba wana uwezo mkubwa wa kwenda mtaani kutafuta nyumba za kuishi na wakaendelea kufundisha chuoni hapo. Hali ni tofauti kwa wanafunzi ambao wengi wao si wakazi wa Dar es Salaam ambao itawagharimu zaidi kupanga chumba au kuweza kujikusanya na kupanga nyumba.

Wanafunzi wanatakiwa kukaa pamoja katika mazingira tulivu ili waweze kujisomea lakini leo wakizagaa mitaani kweli watasoma hao? Hivi tunawajengea mazingira ya kufanya vizuri masomo yao au tunawajengea mazingira ya kuharibikiwa na kuongeza wahuni badala ya wasomi?Nionavyo mimi UDSM iangalie zaidi kupunguza tatizo la hosteli za wanafunzi na si kulizidisha kwa kuwaangalia walimu wao pekee. Iwasaidie pia wanafunzi wao.

Next Page »

Blog at WordPress.com.