Tarishi Hauwawi

May 4, 2009

MAELEZO YA MHESHIMIWA ROSTAM AZIZ KWENYE MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI, JUMAPILI, 03 MEI, 2009

Filed under: habari — tarishi @ 6:20 am

Mheshimiwa Mbunge wa Igunga Rostam Azizi

Mheshimiwa Mbunge wa Igunga Rostam Azizi

Ndugu zangu waandishi wa habari,

 

Naomba nianze kwa kuwashukuru nyote kwa kupokea mwaliko wangu wa kuwaita katika mkutano huu na pia kwa kuja kwenu hapa kunisikiliza. Nataka niwahakikishie kuwa nathamini sana heshima hiyo mliyonipa. 

Nimeitisha mkutano huu kufuatia tuhuma nzito, ingawa ni lazima niseme pia ni za kipuuzi, zilizotolewa na Mwenyekiti wa IPP, Reginald Abraham Mengi, dhidi yangu na wafanyabiashara wengine wanne akituhusisha na kile alichokiita “mafisadi papa“, alizozitoa wakati akilihutubia Taifa kupitia kituo chake binafsi cha televisheni cha ITV tarehe 23 Aprili, 2009. 

Mara baada ya kutoa matamshi yake, nilihojiwa na baadhi ya vyombo vya habari vilivyonitaka nitoe maoni yangu. Niliwaambia kuwa sitaki kujibizana na mzee mwenye umri mkubwa unaozidi hata wa baba yangu. Hata hivyo, baada ya kupata nafasi ya kuangalia mkanda mzima wa maelezo yake, na kuona athari mbaya ya uzushi, chuki na sumu iliyomo, nimeona kuna haja ya Watanzania kuufahamu ukweli hasa ulivyo. 

Naelewa kwamba tayari Serikali na vyombo vyake vimeshatoa kauli za kumuonya Mengi kuhusu kauli alizozitoa. Waziri wa Nchi anayeshughulikia Utawala Bora, Mheshimiwa Sofia Simba, amemtahadharisha Mengi kwamba kitendo chake cha kutumia vibaya vyombo vyake vya habari kuwachafua washindani wake wa kibiashara hakikubaliki. Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa George Mkuchika, amesema Wizara yake inafanya uchunguzi wa matamshi ya Mengi kwa kuupitia mkanda wenye maelezo yake na ikibainika amevunja sheria atachukuliwa hatua. Waziri Mkuu, Mheshimiwa Mizengo Pinda, amemuonya dhidi ya kuwahukumu watu ambao kesi zao bado zinaendelea Mahakamani. Na Jeshi la Polisi nalo limeeleza kumshangaa kwake Mengi kutokana na siyo tu kutowasilisha ushahidi wa shutuma zake kwa vyombo vinavyohusika lakini pia kumueleza Mengi kuwa hana jipya alilosema zaidi ya kurejea mambo yaliyokwisha fanyiwa au yanayoendelea kufanyiwa kazi na vyombo vinavyohusika. Pamoja na kuheshimu na kuthamini maelezo hayo ambayo yamemuumbua Mengi lakini bado nahisi binafsi nina wajibu wa kutoa maelezo ya kina kuhusu kiherehere hiki cha Mengi. 

Kwanza, nataka niweke wazi kwamba tuhuma zote zilizotolewa na Mengi dhidi yangu ni za uongo na ni upuuzi mtupu. Tuhuma hizo ni mwendelezo wa wimbo ule ule ambao amekuwa akiuimba kwa muda mrefu sasa na tayari nilikwishazitolea kauli huko nyuma. Nilipofanya mkutano na waandishi wa habari kama huu mwaka jana, nilisema wazi kwamba sihusiki na tuhuma zote zinazoelekezwa kwangu na nikatoa changamoto kwamba iwapo wale wanaotoa na kusambaza uzushi huo wana ushahidi wa wale wanayoyasema, basi kwa sababu nchi yetu inafuata utawala wa sheria, walipaswa wapeleke ushahidi wao katika vyombo vinavyohusika ili sheria ichukue mkondo wake. Hakuna aliyefanya hivyo. 

Hata baada ya Mengi kurudia tuhuma hizo wiki iliopita, nilimpa taarifa kupitia vyombo vya habari niliyoitoa tarehe 29 Aprili, 2009, nikimtaka ndani ya siku mbili (2) awe amewasilisha kwenye vyombo vya sheria vinavyohusika ushahidi wa tuhuma zake dhidi yangu kwamba mimi ni fisadi na kwamba mimi ni muuaji ninayepanga mauaji dhidi yake na watu wengine aliowaita “watu waliojitolea kupambana na ufisadi”. Kama akishindwa kufanya hivyo, basi aniombe radhi hadharani. Na nilimwambia wazi kuwa asipofanya mojawapo kati ya hayo, nitakuwa na haki ya kumuanika ili Watanzania waelewe tabia na hulka ya mtu huyu. Hakufanya chochote kati ya hayo. Na hawezi kufanya hivyo kwa sababu anaelewa kuwa alichokisema ni uzushi alioutunga mwenyewe. Ni kutokana na kushindwa kwake kuwasilisha ushahidi huo ndiyo maana nimeona sasa nifanye mkutano huu ili kuweka kumbukumbu sahihi. 

Nimetafakari kwa kina athari zinazoweza kulifika Taifa letu ikiwa mwenendo wa watu kama Mengi kujipa haki ya kuchafua wale anaowaona ni washindani au wapinzani wake utaachiwa uendelee, na hasa kutokana na sumu mbaya iliyomo katika maelezo anayoyatoa na malengo aliyoyakusudia kwa kutoa maelezo hayo. Nimeona sitakuwa natenda haki kwangu, kwa familia yangu, kwa wapiga kura wangu wa Igunga, kwa Chama changu cha CCM, na kwa Watanzania wenzangu kwa ujumla iwapo nitakaa kimya.  

Kuendelea kwangu kukaa kimya kunaweza kukapelekea Watanzania wakaziamini propaganda chafu za Mengi zenye dhamira potofu na ovu kwa nchi yetu. Kwa hivyo, kama mzazi na kama mwanafamilia kwa upande mmoja, na pia kama Mbunge, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM ambazo zote ni nafasi za kuchaguliwa nilizopewa kutokana na kuaminiwa na wale walionichagua kwa kura nyingi, nina wajibu wa kukemea uchafu na uovu unaotaka kupandikizwa na Mengi ambaye watu wanajiuliza amepata wapi uhalali wa kujifanya msemaji wa Watanzania wakati hawajawahi kumchagua katika nafasi yoyote na hivyo hana ridhaa yao. 

Taifa letu limepita katika vipindi vingi vya majaribio makubwa lakini limebaki kuwa taifa imara na la kupigiwa mfano katika Bara la Afrika. Tanzania ni nchi ambayo bado wananchi wake wanapambana kuyaondoa matatizo makubwa ya umasikini, ujinga na maradhi lakini inasifika duniani kote kwa umoja na mshikamano wa watu wake, na amani na utulivu walioujenga. Haya yamefikiwa kutokana na misingi madhubuti iliyojengwa na waasisi wa Taifa hili. 

Leo hii anapokuja mtu kama Mengi ambaye kutokana na tamaa, uroho, wivu, chuki, fitina, ubaguzi na ubinafsi uliovuka mipaka alio nao na kujipa jukumu la kuivunja misingi hii, sidhani itakuwa ni haki kuendelea kukaa kimya na kumwacha afanikishe malengo yake hayo. Hatuwezi kukaa kimya maana kufanya hivyo kutakuja kuligharimu vibaya sana Taifa letu. 

