Tarishi Hauwawi

July 6, 2010

SEACOM: A CURSE IN DISGUISE???

Filed under: habari ndio hiyo — tarishi @ 10:59 pm

TECHNICAL hitches experienced by Seacom — the first cable to provide broadband to East African countries — have seriously affected communication in the country for the last two days, almost halting business and other operations that rely on internet.

“It is total chaos in the city…there is nowhere to access the internet,” charged Mr Protas Masawe, who was looking for internet connection through a Vodacom modem.

Vodacom so far are the only Internet Service Provider that has not been affected the glitch, the second one this  year, after a simiar hiccup SEACOM wallowed in early this year.

Hundreds of city residents flocked the Vodacom offices along Ohio Street to buy the gadget but were directed to Mwalimu Nyerere Fair grounds along Kilwa road.

Seacom, in a statement posted on its website on Tuesday, blamed submarine failure that started on Monday as a result of “service downtime between Mumbai, India and Mombasa, Kenya.”

The firm said preliminary investigations had indicated that a special gadget — repeater — has failed on segment nine of the Seacom cable, which is offshore to the north of Mombasa.

Seacom said it had initiated emergency repair procedures to replace the repeater.

“Once mobilised, the repair ship is deployed to the location of the fault to pick up the cable. The cable is then brought on board to undergo repairs — the faulty element is replaced with a new repeater — before being put back in the water.”

Whilst the repair process itself takes a few hours, Seacom said the overall process may last a minimum of six to eight days, saying the actual duration was hardly predictable due to external factors like transit time of the ship, weather conditions and time to locate the cable.

“For this reason, the estimated duration of this repair remains uncertain,” said the service provider, assuring however that it was, through co-operation with individual clients, working round the clock to restore the service by Thursday.

The company was also looking for other options to restore the service, pending the repair work.

Seacom is the first provider of broadband to East African countries, where Kenya and Tanzania, South Africa, Mozambique are inter-connected through protected ring structure.

Advertisements

February 23, 2009

Sakata la vyeti feki launguruma kila mahali Tanzania!

Filed under: habari ndio hiyo — tarishi @ 10:44 pm

Naomba ieleweke kuwa kuna makundi mawili hapa tunayoyaongelea: La kwanza ni kundi la akina Mzindakaya, JK , Karume, Rwakatare n.k. Hawa wana shahada za heshima tu (honoris causa) siyo za kusomea! Chuo chochote kinaweza mtunukia mtu shahada hiyo ya heshima kwa kutambua mchango wake katika jambo fulani. Siku za nyuma hata baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, Spika Adam Sapi,

 Salim Ahmed Salim, Kaunda na Obote walipewa heshima hiyo na vyuo mbalimbali duniani. Kundi lenye matatizo ni lile lenye shahada feki na linadai kuzisomea shahada hizo! Kundi hili ni hatari sana maana linaharibu kabisa heshima, sifa na viwango vya elimu nchini.

Wafuatao wana vyeti feki vinavyoitia aibu Serikali na nchi kwa ujumla:

(1) Salmin Amour – Ph.D yake ni feki, ya kisiasa. Aliipata Ujerumani Mashariki enzi hizo kwa miezi mitatu tu huku akiwa na cheti cha form four tu!

(2) Pius Ng’wandu – Ph.D yake ni feki. Chuo anachodai kusoma cha Stanford, Marekani hakina kumbukumbu zake. Aliosoma nao huko Marekani, akina Prof. Baregu, wanajua kuwa ana Masters tu!

(3) Mary Nagu – Ph.D yaje ni ya kununua kwenye mtandao.

(4) Emmanuel Nchimbi – Ph.D yake ya uchumi ni ya kununua. Hana uelewa wowote wa economics kichwani mwake.

(5) Makongoro Mahanga – Ph..D yake ya ugavi ni ya kununua kama Nchimbi.

(6) Didas Masaburi – Ph.D yake ilinunuliwa pamoja na ya kaka yake Makongoro.

(7) Norman Sigallah – Ph.D yake ni ya kununua kwenye mtandao.

(8) Mafwenga – Ph.D yake sawa na ya Sigallah

(9) Nangale – Ph.D yake ni kutoka chuo kimoja bomu cha chini ya viwango, London .

(10) Mathayo David – Ph.D ya kujipachika.

(11) Mutamwega – Ph.D yake ni feki, ya kununua. Mhusika hawezi kuandika hata sentensi moja sahihi ya Kiingereza.

(12) Lukuvi – Masters yake ni feki. Kaipata akiwa na sifa za elimu ya darasa la saba na cheti cha ualimu, class C..

(13) Samuel Chitalilo – Vyeti vyake vya elimu ya juu toka Uganda vyote ni feki. Ana kesi ya kujibu mahakamani!

Nimepata taarifa mbalimbali kuhusu vyeti vya Wabunge wafuatao:

Sigonda,

Capt.Komba,

 Omari Mzeru na Savelina Mwijage.

Nazifanyia kazi. Nitazianika hapa muda muafaka!

Ijabu Ijabu kanipa hamasa sana juu ya suala hili. Wote aliowaeleza kweli wana vyeti feki na hata ukiongea nao, ni vihiyo vihiyo wa kutupwa! Naomba niongeze majina mengine kwenye listi la Mhe. Diodorus Buberwa Kamala, Mbunge wa Mkenge na Waziri wa A. Mashariki. Huyu bwana kasoma Mzumbe kama Nchimbi ambako mtandao wa vyeti feki ulianzia na Mkuu wa Chuo hicho Bw. Warioba. Ph.D yake ni feki, ni ya kununua kama hizo za wenzake aliowataja Ijabu.

Hata kwenye Bunge la A. Mashariki tunaambiwa anapwaya ile mbaya. Naibu wake, Mohamed Aboud, yeye ndo balaa maana ni form four failure na CV yake inasema uongo kuwa ana diploma ya Uingereza! Wote ni Ze Komedi mbele ya Wakenya, Waganda, Warwanda na Warundi!

Yupo huyu mama wa Kibaha, Zaibab Gama. Anajiita Dk. wakati ana diploma ya radiology tu!

Kuhusu Mbunge Savelina Mwijage (Viti Maalum, Kagera), huyu ana matatizo makubwa maana anatumia jina la marehemu. Taarifa zote zilitoka gazetini, lakini analindwa. Hawezi hata kuandika jina lake, lakini ni Mbunge. Anayebisha aje na ushahidi maana huyu mama namfahamu miaka mingi akiwa mfanyakazi wa ndani wa Mhindi Bukoba.

Namfahamu sana Mbunge Sigonda. Ni mtu wa usalama wa Taifa aliyeishia darasa la nane. Leo naambiwa ni Dk.! Hebu tupe dataz Ijabu na wana JF wengine.

Capt. Komba yeye ni msanii na mwizi asiyestahili kujadiliwa hapa maana anawaibia hata wasanii wenzake dani ya TOT. Mzeru wa Morogoro yeye ni mafix moja kwa moja. Hana udaktari wowote! Alijipachika udaktari kuombea ubunge na unaibu waziri kwa JK ! Agustino Lyatonga Mrema – Pacific Western University , a diploma mill. Yeye alipoenda kuchukua hiyo “degree” alikwenda na matarumbeta kibao, vifijo na nderemo.

Mustafa Mkullo – Almeda University , a diploma mill. Kule youngafrican. com nakumbuka ilisema eti chuo chake kiliwahi kutoa associate degree kwa mbwa anayeitwa “Wally” mali ya mwandishi mmoja wa habari huko Marekani (In 2004 the CBS affiliate in Albany , New York , ran a report on Almeda that featured Peter Brancato, who had filled out an application for an associate degree on behalf of his dog, Wally.

Part of the “life experience” listed on the application was “Plays with the kids every day … teaches them to interact better with each other … Teaches them responsibilities like feeding the dog.” Almeda granted Wally an associate’s degree in childhood development with a course list including European culture, college algebra, American history, and public speaking.[13] In reply, Almeda claims Brancato perjured himself by creating a false identity using a fabricated name and date of birth.

They write, “He completed an application that included a background of the following: Eight-years tutoring pre-K children, curriculum design and development, teaching coping skills, and volunteer coaching.”” Almeda University – Wikipedia, the free encyclopedia Kama sijakosea waheshimiwa wengi sana wana degrees kutoka chuo cha Washington International –

 I think even Sofia Simba anayo ya huko Yona Fares Maro Master of Science in Computer Science and Information Systems (MS) University of Michigan-Flint

Thank You

January 3, 2009

MGONJA AUNGANISHWA KESI NA YONA, MRAMBA

Filed under: habari ndio hiyo — tarishi @ 7:00 am

Gray Mgonja

Gray Mgonja

Kesi iliyokuwa inamkabili Katibu Mkuu wa zamani wa Hazina, Gray Mgonja, imefutwa jana, badala yake mshitakiwa huyo sasa ameunganishwa katika kesi inayowakabili mawaziri wawili waandamizi wa zamani Basil Mramba na Daniel Yona.

Kutokana na Mgonja kuunganishwa kwenye kesi hiyo ya kutumia vibaya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya Sh bilioni 11.7, washitakiwa hao waliomba kurudishiwa sehemu ya mali zao walizowekeza kortini kama dhamana.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam haikuwa na pingamizi na iliamua washitakiwa watakuwa nje kwa dhamana ya Sh bilioni mbili kila mmoja au kuwasilisha hati yenye kiasi hicho cha fedha kutokana na idadi yao kuongezeka.

Awali, Mgonja alikuwa nje kwa dhamana ya Sh bilioni 5.9 kutokana na kushitakiwa peke yake na aliwasilisha hati zenye thamani ya Sh bilioni 6.2. Kwa upande wa Mramba na Yona, walikuwa nje kwa dhamana ya Sh bilioni 2.9.

Kutokana na uamuzi huo, washitakiwa watachagua hati ambazo watapenda kuziondoa mahakamani. Tayari Mgonja ameshaomba aondoe hati ya nyumba ya kitalu 29 iliyoko Adda Estate ya thamani ya Sh bilioni 1.7 na hati ya kitalu namba 80 iliyoko Mikocheni yenye thamani ya Sh bilioni mbili.

Hakimu Mkazi Hezron Mwankenja alisema masharti mengine ya dhamana kama kutoruhusiwa kutoka nje ya Dar es Salaam, kukabidhi hati ya kusafiria kwa waendesha mashitaka na masharti mengineyo yatabaki kama yalivyokuwa awali.

Hatua hiyo ya kuunganishwa Mgonja kulifanya upande wa mashitaka kusoma upya mashitaka kwa washitakiwa wote watatu, huku Mramba akiendelea kukabiliwa na mashitaka yote, Mgonja mashitaka manane na Yona akibakiwa na mashitaka sita.

Hata hivyo, mashitaka yaliyosomwa jana na waendesha mashitaka wa Serikali na wale wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), yamepungua kutoka 13 hadi 12. Kesi hiyo itatajwa tena Februari 2, mwaka huu kutokana na upande wa mashitaka kutokamilisha upelelezi wa shauri hilo.

Katika hatua nyingine, Yona na Mramba wameiandikia barua mahakama kuomba waruhusiwe kusafiri nje ya Dar es Salaam. Yona ameomba siku saba kuanzia leo ili asafiri kwenda kwao Same kuwaona wazazi wake ambao wanaumwa.

Mramba ameomba kusafiri kwenda jimboni kwake kuanzia leo hadi Februari mosi ili kutembelea wapiga kura wake. Pia ameomba aruhusiwe kusafiri kwenda katika vikao vya Bunge Dodoma. Bado hajaruhusiwa uamuzi utatolewa Jumatatu.

Mramba na Yona, wote waliowahi kuongoza wizara nyeti ya Fedha, wanatuhumiwa kutumia vibaya madaraka yao waliyokuwa nayo kwa kuipendelea Kampuni ya Alex Stewart (Assayers) ya Uingereza kwa kuipa mikataba minono na baadaye kuisamehe kodi.

Mkataba unaotajwa katika kesi hiyo ni wa kukagua hesabu za kampuni zinazochimba dhahabu nchini; bila kufuata sheria za manunuzi ya umma. Baadaye washitakiwa hao wanadaiwa kuiongezea mkataba wa miaka miwili kampuni hiyo bila kufuata taratibu.

Makosa yanayowahusisha vigogo hao wawili ni ya kutumia vibaya madaraka kwa kusaini na kuingia mkataba na kampuni ya ukaguzi wa hesabu kwenye migodi ya dhahabu nchini kinyume cha sheria ya manunuzi.

Kosa hilo la kuingia mkataba na kuiongezea mkataba kinyume cha taratibu wanadaiwa kulifanya kati ya Juni 14, 2005 hadi Juni 23, 2007.

Kosa la tatu pia linawahusu washitakiwa wote watatu ambao wanadaiwa kati ya Machi 2005 na Mei 28, 2005 wakiwa mawaziri walitumia vibaya madaraka yao kwa kuiachia kampuni hiyo kujiongezea mkataba.

Katika shitaka hilo inadaiwa viongozi hao walimwachia Dk. Enrique Segura wa Alex Stewart kukamilisha mkataba wa kujiongezea miaka miwili kabla ya timu ya serikali kufanya majadiliano juu ya suala hilo.

Washitakiwa hao pia wanadaiwa kati ya Machi na Mei 2005 wakiwa mawaziri, waliliachia suala la udhibiti wa madini ya dhahabu kufanywa kienyeji na kampuni hiyo bila kulipeleka kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kama ilivyoamriwa na timu ya majadiliano ya serikali.

Upande wa mashitaka ulidai kuwa uamuzi wa mawaziri hao uliisababishia Kampuni ya Alex Stewart kuongezewa mkataba wa miaka miwili kabla hata ya suala la ada kuafikiwa na pande zinazohusika pamoja na masuala mengine ya mkataba.

Shitaka la kusababisha hasara ya Sh bilioni 11.7 linawahusu washitakiwa wote watatu ambao wanadaiwa kufanya kosa hilo kati ya Juni 2003 na Mei 28, 2005 wakiwa mawaziri na Katibu Mkuu wa Hazina katika Serikali ya Awamu ya Tatu.

Shitaka la tano linamhusu Mramba na Mgonja wanaoshitakiwa kwa kudharau ushauri uliotolewa na Mamlaka ya Mapato (TRA) wa kuwataka wasiruhusu msamaha wa kodi kwa Kampuni ya Alex Stewart. Mramba na Mgonja pia wanashitakiwa walitoa msamaha wa kodi kwa kampuni hiyo kinyume cha ushauri wa TRA.

Wanadaiwa kutenda kosa hilo Oktoba 10, 2003 na kutoa tangazo la serikali namba 423/2003 la kutoa msamaha wa kodi zote zilizokuwa zinalipwa na kampuni zilizokuwa zinaisambazia vifaa Kampuni ya Alex Sterwart kinyume cha ushauri wa TRA.

Katika kosa lingine Mramba na Mgonja wanashitakiwa kuwa Desemba 19, 2003 wakiwa waajiri wa Wizara ya Fedha walitumia vibaya madaraka yao kwa kutoa msamaha wa kodi kwa kampuni hiyo kinyume na ushauri wa TRA.

Oktoba 15, 2004 Mramba na Mgonja pia wanadaiwa waliipa msamaha mwingine wa kodi kampuni hiyo kinyume cha ushauri wa TRA.

Kosa kama hilo Mramba na Mgonja wanadaiwa kulitenda tena kati ya Oktoba 14 na 15 baada ya kutoa tangazo namba 498/2004 la kuruhusu msamaha wa kodi kwa Kampuni ya Alex Stewart kinyume na ushauri wa TRA.

Katika shitaka la 10 Mramba na Mgonja wanatuhumiwa kutoa msamaha mwingine wa kodi kwa kampuni hiyo. Walitoa msahama huo kupitia tangazo la Serikali namba 377/2005 na kutoa upendeleo huo wa kutolipa kodi kwa kampuni hiyo.

Shitaka la 11 linawahusu Mramba na Mgonja ambao wanadaiwa kutoa msamaha wa kodi kwa Alex Stewart kitendo wanachodaiwa kukifanya Novemba 15, 2005 kupitia Tangazo la Serikali namba 378/2005.