Historia ya Mengi inamuonyesha kwamba ni mtu anayependa kuanzisha ugomvi katika mambo yanayohusu maslahi yake binafsi lakini unapopamba moto na kuona anazidiwa, hutafuta hifadhi kwa kulia lia na kutaka aonewe huruma na kutaka kuliingiza Taifa zima. Katika kufanikisha hayo, amekuwa akitumia vyombo vyake vya habari kuwapotosha wananchi ili waone anaonewa au eti anapigania maslahi yao. 

Ameanzisha ugomvi na watu wa kada mbali mbali kuanzia Maaskofu hadi kikundi cha wachekeshaji cha Ze Comedy. Huyo ndiye Reginald Abraham Mengi.  

 • Alianzisha ugomvi na wamiliki wa vituo vya televisheni vya DTV na CTN mwaka 1994 kwa hofu tu ya kwamba watakuwa washindani wa kituo chake cha ITV na akafika hatua ya kuwazushia kwamba wanataka kumuua, akaufanya ni ugomvi wa nchi nzima.
 • Alianzisha ugomvi na aliyekuwa Waziri wa Utawala Bora, Mheshimiwa Wilson Masilingi, baada ya kushindwa zabuni ya ubinafsishaji wa Hoteli ya Kilimanjaro, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima. Katika kudhihirisha jinsi alivyo mtu wa chuki na visasi, kutokana na kuikosa tu hoteli hiyo, amekuwa hakanyagi na hata hashiriki shughuli yoyote inayofanyika katika hoteli hiyo.
 • Akaanzisha ugomvi na aliyekuwa Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda, Mheshimiwa Shamim Khan, kwa kutakiwa afute maelezo katika maji ya kunywa yanayozalishwa na kampuni yake kwamba yalikuwa ya chemchem wakati hayakuwa hivyo, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.
 • Akaanzisha ugomvi na aliyekuwa Waziri wa Mazingira, Mheshimiwa Edward Lowassa, aliyemkanya Mengi asitumie nafasi yake kama Mwenyekiti wa Baraza la Mazingira kuwakomoa washindani wake wa biashara kwa kuwazushia tuhuma za kuchafua mazingira na kuvifungia viwanda vyao, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.
 • Akaanzisha ugomvi na aliyekuwa Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Basil Mramba, baada ya kumnasa akikwepa kodi katika uendeshaji wa biashara yake ya bahati nasibu ya BINGO, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.
 • Akaanzisha ugomvi na kampuni ya Habari Corporation iliyokuwa inaongozwa na Jenerali Ulimwengu baada ya kufichua habari za jinsi alivyoifilisi benki ya NBC, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.
 • Akaanzisha ugomvi na mfanyabishara Yusuf Manji ambaye kwanza walikuwa wakigombea uendeshaji wa mchezo wa bahati nasibu, na baadaye akajenga chuki naye binafsi kwa sababu tu alifanikiwa kuusuluhisha mgogoro wa Yanga ambao Mengi ulimshinda, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.
 • Akaanzisha ugomvi na Mheshimiwa Adam Malima ambaye alihoji Bungeni jinsi Mengi anavyotumia vibaya vyombo vyake vya habari kwa kutangaza habari za kujitukuza binafsi zaidi ya hata vinavyotangaza habari zinazowahusu viongozi wa kitaifa, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.
 • Akaanzisha ugomvi na mfanyabiashara Tanil Somaiya baada ya kumuona kijana huyo aliyekuwa wakala wa kuuza bidhaa za viwanda vyake Mengi (kabla ya kuviua mwenyewe), ameweza kujiimarisha na kupata mafanikio makubwa ya kibiashara hata kumshinda yeye Mengi, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima. 
 • Akaanzisha ugomvi na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mheshimiwa Lawrence Masha, kwa kuja na madai ya kutaka kuhujumiwa, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima. Na orodha hii inaendelea na inaendelea.
 • Sasa ameanzisha ugomvi na mimi, baada ya kuona kwamba mimi nimekuwa mshindani wake mkubwa katika umiliki wa vyombo vya habari hapa nchini, anataka pia kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.
 • Huyu ndiye Reginald Abraham Mengi.

 

Tena kwa jinsi alivyo mtu wa visasi na chuki, akishajiingiza katika ugomvi na watu, huhakikisha kuwa habari za watu hao hazitangazwi wala kuandikwa katika vyombo vyake vya habari. Kama ni kutangazwa au kuandikwa basi huwa ni kwa kuwashambulia binafsi na kuwachafulia majina tu. 

Hivi ni kwa nini tuendelee kumvumilia mtu kama huyu? Kwa nini anapokuwa na matatizo yake binafsi na wale anaowaona wabaya wake kibiashara au pengine hata kisiasa aiingize nchi nzima na wananchi wote? 

Nimeamua kuitisha mkutano huu ili kuwaeleza, na kupitia kwenu kuwaelewesha Watanzania, wamjue Reginald Abraham Mengi katika sura yake halisi na dhamira zake chafu na ovu, na kumtambua kwamba mtu huyu ni nyangumi wa ufisadi katika nchi hii. Nimeamua kuwaondolea Watanzania ngozi yake ya kondoo aliyojivika ili waweze kuiona sura yake halisi ya mbwa mwitu anayojaribu kuificha. Nafanya hivi ili kulinusuru Taifa lisije likatumbukia kule Mengi anakotaka kulipeleka. 

Wanasaikolojia wanasema mtu anapotuhumu wengine kuwa na tabia fulani, mara nyingi huwa yeye ndiye mwenye tabia hizo. Hiyo ndiyo hali halisi inayoonekana kwa Mengi kutokana na yale aliyoyasema katika mkutano wake na waandishi wa habari. 

Ukweli wa mambo unathibitisha kwamba ni yeye ndiye mwenye kuhusika na yote hayo aliyotutuhumu sisi kuwa nayo. Hapa nitatoa mifano michache tu ya ufisadi mkubwa sana wa mtu huyu. 

Reginald Abraham Mengi, nyangumi wa ufisadi, alianza kuifisidi nchi kwa kushiriki katika vitendo vya ufisadi vilivyochangia kuifilisi iliyokuwa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), ambayo ni mali ya Watanzania na hatimaye kupelekea kubinafsishwa kwake kwa bei poa. Akitumia kampuni yake ya Anche Mwedu Limited (AML), alichukua mkopo mwanzoni mwa miaka ya 80 wa mabilioni ya shilingi ambayo amegoma kuyalipa hadi leo na kulazimisha suala hilo kufikishwa Mahakamani.  

Mkopo wa kwanza ulikuwa kupitia Akaunti Nam. 6543000020 (uliotolewa kupitia Overdraft Agreements) ambao ulifikia jumla ya shilingi 3,255,429,100.75 ambao hadi Januari 1996 ulifikisha riba ya shilingi 1,737,862,471.75.  

Mkopo wa pili chini ya kampuni hiyo hiyo (kupitia Loan Agreements) ulikuwa ni kupitia Akaunti Nam. 10430000008 ambao ulihusu jumla ya shilingi 386,746,631.06 hadi kufikia Januari 1996. 

Mkopo wa tatu ulihusu Akaunti Nam. 654300584 (kupitia utaratibu wa Government Guarantee) ulikuwa wa jumla ya shilingi 1,803,137,210 hadi kufikia Januari 1996. 

Na wa mwisho kupitia utaratibu wa heading interest on jotter/suspense account ulikuwa wa jumla ya shilingi 417,689,254.10 hadi kufikia Januari 1996. 

Jumla ya fedha zote za NBC ambazo akidaiwa Mengi kupitia kampuni yake ya Anche Mwedu Limited (AML) hadi kufikia Januari 1996 zilikuwa ni 5,863,002,196.45. Fedha hizi hadi kufikia sasa 2009 pamoja na hesabu ya riba zinafikia takriban bilioni 28. 

Hivi ndivyo Mengi alivyochangia kuifilisi NBC, benki ya wananchi masikini wa Tanzania. Fedha hizi zilizochukuliwa na Mengi, shilingi bilioni 28, zinaweza kujenga shule za sekondari 100 ambazo zingeweza kuwanufaisha watoto wa kimasikini wa Tanzania. 

Ukiacha ya NBC, Mengi huyu anayetaka aonekane ni msafi kiasi cha kujipa uthubutu wa kuwatukana watu wengine kuwa ni mafisadi, alichukua fedha nyingi kupitia msaada wa nchi wafadhili wa “Commodity Import Support” ambazo hakuzilipa hadi leo. Hizi ni fedha zilizotolewa kwa njia ya mkopo ili kuwasaidia wafanyabishara kuweza kuagiza bidhaa na zinaporejeshwa ziwasaidie wananchi kwa kuendeleza miradi ya maendeleo hapa nchini kama vile ujenzi wa shule na zahanati. Wafanyabishara wengi tulikopa lakini tumelipa na tunaendelea kulipa. Mengi anayedai ana uchungu na Watanzania anawaongezea umasikini kwa kuchota fedha hizo na baadaye kuruka na kukataa kuzilipa hadi leo. Kati ya fedha hizo ambazo Mengi alichukua ni kama ifuatavyo: 

 

 
Mfuko
 
Kampuni
 
Fedha zilizochukuliwa
Norway CIS 1988/89 IPP – Anche Mwedu NOK (M) 6.00
Norway CIS 1989/90 IPP – Anche Mwedu NOK (M) 4.00
EEC CIS 1988/89 Bonite Bottlers EEU (M) 0.5199
Japan CIS 1991/92 Bonite Bottlers JY (M) 160.000
Japan CIS 1991/92 Medicare JY (M) 115.000
Canada CIS 1988/89 Anche Mwedu C$ (M) 0.5
Italy CIS 1988/89 Anche Mwedu LIRA (M) 1,774.50
Japan CIS NPG–9-1997 Anche Mwedu JY (M) 20,000,000
Japan CIS NPG–5-1994 Bonite Bottlers JY (M) 160,000,000

 

Fedha hizi zilizo katika sarafu tofauti za kigeni zikibadilishwa kwa shilingi za Tanzania pamoja na riba kwa miaka yote tokea zilipochukuliwa zinafikia mabilioni ya shilingi. Na hizi ni sehemu tu ya fedha zote alizochukua ambazo kumbukumbu zake tumeweza kuzipata baada ya kumbukumbu nyengine kupotea katika mazingira ya utatanishi. Badala ya kurejesha fedha hizi alizozikwapua robo karne iliyopita, Mengi alizitumia kujitajirisha.  

Kuonyesha jinsi alivyobobea katika ufisadi, Mengi alikula njama na kushirikiana na afisa mmoja wa Hazina kutengeneza barua ya eti kuthibitisha kwamba alishalipa fedha hizo huku akijua kuwa hakulipa chochote. Pakifanyika ukaguzi huru hata leo hii itathibitika kwamba hakulipa fedha hizo na iwapo anakanusha haya, namtaka akubali kufanyika ukaguzi huo huru. Mtu yeyote wa kawaida angeshangaa Mengi amepata wapi utajiri alio nao katika kipindi kifupi namna hii lakini vielelezo hivi vinatoa majibu ya uhakika. 

Tukiacha ufisadi huo, Mengi kwa kutumia nafasi yake kama Mwenyekiti wa Kamati ya Uwekezaji yenye wajumbe watatu (3) tu ya kampuni ya NICO ambayo ni kampuni iliyoanzishwa kusaidia Watanzania kuwekeza katika biashara na viwanda, amefanya ufisadi mkubwa kwa kukiuka maadili ya kibishara pale alipoitumbukiza kampuni hiyo katika kununua hisa kwenye kiwanda cha Interchem Pharma Ltd kinachomilikiwa na familia ya Mengi, wakati akijua kwamba kiwanda hicho kilikuwa njiani kufilisika. 

Huku akijua hali mbaya ya kiwanda hicho alitumia nafasi yake kuziteketeza Shilingi bilioni 2.558 fedha za Watanzania masikini wasiopungua 22,000 wenye hisa katika NICO kwa kuifanya inunue asilimia 51 ya hisa (majority shareholding). Kiwanda hicho sasa kimewekwa kwenye orodha ya kufilisiwa baada ya kushindwa kujiendesha chini ya mwaka mmoja tokea Mengi kuizamisha NICO. 

Mfanyabishara wa kawaida tu anayeheshimu maadili hawezi kufanya utapeli kama huu kwa kampuni ya wananchi masikini aliyopewa dhamana ya kusimamia uwekezaji wake. Akiwa mhasibu na mfanyabiashara alijua kuwa kiwanda hicho kinakufa lakini alitumia hila na ujanja wa kusuka mipango yote ya kuiingiza NICO katika hasara ili kunusuru kampuni ya familia yake. Ukweli huu unabainishwa katika kitabu cha Prospectus cha NICO cha Oktoba 2007. Kama amebaki na chembe ya aibu, Mengi anapaswa arejeshe fedha hizi za wanahisa wa NICO. 

Ufisadi mwengine wa dhahiri uliofanywa na Mengi ni pale alipoingia ubia na Serikali katika umiliki na uendeshaji wa kiwanda cha TANPACK Industries Ltd. Bila ya kumjulisha mbia mwenzake yaani Serikali, Mengi kisiri siri alitumia dhamana ya TANPACK kwenda kukopa shilingi milioni 600 kutoka benki ya NBC na kuzitumia kwa njia anazozijua yeye. Benki hiyo ilipochachamaa kutaka ilipwe fedha zake, Mengi alitaka TANPACK ilipe lakini Serikali, ikiwa mbia, ilikataa kulitambua deni hilo ambalo haikulijua. Matokeo ya ufisadi huo wa Mengi, TANPACK ikafilisiwa na kufa. 

Huyo ndiyo Reginald Abraham Mengi, nyangumi wa ufisadi, katika sura yake halisi. Anawahujumu maskini huku akijidai kwamba anawaonea huruma. Mtu muadilifu hawezi kusema anawatakia wananchi masikini mema huku anafanya maovu kama haya yanayovuruga misingi ya kusaidia masikini hao hao. 

Lakini mbali na hayo, ngoja niwachekeshe kwa kuwaeleza jinsi mtu huyu alivyokubuhu katika kujenga chuki na fitina kwa kujifanya mtetezi wa wale anaowaita “wazawa“, huku akiwa na lengo la kujinufaisha binafsi kwa kutumia mgongo wa chuki na fitina hizo anazopandikiza. Mwaka 1994, alitoa kauli zake zenye sumu ya ubaguzi pale alipodai kwamba sehemu kubwa ya maeneo ya katikati ya Jiji la Dar es Salaam inakaliwa na Watanzania wenye asili ya Kiasia na kwamba “wazawa“ hawapo katika maeneo hayo. Aliyekuwa Rais wakati huo, Mzee Ali Hassan Mwinyi, akamuagiza Waziri aliyekuwa akishughulikia masuala ya ardhi, Mheshimiwa Edward Lowassa, kumpatia Mengi eneo kubwa la ardhi katikati ya jiji karibu na ilipo International House. Lakini mara tu alipopewa eneo hilo akaliuza kwa Fida Hussein, mfanyabishara Mtanzania mwenye asili ya Kiasia. Huyo ndiye Reginald Abraham Mengi, nyangumi wa ufisadi. 