CHADEMA YAPIGWA CHINI MBEYA VIJIJINI

Filed under: habari ndio hiyo — tarishi @ 6:54 am

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imetupilia mbali rufani iliyowasilishwa kwake na mgombea wa ubunge kwa tiketi ya Chadema katika Jimbo la Mbeya Vijijini, ambaye ni Mwanasheria wa Kujitegemea, Sambwee Shitambala na kumuengua kutokana na kukiuka taratibu za sheria katika ujazaji wa fomu za uchaguzi.

Akisoma uamuzi wa tume, Mwenyekiti wa NEC Jaji Lewis Makame alikubaliana na pingamizi zilizowekwa na mgombea wa CUF, Daud Mponzi na wa CCM, Mwanjale Luckson, kutokana na mgombea huyo kuapa kwa wakili kinyume cha Sheria Namba 1 mwaka 1985 inayotaka mgombea aape kwa hakimu.

Alisema katika kifungu cha 38 (3) (a) cha Sheria ya Uchaguzi Namba 1 ya mwaka 1985 kimebainisha tamko la kisheria linalotakiwa kufanywa na mgombea ubunge, kuwa hakimu ndiye anayepaswa kushuhudia tamko la kiapo.

“Na katika Sheria ya Tafsiri (Interpretation of Laws Act, CAP I R. E. 2002) na Sheria ya The Magistrate’s Courts of Laws Act’ CAP 11 R. E. 2002) haijumuishi mtu mwingine isipokuwa mahakimu wa Mahakama za Mwanzo, Wilaya na Hakimu Mkazi,” alisema na kuongeza kuwa ni dhahiri wakili hawapaswi kushuhudia tamko husika.

Alisema kwa kuwa tamko limesainiwa na mtu asiyehusika, ni dhahiri tamko hilo sio halali na ni sababu ya kuweka pingamizi iliyotajwa katika kifungu cha 40 (1) (d) cha Sheria ya Uchaguzi ambayo haimruhusu wakili kusaini tamko hilo.

Aidha, alisema sheria za Oaths and Statutory Declaration Act na The Notaries Public and Commissioners for Oaths, ni sheria ambazo zinahusu viapo na matamko ya kisheria kwa ujumla, na kifungu cha 38 (3) (a) kinahusu tamko la kisheria kwa wagombea ubunge tu.

“Kuna kanuni ya sheria inayosema wakati wowote ambapo sheria ya jumla inapoungana na sheria maalumu, sheria maalumu ndiyo inayopaswa kutumika,” alisema Jaji huyo mstaafu.

Alisema kutokana na maelezo ya kifungu cha 38 (3) (a), sheria za viapo haziwezi kutumika katika suala hilo kwa sababu Sheria ya Uchaguzi ya 1985, imetamka bayana kuhusu ni nani anayetakiwa kushuhudia tamko la kisheria la mgombea ubunge na fomu za kutumika katika matamshi hayo zimebainishwa katika kanuni za uchaguzi wa rais na wabunge za mwaka 2005.

“Fomu inataka jina la Hakimu, Saini yake na Muhuri wa Mahakama,” alisema. Kadhalika alisema wagombea walikuwa na muda wa kutosha ambao wangeweza kuwasilisha viapo vyao kwa mahakimu.

“Makatibu wote wa vyama vya siasa ngazi ya wilaya, walipatiwa barua iliyokuwa inaonyesha wagombea wanatakiwa kuchukua fomu kuanzia tarehe 17 mpaka tarehe 27 Desemba siku ya kurudisha fomu na ya uteuzi,” alisema na kuongeza kuwa wagombea walikuwa na siku sita za kazi za kuwasilisha viapo vyao.

Alisema kutokana na maelezo hayo yaliyozingatia hoja tatu za msingi za mrufani, na kwa kuzingatia uamuzi wa NEC katika rufaa ya Ernest Binna, mgombea wa Ubunge Jimbo la Bunda kwa tiketi ya CUF katika Uchaguzi Mkuu wa 2005, Tume ya Taifa inakataa rufaa ya mgombea wa Chadema, mwanasheria Shitambala.

Akizungumza baada ya rufaa yao kutupiliwa mbali na NEC, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema na Mbunge wa Mpanda Kati, Said Arfi alisema wamepokea uamuzi wa tume na wanahitaji muda wa kutafakari kabla ya kutoa tamko.

“Haya ni maamuzi dhidi ya demokrasia, inawanyima fursa wananchi kuchagua viongozi wao,” alidai Arfi.Wagombea wa vyama vya CUF na CCM viliwasilisha pingamizi dhidi ya mgombea wakiwa na sababu kuu nne likiwamo suala la kiapo ambacho aliapishwa na wakili Evarist Mashiba wa Dar es Salaam, kinyume cha sheria ya uchaguzi.

Uamuzi wa NEC ulifikiwa na majaji wanne akiwamo Jaji Makame; Makamu Mwenyekiti Jaji Omar Makungu; Jaji John Mkwawa na Jaji Mary Longway waliokuwa wajumbe pamoja na Mchanga Mjaka na Hilary Mkate.

Kuenguliwa kwa Chadema kunaacha uwanja wa ushindani kwa vyama vya CCM chenye mgombea Mchungaji Luckson Mwanjale, CUF kikimsimamisha Mhandisi mstaafu Daud Mponzi na mfanyabiashara Subi Mwakipiki kwa tiketi ya SAU.

Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Mbarali amekihama chama hicho na kujiunga na CCM kwa madai kuwa ruzuku za chama hicho zimekuwa zikiishia ngazi ya taifa na kuwatelekeza viongozi wa wilaya.

Akizungumza wakati akirudisha kadi ya Chadema katika mkutano wa hadhara wa Chama Cha Mapinduzi uliofanyika wilayani Mbarali juzi, Mwenyekiti huyo Sethi Kitaule alisema ameamua kukihama chama hicho baada ya kuona viongozi wanaothaminiwa na chama hicho ni wa ngazi ya taifa pekee.

Alidai tangu ajiunge na chama hicho, ruzuku zote zimekuwa zikiishia ngazi ya taifa, tofauti na CCM ambayo imekuwa ikipeleka fedha na kulipa mishahara baadhi ya wafanyakazi wake. “Chadema inatukumbuka pale tu uchaguzi unapokaribia, ukipita hatuwaoni tena,” alidai.

Mbali ya Kitaule, zaidi ya wanachama 30 wa vyama vya upinzani akiwamo Burton Kihaka aliyegombea ubunge kati ya mwaka 2000 na 2005, alisema vyama vya upinzani vinaibuka wakati wa uchaguzi tu hivyo kushindwa kuwasaidia wananchi.

September 14, 2008

Barua ya wazi kwa waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi.

Filed under: habari ndio hiyo — tarishi @ 8:49 pm
Barua ya wazi kwa waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi.

Barua ya wazi kwa waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi.

WAZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
S.L.P. 1921, DAR ES SALAAM – TANZANIA.
                        
YAH: VIVUNGE VYA MWILI WA BINADAMU KWA SHULE ZA MSINGI.
 
Husika na kichwa cha habari hapo juu. Napenda kukufahamisha kuhusu rushwa iliyokithiri ndani ya wizara yako kuhusiana na somo husika hapo juu. Idara yako ya EMAC imetoa ithibati mbili tu kwa kampuni mbili ambazo zote ni mali ya mtu mmoja. Ithibati hizo zimetolewa kwa kampuni za ABACUS LTD na ACADEMIA LTD ambazo zinamilikiwa na mkurugenzi wa Macmillan Aidan Ltd.
 
Napenda kukufahamisha kuwa mgao wa pesa uliotolewa kwa mwaka wa fedha 2008/9 umelenga kuzichota pesa zote (mabilioni) za mradi huu kupitia mlengwa mtajwa na washirika wake waliomo ndani ya wizara yako. Chunguza kwa kina wakurugenzi wa makampuni hayo ni ndugu.
 
Mradi huu ulianzishwa kwa siri bila wizara kutangaza au kukaribisha ushindani wa bidhaa lengwa mpaka makampuni hayo yalipopata ithibati na mgao kupelekwa wilayani. Hii ilifanyika makusudi ili kunyima nafasi kwa mtu yoyote kushiriki. Mradi huu umejulikana baada ya halmashauri kuanza kutangaza zabuni au kuomba quotations na hivyo kutompatia mtu mwingine yoyote nafasi ya kufanya matayarisho katika kuingia kwenye ushindani. Kwani muda hautoshi na yoyote atakaye jaribu kuingia basi atakuwa amechelewa na fedha zote zitakuwa zimekwisha kombwa na mtu huyu mmoja.
 