Biashara pia ina maadili yake na mwenendo wa mfanyabiashara na biashara zake unaweza kuonyesha ni kwa kiasi gani anafuata au hana maadili. Mambo kadhaa ninayoyafafanua hapa chini yanatoa mwongozo wa kumjua vyema Mengi: 

 1. Inafahamika kwamba utajiri wote wa Mengi ameupata katika kipindi cha kama miaka minane, kuanzia 1984 hadi 1992. Watanzania wanapaswa wajiulize amewezaje kuwa tajiri ghafla katika kipindi hicho kifupi? Lakini hata baada ya kuupata utajiri huo, sasa biashara zake zinasuasua na zimeanguka. Amewezaje kuvurugikiwa kiasi hicho? Kwa mtu yeyote anayeelewa misingi ya biashara atafahamu kwamba Mengi hana uwezo wa kuendesha biashara. Utajiri wake ulitokana na kukwapua fedha kupitia mipango ya ujanja ujanja na kutolipa madeni. Haya yalifanyika huku kumbukumbu zake zikipotea katika mazingira ya ajabu ya majengo kuungua na nyaraka kupotea. Alijifaidisha kwa fedha hizo na sasa zimemalizika. Amebaki kulia wivu na kuonyesha chuki kwa njia ya kutaka kuwakomoa wale anaowaona wamefanikiwa katika uendeshaji wa biashara. Asichokielewa ni kwamba baadhi yetu hatukuamka tu na utajiri bali tumetokana na familia zenye rekodi ya kujishughulisha na bishara tokea mwaka 1852 huko Tabora.

 

 1. Dalili nyengine ya ufisadi wa Mengi ni rekodi yake ya kuua kampuni zake. Ni vyema ikaeleweka kuwa mfanyabiashara makini na anayezimudu biashara zake hawezi kuua kampuni. Mfanyabiashara huua kampuni kwa ama lengo la kukwepa kodi, au kukwepa kulipa madeni, au ameshindwa kibiashara na hivyo hawezi kuiendesha tena kampuni yake. Katika kipindi chake kifupi cha kujishughulisha na biashara, Mengi ameshaua kampuni nyingi.  Baadhi tu ya kampuni alizoziua ni pamoja na Tanzania Kalamu Industries Ltd., Anche Mwedu Ltd., TANPACK Tissue Industries Ltd., Chemical Industries Ltd., Bodycare Ltd., na Medicare Ltd. Hebu tujiulize ni kwa nini Mengi anaua kampuni zake halafu anatafuta mchawi kwa wale waliofanikiwa? Bila shaka ameziua kampuni hizo kwa lengo la kukwepa kulipa kodi na kulipa madeni, mambo ambayo ni ufisadi mkubwa. Binafsi sina mchezo wa namna hiyo.

 

 1. Mfanyabiashara mzalendo pia hupimwa kwa utashi wake wa kulipa kodi na kutoa ajira za uhakika kwa wananchi wenzake. Kama unawatakia heri na ni mtetezi wa wananchi masikini kama Mengi anavyotaka aonekanwe basi utatoa ajira za kudumu na za uhakika, na utalipa kodi ambayo malengo yake ni kuiwezesha Serikali kuhudumia masikini hao kwa kuwapatia matibabu na madawa katika hospitali, watoto wao kupata elimu bora na yenye manufaa, kujengewa miundombinu na hata kupatiwa chakula ikibidi pale nchi inapokumbwa na ukame au njaa. Kama unawadhulumu wananchi masikini kwa kutowapa ajira za kudumu na badala yake kuwaajiri kama vibarua wa siku na kama hulipi kodi unawezaje kusema unawasaidia wananchi wanyonge? Mengi anafahamika kwa kutimua wafanyakazi kila mara na kutowalipa haki zao na pia kukwepa kodi huku akidai kwamba kampuni zake siku zote zinapata hasara. Huu ni udanganyifu kwa sababu kama kampuni hizo zinapata hasara haya mamilioni ya fedha anazodai kuzitoa kama michango anazipata wapi? Katika kuendeleza udanganyifu wake na kujaribu kuchezea akili za Watanzania, Mengi amekuwa anakwepa kodi ambazo zingeweza kutumiwa kusaidia kuwaondoshea matatizo wananchi walio wengi na badala yake amekuja na mtindo wa kualika walemavu wachache na kuwapa chakula na kisha kuvitumia vyombo vyake vya habari kwa staili ya Kim Jong Il, Kiongozi wa Korea Kaskazini, ya kusifiwa na kutukuzwa kwa kuandikiwa habari, kutolewa picha na kuchapishiwa makala maalum kila siku za kumpamba. Amekuwa akiwakaanga wananchi masikini wa Tanzania kwa mafuta yao wenyewe. Binafsi ninajivunia rekodi yangu kwamba kampuni zinazomilikiwa na familia yangu zimetoa ajira za uhakika kwa wafanyakazi takriban 6,000 na pia zinalipa kodi inayostahiki Serikalini. Ninaona fahari kusema kwamba kampuni zetu zinatambulika hata na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwamba zinaongoza katika ulipaji wa kodi hapa nchini. Hiki ndiyo kipimo cha uzalendo kwa nchi na siyo ule wa kutafuta kuonewa huruma kwa kuwazushia maovu watu kupitia vyombo vya habari ulivyovianzisha kukutukuza wewe na kuwachafua wengine.

 

Mbali ya hayo, Reginald Mengi huyu huyu ambaye amenituhumu mimi na wengine kuwa tuna akaunti za fedha nje ya nchi ambako ndiko tunakoweka fedha zetu na akadai huo si uzalendo, yeye mwenyewe ana akaunti ya fedha za kigeni nje ya nchi. Nampa changamoto akanushe kwamba hana akaunti ya fedha za kigeni nje ya nchi. 

Mengi huyu huyu pia anatutuhumu sisi kutumia fedha zetu kuanzisha magazeti ya kumchafua yeye na eti “wale wanaomsaidia Rais Jakaya Kikwete kupambana na ufisadi“. Anayasema haya wakati yeye anaongoza kwa kuanzisha magazeti, tena mengine yakionekana wazi wazi kwamba yameanzishwa kupambana na watu fulani fulani ambao ni mahasimu wake kibiashara au kisiasa. Tayari ameanzisha magazeti ya The Guardian, This Day, Nipashe, Kulikoni, Sema Usikike, Taifa Letu, Alasiri, Lete Raha, Kasheshe, Acha Umbeya  na mengine mengi anayoyafadhili kwa mlango wa nyuma. Hivi yeye amepata wapi fedha za kuanzisha magazeti haya yote? 

Kwa muda mrefu nilikuwa nikihisi kuwa Mengi ndiye aliye nyuma ya kampeni zote chafu za kutuchafua baadhi yetu. Siku zote amekuwa akikanusha hilo kwangu lakini sasa amejianika na kujidhihirisha wazi kuwa ndiye kinara wa mbinu hizo chafu. Wakati fulani mwaka jana, akiwa hewani umbali wa futi 35,000 kutoka usawa wa bahari, aliwaambia watu aliokuwa nao kwamba Jumatano inayofuata “tutammaliza Rostam katika MWANAHALISI”. Nilipopata habari hizo nilimpigia simu na yeye alikanusha vikali kuwa hakutamka maneno hayo. Nilimuamini lakini ilipofika Jumatano, kweli MWANAHALISI lilikuja na habari ya kunichafua kama alivyokuwa ameahidi Mengi. 

Katika kipindi cha takriban mwaka mmoja uliopita, nilipata taarifa kwamba ni Mengi ndiye aliyekuwa akiendesha na kusimamia kampeni ya kunisakama kwa kupika na kusambaza habari zote chafu zilizolenga kunichafua. Nilipoonana naye kumueleza juu ya taarifa hizo, siyo tu aliruka sana bali pia aliapa kwa jina la mama, mke na mtoto wake kwamba hahusiki kabisa na kampeni hizo na kwamba hata yeye anakerwa nazo. Kujitokeza kwake wiki iliopita na tuhuma chafu dhidi yangu zisizo na ushahidi wowote sasa kumeweka kila kitu hadharani kwamba yeye ndiye kinara wa uchafuzi huu wenye lengo la kuleta chuki na mifarakano katika nchi. 

Najua atakanusha haya kwa sababu yeye ni mwepesi wa kulalamika kuwa anaonewa huku akidhani amepewa haki na Mungu ya kuonea wengine. 

Kwa upande mwengine, tabia na mwenendo wake havishangazi sana. Anaonekana kuchanganyikiwa. Hatua ya mzee wa zaidi ya miaka 70 anapofikia kuwaita wengine wauaji pasipo kutoa ushahidi wowote na pia kurejea madai ya kutaka kuuliwa au kudhuriwa mara kwa mara ni dalili ya kuchanganyikiwa. He is a paranoid old man! 

Ni vyema Watanzania wakafahamu kwamba kila anapokabiliwa na matatizo au anapotenda maovu, kimbilio lake la haraka la kujifichia limekuwa ni kusaka huruma kwa wananchi kwa kutaka aonekane ni sehemu yao na kwamba anaonewa kwa kuwatetea wao. Ukweli ni kwamba amekuwa akifanya hivyo ili kutafuta hifadhi na kinga akijua ana madhambi mengi. 

Kwa ufupi, Reginald Abraham Mengi ndiye kinara wa fitina zilizoivuruga nchi na hata kujaribu kuvuruga mipango ya Serikali ya kuwatumikia wananchi na kutekeleza ahadi zake. Halafu mtu huyu anapata ujasiri wa kudai eti anamuunga mkono Rais Jakaya Kikwete. Ameingiza vurugu kila mahala alipotia pua yake. Nchi imekuwa haiendi. Kila kukicha, shughuli imekuwa ni porojo zake na malumbano tu yanayotumia muda mwingi ambao ungeweza kutumika kuendeleza nchi na wananchi wake. 

Niseme kwamba tofauti na yeye ambaye ameishia kutoa porojo zake bila ya kutoa ushahidi wowote na kufikisha hoja na ushahidi wake kwa vyombo vya sheria vinavyohusika, mimi nawagawia hapa baadhi tu ya ushahidi wa ufisadi wa Mengi ambao pia nakusudia kuuwasilisha pamoja na maelezo haya kwa vyombo hivyo ili wamchunguze Mengi na kuchukua hatua zipasazo. Kwa upande mwengine, nimewaagiza wanasheria wangu kuzifanyia kazi tuhuma za uzushi alizozitoa na kuchukua hatua za kisheria zinazofaa dhidi yake. 

Nimalizie kwa kusema Reginald Abaraham Mengi hana mamlaka wala nguvu ya kimaadili (moral authority) ya kuwanyooshea vidole wengine kwa kuwaita mafisadi wala ya kujifanya ni shujaa wa kupambana na ufisadi. Sote tunakubali kwamba kuendesha vita dhidi ya ufisadi ni lazima lakini wale wanaopambana ni lazima vile vile wawe watu safi. Ukweli wa maelezo haya unaonyesha wazi kuwa Mengi hana sifa hiyo bali ni nyangumi wa ufisadi anayejaribu kuficha ufisadi wake kwa kuchafua watu wengine. Watanzania si wajinga kama anavyodhani yeye. Wanaelewa mchele ni upi na pumba ni zipi. 

Nawashukuru kwa kunisikiliza. Ahsanteni sana.

SIKILIZA SAUTI KWA KUBONYEZA HAPA

 

Advertisements

February 23, 2009

Liyumba, Liyumba, Liyumbaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!

Filed under: habari — tarishi @ 11:07 pm

SIKU moja baada ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU), kutangaza donge nono kwa atakayetoa taarifa za alipojichimbia mshitakiwa wa kwanza, Amatus Liyumba, katika kesi ya matumizi mabaya ya ofisi za umma na kusababisha hasara ya sh bilioni 221, mali ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), wananchi mbalimbali wamejitokeza katika taasisi hiyo kutoa taarifa za siri.

Vyanzo vyetu vya habari kutoka katika ofisi hiyo vilisema kuwa licha ya jana kuwa siku ya mapumziko, zaidi ya watu 50 walifika wenyewe katika ofisi hiyo, huku wengine wakipiga simu za kuisaidia TAKUKURU, si tu kwa ajili ya kuhakikisha wanampata Liyumba, bali pia kuibuka na donge nono lililoahidiwa na taasisi hiyo.

“Tunashukuru kwamba wananchi wengi, wameitika mwito, maana hadi kufikia majira ya saa 8:30 mchana, zaidi ya watu 50 walifika kwa siri ofisini kwetu kutoa taarifa za mahala alipo Liyumba.

“Wengine wengi zaidi walitupigia simu na kila taarifa tunaifanyia kazi, tunawaomba wananchi wengine waendelee kutupa taarifa,” alisema mmoja wa maofisa wa TAKUKURU ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe.

Huku akiwa makini kuchagua maneno ya kuzungumza, ofisa huyo alisema taarifa hizo zimewasaidia, lakini pia zimewachanganya, kwani ni wachache waliotaja sehemu zinazofanana, huku wengine wakitaja sehemu tofauti za jijini Dar es Salaam, na wengine nje wakitaja mikoa mingine kama Morogoro, Pwani na Arusha, na kusisitiza kuwa taarifa zote wanazifanyia kazi.

Alipoulizwa kwamba haoni kama kinachofanyika kati ya Liyumba na TAKUKURU ni sawa na filamu au mchezo wa kuigiza, ofisa huyo alisema: “Hili ndilo tatizo, maana baadhi wanafikiri ni utani, taasisi yenye dhamana kubwa kama takukuru, haiwezi kujiingiza kwenye usanii wa aina yoyote unaoweza kufikirika.

“Tunasisitiza kuwa kuna donge nono kwa atakayetoa taarifa za kumkatama Liyumba.”

Alisema TAKUKURU inafanya kila iwezalo kumpata Liyumba, kwani kesho anatarajiwa kupanda tena kizimbani ambapo kesi yake inakuja kwa kutajwa kwa mara ya kwanza tangu alipotoka rumande kwa dhamana tata.

Hata hivyo habari zaidi zilisema Liyumba, aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa BoT, anatarajiwa kujitokeza kesho mahakamani baada ya kukamilisha masharti ya dhamana ya hati za mali za sh bilioni 55.

Mbali na Liyumba, mshitakiwa mwingine katika kesi hiyo ni Meneja Mradi wa BoT, Deogratius Kweka, ambaye hadi sasa bado anasota rumande kutokana na kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.

Hatua hiyo ya TAKUKURU kutangaza donge nono kwa atakayetoa taarifa za kumpata Liyumba, zinatokana na juhudi za vyombo vya dola kuanzia Alhamisi ya wiki iliyopita hadi sasa kushindwa kumkamata na kumfikisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, ambayo Jumatano wiki iliyopita ilitoa hati ya dharura ya kukamatwa mshitakiwa huyo na wadhamini wake wawili.

Wakili wa Serikali, Mwangamilia, ambaye alikuwa akisaidiana na Tabu Mzee kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), alidai mahakamani Ijumaa iliyopita kuwa hawajafanikiwa kumkamata Liyumba kama walivyoamriwa na mahakama hiyo.

Wakili wa mshitakiwa Liyumba, Majura Magafu, ambaye alijiunga rasmi mwishoni mwa wiki iliyopita kumtetea mshitakiwa huyo akisaidiana na Wakili Hudson Ndusyepo, aliiambia mahakama kuwa mteja wake hajafika mahakamani, lakini wadhamini wake ambao ni Otto Agatoni, na Benjamin Ngulugunu walikuwapo mahakamani hapo.

Hakimu Hadija Msongo wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, alisema kesi hiyo itatajwa Februari 24 mwaka huu (kesho), kama ilivyopangwa awali na kwamba wadhamini hao wanatakiwa kufika siku hiyo pamoja na mshitakiwa.