Tunaomba wizara yako itoe taarifa ni vigezo gani vilivyo tumika kumpatia mtu mmoja nafasi kama hii ya kuzoa mabilioni na kupitia katika utaratibu upi? Pia wizara isitishe zoezi hili mapema iwezekanavyo na kutoa  nafasi ya ushindani na sio uzoaji wa fedha kifisadi kama inavyo endelea. Fanya uchunguzi wa kina kuhusiana na mmiliki huyu wa makampuni haya mawili kwani hizi taarifa sio za kukisia bali ni zenye uhakika na umakini. Tusingepanda kuona wizara yako inageuka EPA au RICHMOND.
 
Fuatilia kwa umakini yafuatayo:-
                                                                                                                                                                                     
1.       Ni lini kampuni hizi zipeleka vivunge EMAC?
2.        Ni lini barua ya muongozo kwa halmashauri ilitolewa?
3.       Ni kigezo gani kilitumika kuzitaarifu kampuni hizi juu ya bidhaa hitaji? (hakuna kampuni nyingine yoyote iliyokuwa na taarifa)
4.       Ni kigezo gani kilichotumika kupanga bei ya bidhaa pasipo kushirikisha kampuni nyingine yoyote zaidi ya kampuni hizi mbili zinazomilikiwa na mtu mmoja?
5.        Ni kwanini barua ya muongozo imetoa nafasi ya kutumia quotation (hii ni kwasababu ya kuharakisha zoezi linaenda haraka ili kutotoa nafasi kwa mtu mwingine yoyote, tenda huchukua muda mrefu).
 
Ni matumaini yetu kuwa haki itatendeka na kuhakikisha ufisadi kama huu haufanyiki tena katika wizara yako.
 
Wako mtiifu,
EDUCATIONAL FUNDS WATCHDOG.
 
cc. TAKUKURU
     OFISI YA WAZIRI MKUU
     TAMISEMI
     USHIRIKA WA VYOMBO VYA HABARI

September 11, 2008

Nape bado anadunda CCM, pamoja na kutimuliwa UVCCM

Filed under: habari ndio hiyo — tarishi @ 6:41 pm
Nape Nnauye akihutubia mkutano wa CCM huko Mysore, India

Nape Nnauye akihutubia mkutano wa CCM huko Mysore, India

 

RAIS Jakaya Kikwete jana alihitimisha kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kutoa tamko lake kuhusu hatima ya kisiasa ya kada kijana wa chama hicho- Nape Nnauye.

Katika hali inayoweza kutafsiriwa kuwa ni ya kuuma na kupuliza, Kikwete, Mwenyekiti wa Taifa wa CCM, alisema uamuzi wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana kumvua Nape uanachama wa jumuiya hiyo, hauwezi kusababisha kada huyo apoteze sifa za kuendelea kushika nyadhifa zake nyingine ndani ya chama hicho.

Habari Tanzania Daima ilizopata, zinaeleza kuwa Rais Kikwete alitoa kauli hiyo jana baada ya vikao vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM vilivyokutana juzi na jana, kushindwa kutoa uamuzi wowote kuhusu mapendekezo ya UVCCM kutokana na kutokuwa na taarifa rasmi kutoka katika jumuiya hiyo ya vijana.

Kwa upande wake, Kikwete alisema nyadhifa zote nyingine ambazo Nape anazishika ni za chama na si za UVCCM, hali ambayo kimsingi inamfanya aendelee kuzishikilia hata baada ya jumuiya hiyo ambayo yeye ni mwanachama kupendekeza anyang’anywe.

Katika hatua nyingine, Rais Kikwete alikaririwa akiwaeleza wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM kwamba Nape bado alikuwa anayo nafasi ya kutoa utetezi wake katika vikao vya juu vya chama kupinga maamuzi ya UVCCM dhidi yake.

Kauli hiyo ya Rais Kikwete imetafsiriwa na baadhi ya makada wa chama hicho waliogawanyika katika makundi mawili – moja likimtetea Nape na jingine likimpinga – kutofautiana maoni kuhusu hatima ya kisiasa ya kijana huyo – mtoto wa mwanasiasa mkongwe – Moses Nnauye.

Kundi la wanasiasa linalomuunga mkono Nape, likijumuisha viongozi wa juu wastaafu na makada wengine wanaharakati wa vita ya ufisadi ndani ya chama hicho tawala, wameitafsiri kauli hiyo ya Kikwete kama inayopingana na ile iliyotolewa juzi na Katibu Mkuu wa CCM, Yussuf Makamba, kwamba kijana huyo alikuwa hana nafasi ya kupinga maamuzi ya UVCCM juu ya uanachama wake mahali pengine popote.

Kwa wale wanaompinga Nape na kuungana na maamuzi ya Baraza Kuu la UVCCM linaloongozwa na Emmanuel Nchimbi, wanaitafsiri kauli hiyo ya Kikwete kuwa ilitolewa kwa nia ya kumpoza pasipo kumsaidia kwa lolote mwanasiasa huyo kijana, ambaye ni miongoni mwa watu wanaowania kuteuliwa kugombea nafasi ya uenyekiti wa taifa wa jumuiya hiyo katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.

Akizungumza na Tanzania Daima kwa simu kutoka Dodoma, Nape mwenyewe aliielezea kauli hiyo ya Kikwete aliyoitoa wakati yeye mwenyewe akiisikia kuwa ni ya faraja na iliyomrejeshea matumaini na imani mpya.

Nape alisema kauli hizo za Kikwete zinaendelea kumfanya aendelee kujiona kuwa yeye ni mwanachama wa UVCCM, mjumbe wa Baraza Kuu la jumuiya hiyo, Mjumbe wa NEC, ofisa katika ofisi ndogo ya Makao Makuu ya CCM Dar es Salaam na bado ni mgombea halali wa nafasi ya mwenyekiti wa UVCCM.

“Kwa hiyo, ninachoweza kusema ni kuwa nasubiri barua ya UVCCM nione inasemaje, ili nijue namna nitakavyokata rufaa, lakini nimefurahi kitu kimoja kwamba mwenyekiti anasema naweza kukata rufaa, wakati Katibu Mkuu, Makamba, alisema siwezi kukata rufaa popote. Hilo kwangu naona ni ushindi na haki imetendeka kama nilivyotarajia,” alisema Nape kwa sauti ya kujiamini.

Katika hatua nyingine pia inayoweza kuthibitisha kuwa Nape alikuwa na hoja katika malalamiko yake, Kamati Kuu ya CCM iliyokutana juzi, iliamua kuunda timu ya makada watatu kufuatilia mchakato na kufanya marekebisho katika mkataba wa ujenzi wa jengo la UVCCM.

Habari ambazo Tanzania Daima ilizipata kutoka ndani ya Kamati Kuu (CC) na baadaye kuthibitishwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Ferouz, zilisema timu hiyo inawajumuisha wajumbe wa Kamati Kuu – Mbunge wa Handeni, Dk. Abdallah Kigoda, Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge, na Mbunge wa Viti Maalumu, Pindi Chana.

Kwa mujibu wa habari hizo, timu hiyo inatakiwa kufanya marekebisho katika kasoro zilizopo na baadaye kuwasilisha mapendekezo yake ndani ya vikao vya UVCCM vya Kamati ya Utekelezaji, Baraza Kuu kwa ajili ya kusainiwa.

Hatua hiyo ya CC kuunda timu ya kufanya marekebisho ya kasoro katika mradi huo, imepokewa na mashabiki wa Nape kuwa ni ushahidi wa kwanza wa kuwapo kwa ukweli katika madai ya kijana huyo aliyekuwa akisema kuwa mkataba huo hauna maslahi ya UVCCM na CCM kwa ujumla.

Uamuzi huo wa kuundwa kwa timu na Kamati Kuu umetafsiriwa na baadhi ya mashabiki wake kwamba unaweza kumpa fursa nzuri ya kujitetea kupinga maamuzi ya UVCCM dhidi yake.