Hata hivyo, habari ambazo Tanzania Daima imezipata jana kutoka vyanzo vya kuaminika vya habari, zinadai kuwa Liyumba hajatoroka, bali yupo nchini, tena jijini Dar es Salaam, amejificha na anachokifanya ni kuhakikisha anakamilisha masharti ya dhamana, ili kesho atakapofika mahakamani aweze kutimiza masharti hayo.

Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, taratibu zilizotumika kumpatia dhamana ya awali zitafutwa na atatakiwa aenze upya, hali itakayosababisha kurudishwa tena rumande.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, uvumi ulizagaa jijini Dar es Salaam, kuwa Liyumba ametoroka. Uvumi huo uliifanya mahakama kutoa hati ya kukamatwa kutokana na mazingira ya utata wa dhamana yake, kwani alidhaminiwa kwa hati ya mali ya sh milioni 882, badala ya mali yenye thamani ya sh bilioni 55.

Amatus Liyumba ambaye ametoweka ghafla na kuacha kizaazaa cha aina yake ambacho hakijapata kutokea toka Uhuru

Amatus Liyumba ambaye ametoweka ghafla na kuacha kizaazaa cha aina yake ambacho hakijapata kutokea toka Uhuru

Liyumba na Kweka wanakabiliwa na matumizi mabaya ya fedha za umma kwa kuidhinisha ujenzi wa minara pacha ya BoT, maarufu kama ‘Twin Towers’ na kuisababishia serikali hasara ya sh bilioni 221.

February 4, 2009

Signs I Wish I Could Hang At Work

Filed under: habari — tarishi @ 6:09 pm

image002image001

January 17, 2009

Ukatili na mauaji ya Albino: Nini kifanyike kuzuia?

Filed under: habari — tarishi @ 6:07 am
Mmoja wa wahanga wa ukatili na mauaji ya albino ambayo yameweka doa kubwa kwa nchi ya Tanzania inayosifika kwa utulivu na amani. Je kifanyike nini kuzuia unyama huu??

Mmoja wa wahanga wa ukatili na mauaji ya albino ambayo yameweka doa kubwa kwa nchi ya Tanzania inayosifika kwa utulivu na amani. Je kifanyike nini kuzuia unyama huu??

January 3, 2009

SERIKALI YAIKOMBOA ATCL

Filed under: habari — tarishi @ 7:32 am

Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL David Mattaka

Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL David Mattaka

Serikali imetoa Sh bilioni 2.5 kwa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) ikiwa ni fedha za awali za kuendesha kampuni hiyo na kulipa baadhi ya madeni kati ya Sh bilioni 3.3 zilizoombwa na kampuni hiyo kama mtaji wa haraka.

Sambamba na hilo, Waziri wa Maendeleo ya Miundombinu, Dk. Shukuru Kawambwa ameunda Tume na kuitaka ifanye kazi kwa siku 21 tangu Desemba 29, mwaka jana ili kubainisha kiini cha matatizo ya ATCL baada ya ripoti ya Bodi ya kampuni hiyo kutotoa maelezo ya kutosheleza.

Mwenyekiti wa Tume hiyo ya watu saba ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ardhi, Profesa Idrissa Mshoro na wajumbe wengine sita, alisema Dk. Kawambwa. Kuhusu mtaji huo wa Sh bilioni 2.5, Dk. Kawambwa aliwaambia waandishi wa habari jana Dar es Salaam kuwa serikali imeamua kuibeba ATCL kuanzia mtaji mpaka ulipaji wa madeni kwa kuwa ni mmiliki wa kampuni hiyo na kwamba itatoa fedha kwa awamu kulingana na mahitaji ya wakati ya kampuni hiyo.

Alisema hapo awali wakati mkataba na Shirika la Ndege la Afrika Kusini unakufa, kulikuwa na deni la takribani Sh bilioni 30 ambazo ni pamoja na Sh bilioni 9.1 za watoa huduma kama ya mafuta ambao ni BP na wasambazaji wa chakula, Sh bilioni saba za uendeshaji na Sh bilioni 17.5 zilizotolewa na serikali kama mkopo.

Alisema deni lingine ni dola za Marekani milioni 4.2 sawa na Sh milioni 5.04 linalodaiwa na SAA ambapo pamoja na kuibeba kampuni hiyo alisisitiza kuwa waliohusika kuihujumu watashughulikiwa ipasavyo, tena mapema.

Alikiri kuwapo matatizo ya utaalamu mdogo katika menejimenti yanayosababisha utendaji mbovu na kusema ni mapema kuchukua uamuzi wa kisiasa kumwajibisha mtu, lakini aliahidi kufanya mkutano karibuni na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya ATCL, Balozi Mustafa Nyang’anyi ili kumpa mwongozo wa namna ya kuchukua hatua za nidhamu kwa waliohusika kuhujumu kampuni.

“Wale ambao watakuwa juu ya uwezo wa Bodi kuwajibishwa, basi Mwenyekiti atapeleka mapendekezo kwa mamlaka ya juu inayohusika ili wawajibishwe na kamwe hatutasita kuchukua hatua zaidi ya hapo kama za kisheria na nyingine kwa wahusika pale itakapobidi,” alisema.

Alisema mbali na madeni hayo ambayo yataendelea kulipwa kwa awamu kulingana na fedha, deni la Sh bilioni 17.5 serikali imelifanya kama mtaji tena kwa kampuni hiyo na pia serikali itatoa Sh milioni 320 kulipa mishahara ya Desemba mwaka jana ya wafanyakazi 300 ambao mpaka leo haijalipwa.

Kuhusu mtaji wa Sh bilioni 91.2 ambao ATCL uliiomba serikali awali, alisema hana kauli kuhusu mtaji huo, lakini alisisitiza kuwa tangu kampuni hiyo iombe mtaji, imenunua ndege mbili aina ya Bombadia, DASH8-Q300 na kukodisha moja, Air Bus 320 kwa gharama za dola za Marekani 370,000 kwa mwezi (Sh milioni 444).

“Lengo ni kuona kampuni yetu inasimama na ndege zinaruka tena, siku za baadaye kuna mpango wa uwekezaji wa mabilioni ya shilingi kwa kununua ndege nyingine, kukodi na kununua vifaa pamoja na kufanya mafunzo…kwa hivyo utaona fedha hizo ni za mahitaji ya dharura ya sasa,” alifafanua Dk. Kawambwa.

Alisema katika hatua hizo zilizochukuliwa na serikali bado mazungumzo yanaendelea baina yake na mwekezaji wa China, ingawa hakuwa tayari kumtaja ila alisema yatakapofikia hatua ya kuridhisha wataweka suala hilo wazi.

Kuhusu ripoti iliyosababisha kuundwa Tume hiyo, alisema kuna mkanganyiko wa maelezo katika taarifa hiyo na mambo kadhaa hajapatiwa majibu hivyo Tume hiyo inapaswa kufuata hadidu tatu za rejea alizozitaja kuwa ni; kubainisha matatizo ya ATCL kitaalamu na kwa kina, kubainisha chanzo chake na kutoa mapendekezo ya mkakati wa kuyatatua na kuhakikisha hayajitokezi wakati mwingine.

Aliwataja wajumbe wengine na wanakotokea katika mabano kuwa ni Dk. Marcellina Chijoriga (Mwenyekiti, Bodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Profesa Ibrahim Juma (Chuo Kikuu cha Dar es Salaam), Dk. Gideon Kaunda (Chama cha Wafanyabiashara Wenye Viwanda na Kilimo-TCCIA), Mtesigwa Maugo (Shirika la Usimamizi wa Usalama wa Usafiri wa Anga Afrika Mashariki – CASSOA), Dk. Mussa Assad (Chuo Kikuu cha Dar es Salaam) na Dk. Hamisi Kibola (Mfuko wa Dhamana ya Uwekezaji Tanzania-UTT).

Wiki tatu zilizopita Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) iliinyang’anya leseni ATCL kutokana na dosari za kukidhi viwango na kanuni za kiufundi na usalama wa anga. Ilirejeshewa Jumanne wiki hii.

Katika hatua nyingine, serikali imeunda Kamati ya kupitia upya mkataba baina yake na kampuni yenye ubia katika usafiri wa reli ya Rites kutoka India ili kuangalia namna ya kufanya mabadiliko katika Menejimenti ya Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) baada ya kubainisha kasoro zilizopo katika mkataba huo.

Dk. Kawambwa alisema tayari kikao cha kwanza kimefanyika Novemba mwaka jana na cha pili kinatarajiwa kufanyika siku yoyote katika mwezi huu; lengo ni kuleta uwiano wa kiutendaji katika ngazi mbalimbali za kampuni hiyo kutokana na sasa kuonekana kuwa nafasi kubwa nyingi zinashikwa na wabia wa Rites zaidi.

December 14, 2008

Shusheni bei ya mafuta jamani, JK awaambia EWURA

Filed under: habari — tarishi @ 6:04 am

Na Mwandishi Maalum 

Rais Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa Serikali imeitaka Mamlaka ya Usimamizi wa Nishati, Maji na Huduma za Umma (EWURA) kuyabana makampuni ya mafuta nchini ili yateremshe bei za bidhaa hiyo, kwa sababu bei ya mafuta duniani imepungua kwa kiwango kikubwa. 

Rais ameshangaa kwa nini wafanyabiashara hao wa mafuta hawapunguzi bei ya mafuta kwa kasi ile ile waliyoyapandishia mafuta bei wakati bei ya bidhaa hiyo kwenye soko la dunia ilipokuwa imepanda sana. 

Rais alikuwa akizungumza leo, Desemba 8, 2008, kwenye Baraza la Idd kwenye Sikukuu ya Iddi El Hajji kwenye Viwanja vya Karimjee mjini Dar Es Salaam. 

Rais Kikwete alitoa ufafanuzi kuwa Waziri wa Madini na Nishati anawasiliana na EWURA kuitaka mamlaka hiyo kuwabana wafanyabiashara wa mafuta, ili kupunguza bei la mafuta kwa sababu bei hiyo imeteremka mno kwenye soko la dunia. 

“Mbona hawa wafanyabiashara hawapunguzi bei kwa kasi ile ile kama walivyokuwa wakiipandisha,” ameuliza Rais kwenye hotuba yake ambayo kwa kiasi kikubwa ilielezea matatizo ya kuyumba kwa soko ya fedha duniani, na hivyo kusababisha matatizo makubwa ya uchumi kimataifa. 

“Kama walivyokuwa hodari katika kupandisha, hivyo hivyo wanatakiwa kuwa hodari katika kuteremsha. Hodari wa kuamka mapema ni lazima awe hodari wa kukabiliana na umande,” amesisitiza Rais Kikwete. 

Bei ya mafuta nchini ilipanda kwa kasi sana kulingana na ongezeko la bei ya bidhaa hiyo kwenye soko la dunia kati ya Desemba mwaka 2005 hadi Julai mwaka huu. Bei ya pipa la mafuta ilipanda kutoka dola za Marekani 50 hadi kufikia dola 147. 

Lakini kutokana na kupungua kwa kiasi kikubwa cha mahitaji ya mafuta, hali iliyosababishwa na kuyumba kwa uchumi wa dunia kulikosababishwa na zahama kubwa katika mfumo wa fedha duniani, bei hizo zimeteremka ghafla. 

Rais Kikwete amesema kuwa katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita, bei ya pipa moja la mafuta imeteremka kutoka dola 147 hadi kufikia dola 45, chini ya kiwango cha bei za bidhaa hiyo ilipoanza kupanda Desemba 2005. 

Rais Kikwete pia amesema kuwa pamoja na kwamba hazijaonekana dalili za dhahiri za kuyumba kwa uchumi wa Tanzania kutokana na mtikisiko katika uchumi wa dunia, lakini madhara ya mali hiyo yanaweza kuikumba Tanzania. 

“Kwa maana hiyo, masoko ya bidhaa zetu katika nchi hizo yamedhoofika. Uuzaji wa mazao yetu makubwa kama ya kahawa na pamba unaweza kuathirika. Vile vile tuna shaka kwamba tunaweza kuathirika kwenye mapato yatokanayo na utalii, ambayo sasa tunayategemea sana kwa uchumi wetu,” amesema Rais Kikwete.

September 7, 2008

FRONT PAGE HEADLINES IN MAINSTREAM NEWSPAPERS

Filed under: habari — tarishi @ 7:43 am

Daily News I Front page

JK: Produce more engineers

Tanzania produces 500 engineers annually and President Jakaya Kikwete has challenged concerned institutions to ensure the figure is doubled to cope with the country’s development goals. The President is optimistic that the country can produce 1,000 engineers annually in a few years’ time. “I am an optimist, just bring me your plans on how we can achieve that and I believe we can reach that target…we can do it in the next few years”, he said. Kikwete was addressing the 6th Annual Engineering Day [AED 2008] in Dar es Salaam yesterday when he made the challenge. The meeting was organized by the Engineering Registration Board [ERB]. He observed that the shortage of engineers in the country reflected the nation’s poverty, adding that Tanzania has a long way to go since a country like India produces 300,000 engineers annually while China produces 600,000 engineers per annum. He said he is aware that very few students opt for engineering courses and stressed the need to put more emphasis on science subjects in secondary schools. “We have to take deliberate measures to ensure more students pursue science subjects in secondary schools. Secondary education is an onerous burden and we have to invest heavily in that area”, he said.

[The Guardian; The African] 

Court rejects exhibit in Zombe trial – The High Court yesterday refused to accept as Exhibit 24, still pictures and a sketch showing places at Pande Forest where three mineral dealers and a taxi driver were allegedly brutally shot dead by the police, citing legal technicalities. Principal Judge Salum Massati upheld objections raised by advocates Majura Magafu, Denis Msafiri and Gaudious Ishengoma that the album containing the pictures was not admissible as it was not listed during committal proceedings. He rejected submissions by chief prosecutor Mugaya Mutaki that it was not necessary to list all exhibits before the case was committed to the High Court for trial – and that it would, therefore, be prejudicial to accept the pictures at the moment.

[The Guardian; The Citizen; ThisDay]

The Guardian I Front page 

Ex-detainee Salim suffers memory loss – Suleiman Abdallah Salim, the Tanzanian arrested and detained five years ago for his alleged involvement in the 1998 bombings of the US embassies in Dar es Salaam and Nairobi, has said he is down with temporary memory loss. He blames the problem on the physical and psychological torture he says he was subjected by American soldiers during and following his arrest.

The African | Front page

ANC thanks Tanzania for aid

– The Africa National Congress [ANC] has thanked Tanzania for the role it played in helping South Africans fight against apartheid. Tanzania provided training for South Africans during the struggle against apartheid. This was said by the ANC president Jacob Zuma while thanking President Jakaya Kikwete during dinner hosted for him at the State House in Dar es Salaam. Zuma, who led an ANC delegation, said they had come to Tanzania to borrow CCM’s experience in running party affairs.

[The Guardian].

Ministry sends team of experts to Ruvuma – The Ministry of Health and Social Welfare has sent a medical team to Mbinga District/Ruvuma Region to establish the kind of disease that has killed six pupils of Makatane Primary School. The Minister for Health and Social Welfare, Prof. David Mwakyusa, who apparently was unaware of the story, phoned the Ruvuma Regional Medical Officer to get more details. After the briefing, Mwakyusa told ‘The African’ that a team of experts had been dispatched to ascertain the disease and how to curb it. He said according to the report, the symptoms of the disease were strange since the patients were paining of headache, stomachache, and traces of blood were found in their stool. 