Nape alivuliwa uanachama na Baraza la UVCCM kwa madai ya kusema uongo kuhusu mradi huo wa jengo la UVCCM na ikidaiwa kwamba kwa kuwatuhumu viongozi wa jumuiya hiyo hadharani na nje ya vikao, alikuwa amekwenda kinyume na Kanuni za 17 (C) na18 (B) za umoja huo.

Tangu Baraza Kuu la UVCCM limvue Nape uanachama, mawaziri wakuu wawili wastaafu kwa nyakati tofauti – Cleopa David Msuya na Frederick Sumaye – wamejitokeza kumtetea, wakiielezea hatua hiyo kuwa ni ya jazba na iliyochukuliwa kwa hamaki.

August 21, 2008

JK ANGURUMA BUNGENI NA KUWEKA MAMBO SAWA

Filed under: habari ndio hiyo — tarishi @ 10:15 pm
President Jakaya Kikwete arrives at the National Assembly to address legislators and the Nation.

President Jakaya Kikwete arrives at the National Assembly to address legislators and the Nation.

Baada ya kutembelea tovuti zote za Tanzania nimegundua ni www.dailynews-tsn.com ambayo imeweza kukidhi sehemu ya kiu ya wananchi kujua Raisa Kikwete anazungumza nini huko Bungeni Dodoma. Na hii imekuja kwa msaada wa blogu ya issamichuzi.blogspot.com ambayo imeelekeza mamilioni ya wasomaji wake kwenda kuona video za hotuba hiyo iliyokuwa ikisubiriwa kwa udi na uvumba na wa-Tanzania wote

August 18, 2008

Mwakyembe awasha moto Zanzibar

Filed under: habari ndio hiyo — tarishi @ 6:50 am
Mh. Harrison Mwakyembe akiwa na Mh. Hawa Ghasia

Mh. Harrison Mwakyembe akiwa na Mh. Hawa Ghasia

   
*SMZ yataka aombe radhi wananchi
*Mwenyewe asema:Sitabadili kauli
*Hati za Muungano sasa zatoa jibuNa Waandishi Wetu Zanzibar, Dar

KAULI iliyotolewa bungeni wiki hii na Mbunge wa Kyela (CCM), Dkt. Harrison Mwakyembe kuwa mawaziri wa Zanzibar wanaoendelea kudai Zanzibar ni nchi ni watovu wa nidhamu, imezidi kuwasha moto na sasa S.M.Z imetoa tamko rasmi ikimtaka mbunge huyo si tu awaombe radhi mawaziri bali pia wananchi wote wa visiwa hivyo.

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) katika ‘kupambana’ na mbunge huyo pia sasa imeibua jipya ikisema kauli ya Dkt. Mwakyembe ni sawa na uchochezi na kejeli.

Msimamo huo rasmi wa SMZ umetolewa jana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Kiongozi. Bw. Hamza Hassan Juma aliyeweka bayana kuwa anawasilisha tamko la Serikali, alipozungumza na waandishi wa habari.

“Mheshimiwa Mwakyembe tunamheshimu sana kama ni mwanasheria…..lakini inaonesha wazi amekiuka maadili kwani matamshi aliyotoa ni kejeli kubwa kwa mawaziri wa SMZ na kusisitiza Serikali haiwezi kukaa kimya katika suala hilo,” alisema.

Hamza ambaye ni mjumbe wa Baraza la Wawakilishi kutoka jimbo la Kwamtipura, alisema mawaziri wa SMZ kamwe hawawajibiki kwa Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda wala Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“SMZ haiwajibiki kwa Bunge…hapa kipo chombo chake cha kutunga sheria-Baraza la Wawakilishi….wadhifa wa Pinda sawa sawa na wa Waziri Kiongozi Shamsi Nahodha,” aliongeza Bw. Hamza.

Akichangia hotuba ya Wizara ya Sheria na Katiba katikati mwa wiki hii, Dkt. Mwakyembe ambaye ni mtaalamu wa sheria za katiba aliyehitimu shahada yake ya Udaktari wa Falsafa (Ph. D) kutoka Chuo Kikuu cha Hamburg, Ujerumani, alisema kitendo cha baadhi ya mawaziri wa Zanzibar kupingana na Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda ni kejeli dhidi ya kanuni ya kikatiba ya uwajibikaji wa pamoja wa mawaziri.

Naibu Waziri Kiongozi wa Zanzibar, Bw. Ali Juma Shamhuna, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Bw. Idd Pandu Hassan, baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Bunge la Muungano ni miongoni mwa wanasiasa wa Zanzibar waliokuwa wakilumbana na Bw. Pinda wakisisitiza kuwa Zanzibar ni nchi inayojitegemea.

Dkt. Mwakyembe ambaye kati ya mwaka 2001 na 2005 alikuwa mshauri wa sheria wa Chama cha Mapinduzi (CCM) NA Kamishina visiwani Zanzibar akisaidia kujenga utawala bora na kuimarisha katiba, katika mchango wake huo bungeni, alitaka viongozi hao wa Zanzibar wachukuliwe hatua kwa kubishana hadharani na Waziri Mkuu wa Muungano.

Hamza akizungumzia kauli hizo za Dkt. Mwakyembe, aliongeza kuwa wameamua kumtaka Mbunge huyo si tu kuwaomba radhi mawaziri wa Zanzibar bali kufanya hivyo kwa wananchi wote wa visiwa hivyo.

Alipoulizwa, Dkt. Mwakyembe alijibu kwa kifupi, akionekana kupuuza shinikizo hizo kwa kusisitiza kuwa hatafuta kauli yake aliyoitoa Bungeni.

Naye Naibu Spika wa Bunge, Bibi Anne Makinda alipoulizwa kuhusu kanuni za Bunge zinasemaje kuhusu shinikizo anazopewa Dkt. Mwakyembe, alimtaka mwandishi azitafute ili ajionee mwenyewe.

Kisheria, kauli inayozungumzwa Bungeni ina kinga ya kutohojiwa katika chombo chochote cha kisheria hata hivyo uamuzi wa Spika katika shauri la Reginald Mengi na Mbunge Adam Malima, pamoja na kusisitizia kinga hiyo ulielezwa kuwa mwananchi wa kawaida aliyeumizwa na kauli iliyotolewa bungeni, anaweza kuwasilisha malalamiko yake kwa Spika.

Katika hatua nyingine, wakati sakata hilo likichukua sura mpya, uchunguzi wa Majira Jumapili, umebaini kuwa pamoja na wanasiasa wa Zanzibar kushupalia kuwa visiwa hivyo ni nchi, Hati za Muungano ambazo gazeti hili limefanikiwa kuziona, zinasisitiza kuwa April 26, 1964 iliundwa nchi moja ya muungano.

Kwa mujibu wa hati hizo ambazo kwa sasa ni sehemu ya sheria iitwayo ‘The Union Between Tanganyika and Zanzibar Act (no. 22) 1964, kifungu cha 4, kinatamka bayana kuwa nchi iliyoundwa ni moja.

Kifungu hicho kinasema: ” Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, zitaungana na kuunda nchi moja; Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar’.”Baadaye jina la jamhuri hiyo lilibadilishwa na kuitwa Tanzania.

Uchunguzi zaidi umebaini kuwa utata wa Zanzibar kuwa nchi au la pia ulishatatuliwa na Mahakama ya Rufani katika hukumu yake ya Novemba 21, 2000 katika kesi ya S.M.Z. vs. Machano Khamis Ali & Others (Criminal Application no. 8 of 2000), ambapo Jaji Augustino Ramadhani katika sehemu ya hukumu hiyo alisema:

“Ni vyema tukabaini ibara hiyo (ya 103 ya katiba ya Muungano) inabainisha wazi kuwepo kwa kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na si Kiongozi wa Nchi ya Zanzibar ingawa Kiongozi huyo wa Serikali ya Mapinduzi anaitwa Rais.

“…Hili linafupisha mjadala na kufikisha hoja ya dhahiri kuwa Zanzibar si nchi, si tu kwa mujibu wa sheria za kimataifa bali pia hata kwa mujibu wa katiba ya Muungano.”

August 15, 2008

Mbowe afanyia sherehe kifo cha Wangwe

Filed under: habari ndio hiyo — tarishi @ 1:03 pm

Mwenyekiti wa Chadema Mh. Freeman Mbowe

Mwenyekiti wa Chadema Mh. Freeman Mbowe

Na Tarishi, magazeti

 

 

 

MWENYEKITI wa CHADEMA, Bw. Freeman Mbowe, anadaiwa kufanya hafla kubwa Afrika Kusini saa chache baada ya kupata taarifa za kifo cha Makamu wake, marehemu Chacha Wangwe.Habari zilizopatikana kutoka hoteli ya Garden Court jijini Johanesburg ilikoifanyika hafla hiyo Julai 29 mwaka huu, zilisema baada ya Mwenyekiti Mbowe kupokea taarifa za msiba, alifanya hafla ya kuwaaga wajumbe aliokuwa nao huko ili arejee nchini kwa mazishi.

“Kwanza taarifa ilipopatikana, hakututangazia mpaka tulipopata kutoka kwa vyanzo vyetu vingine ndipo tukathibitisha naye…akatuandalia hafla jioni ya siku hiyo,” kilidai chanzo cha habari hii.

Kilidai kuwa kilishangaa kuona katika mazingira yale ya majonzi, kuandaliwa hafla kubwa namna ile.

“Tulishangaa na kumuuliza kwa nini hafla ile, akatujibu kuwa alikuwa akituaga, kwani anarudi nchini kushiriki mazishi ya marehemu Wangwe,” kiliongeza chanzo hicho.

Kilidai kuwa hata wajumbe wa vyama vya siasa waliokuwa nchini humo kuhudhuria semina ya vyama vyenye wabunge Afrika, walipotaka kumchangia rambirambi, hakutaka kuipokea na badala yake kuwaambia kila mmoja ataje kiwango naye atawalipia.

“Tulitaka kumchangia fedha za rambirambi mwenzetu huyo, lakini hakuonesha nia ya kuzipokea na badala yake akatuambia kila mmoja ataje kiwango chake naye akifika Tanzania ataziwasilisha msibani,” kilidai chanzo hicho.

Wajumbe tisa kutoka Tanzania walikuwa wakiongozwa na Bw. Mbowe katika semina hiyo ya siku nne ya kujifunza jinsi Tume Huru ya Uchaguzi inavyofanya kazi nchini Afrika Kusini.

Chanzo hicho cha habari kilisema semina hiyo ilikuwa ni kwa ajili ya makatibu na naibu makatibu wa vyama vya siasa nchini, lakini walishangaa kumwona Mwenyekiti wa CHADEMA naye akishiriki.

“Yawezekana alialikwa, lakini mbona wenyeviti wenzake hawakualikwa, tulijiuliza sana lakini tukaacha mambo yaendelee hivyo hivyo,” kilidai chanzo hicho.

Pia wanasiasa hao walikutana na viongozi wa chama tawala cha Afrika Kusini cha African National Congress (ANC).

Wajumbe waliohudhuria semina hiyo ni wawili kutoka CHADEMA, wawili CCM, mmoja mmoja CUF, TLP, Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Tume ya Haki za Binadamu na Mkurugenzi wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD).

Bw. Mbowe alipoulizwa kuhusiana na madai ya kuwaandalia tafrija baadhi ya watu aliokuwa akihudhuria nao mkutano huo, kabla ya kurejea Dar es Salaam kuhudhuria msiba wa marehemu Wangwe, alijibu:

“Hao waliokuambia ni akina nani! Waambie wakuthibitishie maana siwezi kuingia kwenye malumbano ya mambo ambayo hayakuwapo.”

Alipoulizwa ilikuwaje akahudhuria mkutano huo wakati ulikuwa ni kwa ajili ya makatibu wakuu na manaibu wao kutoka vyama vyenye wabunge, Bw. Mbowe alisema alipewa mwaliko wa kuhudhuria mkutano huo.

“Mimi nilialikwa na watu TCD kuhudhuria mkutano huo,” alisisitiza Bw. Mbowe alipozungumza na gazeti hili kwa njia ya simu.

Akizungumzia madai kuwa alikataa michango waliyotaka kutoa baadhi ya washiriki aliokuwa nao kwa ajili ya rambirambi na badala yake kudaiwa kuwataka watoe ahadi zao na akifika Dar es Salaam atawatolea, Bw. Mbowe alijibu:

“Wewe zungumza na vyanzo vyako hivyo vikuthibitishie  kama hayo yalitokea.”

Bw. Mbowe alimtaka mwandishi wa habari hizi kuwauliza watu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) au CCM au TCD kama kweli hayo yalitokea au la kwa sababu nao walihudhuria mkutano huo.

 

Chacha Wangwe aibuka toka kuzimu

Filed under: habari ndio hiyo — tarishi @ 12:15 pm

Hayati Chacha Wangwe

Hayati Chacha Wangwe

JARIDA LA CHACHA ZAKAYO WANGWE MBUNGE WA TARIME CHADEMA

 

 

 

Utangulizi:

 

Jarida hili la Mheshimiwa Chacha Zakayo Wangwe lina sehemu tatu.  Sehemu ya kwanza litaweka bayana na kufafanua sababu za mimi kuchafuliwa kisiasa na baadhai ya viongozi wa ngazi za juu za Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, na sehemu ya pili itaonyesha baadhi ya maswali ya msingi niliyopata kuuliza Bungeni na majibu yake na sehemu ya tatu itakuwa na michango mbalimbali niliyopata kuchangia kwa muda wa miezi miaka miwili na nusu.

 

Lengo hasa la Jarida hili ni kumwelewesha Mtanzania na hususan MWANADEMOKRASIA juu ya tuhuma zilizoelekezwa kwangu kwa lengo la kunichafua kisiasa huku viongozi wa CHADEMA wakidai kukisafisha chama jambo ambalo si kweli na ni kampeni chafu zilizoandaliwa na baadhi ya viongozi wa Chama na kuwarubuni wajumbe 31 wasiokuwa wanademokrasia na kunipaka matope ya siasa zao zisizo na hata chembe ya Demokrasia.

 

Nasema hivi nikijua wazi kwamba, CHADEMA kama chama kinaendeshwa kwa katiba na kwa wakati huo huo kikiwa kinaendeshwa kidikteta na kauli za NDIYO MZEE.  Ninajua wazi kwamba, viongozi wa sasa wa chama changu wanatofautiana sana na viongozi wa mwanzo wakati CHADEMA ikianzishwa kwani wanatofautiana kiitikadi, kisera na hata kimtazamo.  Kwa mfano, mzee Mtei alikuwa akikieneza chama hasa vijijini miaka ya 95 kwa kutumia magari chakavu na alifanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwashawishi wananchi na wakijua kuwa CHADEMA si chama cha mjini, na hapa ndipo mwanzo wa CHADEMA kuwa Chama Tawala kule Tarime hadi sasa.  Ila katika uongozi huu wa kizazi kipya basi kila kitu kinaenda kwa kauli za “Mheshimiwa Mwenyekiti kasema” na matumizi mabaya huku ufisadi ukikitafuna chama kwa matumizi hewa na kwa kigezo kuwa eti wanajilipa madeni ya Kampeni.  Nililia sana juu ya matumizi ya helkopta katika kampeni lakini nikaanza kuonekana kuwa mini ni mbaya.  Binafsi sikuona sababu za Chama kutumia helkopta ilhali bado wanachama wa vijijini hawakijui chama wala sera zake huku viongozi wa wilaya na mikoa wakishindwa hata kutoa durufu (photocopy) za viepeperushi vya chama kwa kukosa ruzuku.  Hii si sawa.

 

SEHEMU YA KWANZA

 

Sababu za baadhi ya Viongozi wa CHADEMA kuamua kunichafua kisiasa.

 

          Baadhi ya Kampeni za chini chini dhidi yangu, tarehe 28 na 29 Juni 2008 katika kikao cha Kamati Kuu kilichofanyika Dodoma ambacho kiluhudhuriwa na wajumbe 31 kiliridhia mimi kuondolewa kwenye wadhifa niliokuwa nao ndani ya chama kama Makamu Mwenyekiti kwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutuhumiwa kuwa navujisha siri za chama kwa CCM.  Binafsi kwangu kama mwanasiasa wa kiwango cha juu ni pigo kubwa sana kisiasa kuchafuliwa na watu 31 tu ndani ya chama.  Ninachokiamini hapa ni kwamba, kutokana na msimamo wangu wa siku nyingi hata kabla sijawa makamu mwenyekiti CHADEMA, ndiyo sababu rasmi ya kupigiwa kampeni na baadaye kura za kutokuwa na imani na mimi kwa taarifa nilizo nazo ni kwamba anaandaliwa Dr. Slaa kushika nafasi hiyo.  Hapa ikumbukwe kuwa Mke wa Dr. Slaa ni diwani kupitia CCM hivyo kuna uwezekano wa sera za chama zikavuja kupitia Mama huyu katika njia mbalimbali.

 

Ofisi ya Katibu Mkuu (Ofisi ya Slaa) ndiyo ya kwanza kunituhumu kuwa nawaingilia majukumu yao katika suala zima la matumizi mabovu ya fedha za ruzuku ya chama.  Chama hupata zaidi ya milioni 60 kila mwezi.  Ni fedha nyingi sana kukijenga chama kama zikipata mipango mizuri na kuachana na matumizi mabovu kama matumizi ya helkopta kwenye kampeni kama ilivyotokea kwenye chaguzi zetu pamoja na baadhiya viongozi kudai kuwa wanajilipa madeni waliokikopesha chama wakati wa kampeni za 2005.

 

Mhe. Philemon Ndesamburo Mbunge wa Moshi Mjini inadaiwa kuwa anakidai chama milioni 100 alizokopesha wakati wa kampeni za 2005.

 

          Mhe. Philemon Ndesamburo Mbunge wa Moshi Mjini inadaiwa kuwa anakidai chama milioni 100 alizokopesha wakati wa kampeni za 2005, Freeman Mboe ambaye hadi sasa ni Mwenyekiti wa chama changu katika ngazi ya Taifa naye kwa taarifa nilizo nazo ni kwamba kila mwezi hulipwa shilingi milioni 10 ili kufidia fedha anazodai kukikopesha chama ambazo ni zaidi ya milioni 500 katika kampeni hizo hizo na hadi sasa anaendelea kukidai chama mamilioni ya shilingi.

 

          Mimi nilipoonyesha wasiwasi juu ya madeni haya yasiyoisha, ikaundwa tume ya kampeni za kutokuwa na imani na mimi.  Binafsi sijui kama viongozi wanaojiita makini kama kina Dr. Slaa na Kabwe Zitto wangeweza kuusimamia ufisadi mkubwa kama huu ndani ya chama huku wakiwa mstari wa mbele kuwafichua mafisadi Serikalini.  Au ni kawaida kuwa Mganga hajigangi?  CHADEMA kuna ufisadi wa aina nyingi sana kuanzia uchapaji bendera hadi manunuzi ya vifaa vya chama!

 

          Katika ofisi ya Vijana nako kunanuka ufisadi kwani ni vijana wachache sana ambao hupata nafasi ya kwenda nje ilhali mikoani nako kuna vijana wanaohitaji kujifunza.  Ofisi hii ina watu maalumu wa kwenda kwenye Semina na Matamasha mbalimbali.  Na watu hao hupangwa na John Mnyika.

 

          Pamoja na hayo, Kurugenzi hii inayoendeshwa na John Mnyika imekuwa ikifanya hesabu za “Mbili mara Mbili toa nne”.  Nakumbuka matamasha mbalimbali yaliyowahi kuratibiwa na Kurugenzi hii kwa kutumia fedha za chama yamekuwa hayana maslahi yoyote kwa chama ….labda kwake mwenyewe kwani itakumbukwa kwamba Kurugenzi ilizindua mfuko ulioitwa Tumaini jipya Septemba 16, 2007 katika hafla ya wafanyakazi vijana na akaunti ya Tumaini Jipya 01810301 NBC ilifunguliwa.  Jumla ya shilingi milioni 6,176,500 zimekusanywa na shilingi milioni 6,064,300 zimetumika kwa shughuli mbalimbali za vijana ikiwemo gharama za hafla yenyewe.  Hafla nyingine kama hiyo ilifanyika Arusha.

 

          Hafla hii ilifanyika tarehe 29 Machi, 2008 The New Polygon Triangel Arusha na kuhudhuriwa na washiriki 67 mgeni rasmi akiwa Mhe. Mzee Edwin Mtei.  Jumla ya shilingi milioni 2,300,700 zilikusanywa na shilingi milioni 1,885,000.  Zimetumika kwa shughuli mbalimbali za vijana ikiwemo gharama za hafla yenyewe.  Sasa najiuliza, kulikua na mantiki gani ya kutumia fedha za chama kiasi cha shilingi 6,064,300 na kukusanya shilingi 6,176,500/=?  Ni faida ya shilingi ngapi ilipatikana kama ameamua kukiingiza chama katika kufanya biashara ya matamasha?

 

          Jingine, tangu nimekuwa mbunge Chadema na Baadaye Makamu Mwenyekiti sijawahi kuandaliwa safari za kibunge ama za kukiwakilisha chama ilhali kuna watu wasio na uwezo kiakili, kifikra na hata nafasi za uongozi lakini waliandaliwa safari za nje.  Chama kimefikia hatua ya kuwakilishwa kimataifa na watu wasio na vigezo kwa ajili ya utawala mbovu!  Siandiki haya kwa kuwa nimeondolewa katika uongozi, hapana!  Hizi ni harakati zangu za muda mrefu juu ya utawala bora.  Tazama, wafuatao wamewahi kusafiri katika mataifa mbalimbali kwa shughuli mbalimbali kukiwakilisha chama.  Mhe. Suzan Lymo (Mb. Viti maalumu) Cape Towan, Afrika Kusini kwa Mkutano wa Interparliamentary Union.  Susan pia amesafiri kwenda USA kwa High Level meeting ya HIV/AIDs mwezi June, 2008.  Mhe. Zitto Kabwe, (Mb) alisafiri kwenda Berlin mara mbili – Mhe. Zitto pia alisafiri kwenda Marekeani kwa wiki 3 kwa mwaliko wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani pamoja na Wabunge vijana toka dunia nzima ambako walipata nafasi ya kutembelea majimbo mbalimbali ya Marekani.  Mhe. Mhonga Said (Mb – Viti maalum)  alisafiri kwenda Burundi kwa Mkutano wa Nchi za Maziwa Makuu.  Mhe. Dr. Slaa amesafiri kwenda Johannesburg, Windhoek na Manzini Swaziland kwa vikao vya Kamati na Bunge la SADC.  Dr. Slaa ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya InterParliamentary Cooperation Committee ya Bunge la SADC.  Mhe. Maulida Komu (Mb. Viti Maalumu)  alisafiri kwenda Nairobi na pia Finland.  Mhe. Ndesamburo (Mb) alisafiri kwenda Australia kama Commissioner wa Bunge.

 

          Wafuatao walisafiri kichama;  Mhe. Mhonga Said (Mb – Viti Maalum), Maulida Komu (Mb – Viti Maalum), Suzan Kiwanga (Afisa Msaifizi Idara ya Uchaguzi na Kampeni) na John Mnyika Mkurugenzi wa Idara ya Vijana) walisafiri kwenda Norway na Sweden.  Anthony Komu (Mkurugenzi wa Fedha na Utawala)  alisafiri kwenda Norway kwa mwaliko wa Centre Party, Mhe. Balozi Ngaiza (Mjumbe wa heshma wa kamati kuu wa kuteuliwa na Mwenyekiti), John Mnyika (Mkurugenzi katika Ofisi ya Vijana), John Mrema (Afisa katika Kurugenzi ya Halmashauri na Bunge), walisafiri kwenda Windhoek Namibia kwa Mkutano wa Dua, na Mhe. Kimesera (Katibu Mtendaji wa kuteuliwa na Mwenyekiti), Suzan Lymo (Mb) Viti maalum, na John Mrema walisafiri kwenda Kampala, Uganda kwa Mkutano wa Dua.

 

          Ndugu Regia Mtema (Afisa katika Kurugenzi ya Vijana) alisafiri kwenda Malawi kwa Mkutano wa NIMD.  Mama Naomi Kaihula (Mkurugenzi katika Idara ya Wanawake) na Regia Mtema walisafiri kwenda Finland kwa mwaliko wa Shirika la Demo Finland.  Johna Mrema, Msafiri Mtemelwa na Happiness Mwaipopo (Sina hakika kama ni Mwanachama) walisafiri kwenda London/Uingereza kwa mwaliko wa Conservative Party/WFD wakati wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.  Mhe. Benson Kigaila (Mkurugenzi wa Oganaizesheni na Mafunzo) alienda Zimbabwe katika uchaguzi uliofanyika 27 June, 2008 kupita Ofisi ya Msajili wa Vyama.

 

          Suala la ukabila ni jambo ambalo halihitaji kupingwa kwani asilimia karibu 85 ya viongozi wa CHADEMA wametoka katika mikoa ya Kilimanjaro na Arusha pamoja na kwamba baada ya mimi kulishupalia jambo hili wameanza kubadilisha majina.

 

          Wapo wanachama kama mimi ambao nao wakipewa nafasi za uongozi ndani ya chama hiki watafanya vizuri zaidi ya hawa na wengine ambao ni Jobless!  Pengine niweke wazi hapa kuwa, mimi ni kiongozi shupavu nisiye kuwa na hata chembe ya woga katika kuteta na kusimamia haki za mwanachama wa CHADEMA tena nisiyependa siasa za kisanii.  Ukweli huu ndio uliowafanya kina Mbowe, Slaa kuwa mstari wa mbele katika kupiga kampeni na baadaye kura ya kutokuwa na Imani na mimi.  Binafsi naamini katika chama cha siasa mtu muhimu ni Mwanachama na si Mwenyekiti au Katibu.  Hapa mimi siandiki maneneo haya kukufanya udhani kuwa nataka kuwa king’ang’anizi kwenye wadhifa niliovuliwa, la hasha bali napenda upate picha halilisi ya uendeshwaji wa Siasa ya CHADEMA na kisha uweze kugundua uhalisia wa mgogoro ulivyo.  Viongozi wa CHADEMA Makao Makuu wamening’oa kutoka katika wadhifa niliokuwa nao kwa sababu zao binafsi na si sababu za chama kama chama, na wanajitahidi kuzunguka mikoani kwa siri kuendelea kunichafua kisiasa kuwa sifai.  Kweli sifai kwa wafuja ruzuku ya chama, kweli sifai kwa mafisadi ndani ya chama ila nafaa kukiendesha chama katika ngazi ya taifa katika nafasi yoyote na siku zote.  Nafaa kwa sababu nimefukuzwa kwa kusema ukweli hivyo nikageuka mwiba kati kati ya majipu, nikatolewa.  Ndiyo, nafaa kwa sababu siko tayari kufanya kazi na watu waliozoea kukaa ofisini kama mafaili!  Nafaa kwa sababu mimi ni mpambanaji, kamanda shujaa niliye tayari kuwajibishwa kwa ajili ya kuwatetea WANADEMOKRASIA hususan WANACHADEMA nchi nzima.

 

          Kuliendesha Taifa kama Tanzania hakuhitaji siasa za kisanii, fitina, na chuki.  Kinachotakiwa ni nani abadilike alete mabadiliko katika siasa ili aweze kukabidhiwa dola na alete mabadiliko.  Wananchi wamechoshwa na siasa zetu ndio maana wanaziita siasa za kisanii.  Wanahitaji mabadiliko.  CHADEMA maana yake ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo, lakini huku wanakoelekea tayari uongozi wa Mbowe na Slaa wameiondosha Demokrasia kwa kunitoa katika wadhifa wa umakamu Mwenyekiti kwa kupiga kampeni ndogo ya wajumbe 31 tu! Tena huku wakinituhumu kuwa navujisha siri za chama!!.  Dhahama kama hii siwezi kuivumilia hata kidogo na ni wazi kuwa hata wanachama wetu hawajafurahishwa na jambo hili.  Mimi nilipokuwa kwenye ngazi hiyo ndipo fedha zilipoanza kupelekwa mikoani kwa viwango halali, ndipo ukarabati wa Makao Makuu ulifanyika.  Niweke wazi hapa kuwa, jambo lililonifanya niandike jarida hili si kuwashawishi Freeman Mbowe na Slaa kunirudisha kwenye nafasi waliyonitoa kwa matusi, la hasha!  Lengo ni kuweka wazi kwa wanachama wajue aina ya uongozi uliopo Makao Makuu ya Chama. Kama ni suala la mimi kurudi katika nafasi hiyo ni mimi mwenyewe nikiamua na kwa kutumia Demokrasia.  Ikumbukwe kuwa, Freeman ndiye aliyesema kuwa hataki kufanya kazi na mimi na kutokana na UMANGIMEZA na Kauli za NDIYO MZEE akapata kuungwa mkono na wajumbe 31 tu!  Baada tu ya mimi kutangazwa kuwa nimetolewa kwenye wadhifa niliokuwa nao nilipata simu nyingi sana za wanachama na hata baadhi ya watendaji Makao Makuu wakiniambia kuwa kama Mbowe hayuko tayari kufanya kazi na mimi, wao bado wananihitaji katika Uongozi Taifa.  Kuna mila ya kichagga kuwa, katika eneo la kazi/biashara, ukimuona anayekusababisha ukose maslahi Fulani unatakiwa kumuondoa kwa gharama yoyote! Na hili ndilo lililojiri kwangu na mwenyekiti wangu.

 

Aluta Continue…………………..

 

Wangwe Chacha Zakayo,

Mbunge wa Tarime-CHADEMA

 

 

KAULI YANGU KWA MSOMAJI

 

          Awali ya yote, nasikitika sana kwa maamuzi yaliyofikiwa na wajumbe 31 kule Dodoma aidha, kwa hasira, chuki au majungu na kuamua kuniondoa katika wadhifa niliokuwa nao wa Makamu Mwenyekiti Tanzania Bara wakitumia kivuli cha Katiba ya Chama.  Pili nimezidi kuumia zaidi pale nilipotuhumiwa kuwa eti navujisha siri za Chama kwa CCM!  Niliwapa siku Arobaini (40) kuwaza kuthibitisha juu ya tuhuma hizo lakini wameshindwa hadi leo! Inamaanisha kuwa walitumia tuhuma hizo ili kunitoa kati yao ili nisiendelee kutetea ahadi za wanachama wa CHADEMA na nisiendelee kupinga ubadhirifu wa fedha za chama.  Pengine kutokana na hasira, chuki na majungu hayo hayo wakaamua kuzidi kunichafualia jina katika mkutano uliofanyika Tanga kwa kunisema kuwa mimi ni mhuni.  Hapa sintakuwa na huruma wala urafiki na yeyote aliye mstari wa mbele kunichafua kisiasa nitahakikisha nawafungulia mashtaka na waweze kuthibitisha tuhuma hizo.  Mpendwa msomaji, pamoja na hayo ni vyema ukumbuke kuwa, uongozi wa CHADEMA Taifa umeshindwa kukieneza chama hadi vijijini.  Ni kwa ajili ya majungu haya haya!.

 

          Kimsingi, tusiposhikamana kwa sauti moja, lengo moja na kwa msimamo, ni dhahiri kuwa chama cha mapinduzi kitaendelea kushika Dola hadi Ukamilifu wa Dahari!  Chama kisipokuwa madhubuti hakitaweza kushika Dola hakiwezi kuaminika na Wananchi.  CHADEMA tufike mahali tugeuke, tujue tuna lengo la kuiongoza Tanzania na si vinginevyo.  Badala ya kulewa katika kuwafichua mafisadi.  Tumejisahau!.

 

          Naamini kuwa, nguvu za umma ndiyo nguvu inayoweza kuleta mabadiliko ya kweli.

 

          Naamini kuwa, katika chama chochote cha siasa, mwanachama ndiye bora kuliko Kiongozi.

 

          Naamini kuwa msingi bora wa chama hujengwa na watu makini.

 

          Naamini pia baada ya kusoma Jarida hili ukiwa kama mwanachama au Mwanademokrasia utaungana nami katika kupiga vita UFISADI ndani ya CHADEMA.

 

Next Page »

Blog at WordPress.com.