ThisDay I Front page
 

Revealed: Up to 40% of goods sold locally are fake – Up to 40 per cent of goods on sale in Tanzania – particularly construction equipment, electronics, vehicle spare parts and some medicines – are counterfeit thus posing serious threat to the welfare of consumers and the national economy in general. “According to our study, between 20 and 40 per cent of goods in local shops were found to be counterfeit,” the director general of the Fair Competition Commission [FCC], Godfrey Mkocha, told ‘THISDAY’ in an interview in Dar es Salaam yesterday. He added: “Bringing counterfeit goods into a nascent economy like ours is just as criminal as engaging in terrorism and economic sabotage.” According to Mkocha, although the problem of counterfeit goods in the country has existed for sometime now, it was actually worse before the recent enactment of a new law prohibiting intrusion of counterfeits. He said since the new legislation started being enforced last year, the FCC has managed to impound and destroy counterfeit goods worth well over one billion shillings.

 Daily News | Inside pages 

Explore opportunities, PM tells traders [Pg 2] –

The business community needs to change mindsets and become more aggressive and outward looking to benefit from emerging opportunities. Prime Minister Mizengo Pinda made the call yesterday when speaking to representatives of various business interests in Dar es Salaam. He said that the business community has learnt diverse business environments and explored new opportunities. The community can also advise the Government on the best policies that the country can adopt to compete at the regional level. “There was a time after independence we were left behind because of the policies we adopted…but that has to change now and we have to rid ourselves of policies and attitudes that do not benefit us in a competitive environment,” he said. Delegates of the Trade, Business and Investment Mission from Tanzania will from tomorrow to September 16 visit four countries of East Africa to familiarize themselves with counterpart business communities and to secure business opportunities.

[The Guardian]

Govt extends measles vaccination until tomorrow [Pg 2] – The Ministry of Health and Social Welfare yesterday extended the measles immunization campaign to tomorrow. According to a press release issued in Dar es Salaam by the Ministry’s acting Permanent Secretary, Dr. Gilbert Mliga, the extension follows a low turnout by parents in this year’s campaign. Earlier, the campaign which was launched on August 30 in Tanga Region by the Vice President, Dr. Ali Mohamed Shein wound up as scheduled last Monday. Mlinga said that the vaccine was safe and has been used to serve the purpose for more than 30 years.

·

 

Dar police hold 22 ‘wild dog’ bandits [Pg 2] – Police in Dar es Salaam are holding 22 bandit’s alias ‘mbwa mwitu’ for robbery in different areas by using knives and grill. The Special Zone Regional Police Commander, Suleiman Kova, said yesterday that the suspects were engaged in robbery at Kichangani, Mtoni Mtongani and Temeke areas. “It is due to the police patrol search of one week, the suspects accepted the crime and four among 22 were taken to the Court”, he said.

·

 

JK’S visit to US big success [Pg 2] –

The United States Ambassador, to Tanzania Mark Green, has described President Jakaya Kikwete’s recent visit to Washington DC as a ‘tremendous success’ and has also strengthened bilateral relations between the two countries. In a statement issued yesterday, Ambassador Green, said President Kikwete and his counterpart President George Walker Bush were able to discuss important new initiatives such as improving education, health care, and agriculture related matters, especially providing local farmers with increased access to credit. The statement said that during President Kikwete’s one-week visit to the US capital, American and Tanzanian leaders announced tens of million of dollars in new initiatives to help strengthen education sector, health and economic development.

[The Guardian; The African; ThisDay]

·

 

Trial of ICTR staff murder suspect likely in October [Pg 2] – The hearing of a murder trial of a Cote d’lvoire [Ivory Coast] national, Armandi Guehi, who allegedly murdered his wife nearly three years ago, Angele Kosiah Sama, an employee of the International Criminal Tribunal for Rwanda [ICTR] in the outskirts of Arusha is likely to commence next month in Moshi. The UN tribunal is trying the key suspects of the 1994 genocide, which claimed lives of approximately 800,000 ethnic Tutsis and moderate Hutus.

[The Citizen]  

Drama as accused Chinese refuse to sign Court documents [Pg 2] – The Mbeya Resident Magistrate’s Court was yesterday thrown into confusion as three Chinese nationals accused of roughing up and injuring an immigration officer and destroying government property worth sh s200,000/- refused to sign documents before Magistrate In-charge, Happiness Ndesamburo. “We cannot sign something we don’t know,’’ maintained the first accused in the case, Zhaofeng Zhang when he was responding through an interpreter to a threat by the magistrate to imprison them for contempt of Court if they continued refusing to sign the document. “Why do you refuse to sign the document?’’ queried Ms Ndesamburo. “Are you not of Chinese nationality, didn’t you plead appear in this Court on September 03 this year? She asked. It was only after clarification was made to them that the three Chinese agreed to sign.

 The Guardian I Inside pages
 

Opposition pledge for unity in polls thrown overboard [Pg 2] – Opposition parties in Ngara District/Kagera Region, have virtually backpedaled on their pledge to field one candidate in a bye-election for councilors to be held later this month. This follows removal of Jactani Meshak, a candidate for Chama cha Mapinduzi [CCM], on suspicious that he entered a girl’s dormitory in a secondary school where he had sexual relations with one of them. According to the opposition, Meshack was regarded as a formidable force in the expected elections. Talking to PST on the break-up of the alliance, Chama cha Demokrasia na Maendeleo [CHADEMA] chairperson in Ngara District Hesau Hosea said that following the incident, opposition parties had each vowed to field their own candidate.

Causes of schoolgirl pregnancies in Kwimba laid bare [Pg 3] – The incidence of early pregnancies in schoolgirls in Kwimba District/Mwanza Region, is alarming, leading to a high number of dropouts. Major causes of the problems include low family incomes, lack of accommodation at schools and prevailing social traditional morals and customs. Others are long walking distances whereby pupils have to walk more than eight kilometres to reach school; and poor school environment. A survey conducted by ‘the Guardian’ in the district recently shows that most parents are low-income earners who cannot adequately fulfill the needs of their children.

·

 

Manual on reporting of gender issues is born [Pg 3] – Gender and Media Southern Africa-Tanzania Network [GEMSAT] on Thursday launched an institutional and capacity building manual to enable journalists to report gender issues accurately. GEMSAT director Rose Haji said in Dar es Sala that the manual would be used to provide training on gender development violence, equality, reproductive health and child abuse. It would further help in mainstreaming gender issues at the workplace. “Our goal is to enhance the capacity of journalists on reporting gender issues and at the same time ensure that the voices of women and men in all their diversity are equitably represented and fairly portrayed in the media,” she said.

·

 

Sitta discusses plight of women, children in war situations [Pg 3] – Community Development, Gender and Children minister Margaret Sitta has said that women and children are more vulnerable to sporadic civil wars in Africa. Sitta made the remakes in Bagamoyo on Monday when opening a three-day international conference on women, peace and security in Somalia. She said Tanzania and other African countries had a lot to learn from women who, in one way or another, got involved in wars such as those in Somalia. 

Monduli council standoff undermines community development [Pg 3] – A simmering conflict between councilors in Monduli District in Arusha Region and newly posted council director Zipora Liana will cause more harm to the community unless higher authorities make timely intervention to iron out their differences. Interviewed Monduli residents have warned. In a council meeting held recently, conflict of interest appeared to be the major reason for the misunderstanding between the antagonistic parties that led to a verbal war which drew curious wananchi to the conference hall where the fracas was talking place. Among issues which prompted the standoff was alleged misappropriation of funds set aside for development projects in the area.

Meeting on Muhimbili workers’ dues comes to premature end [Pg 4] – A meeting between the government and workers of the Muhimbili National Hospital ended prematurely on Thursday in Dar es Salaam after Health and Social Welfare permanent secretary Wilson Mukama failed to give satisfactory explanation as to when the hospital workers would get their salary arrears. Mukama was among top government officials who attended the meeting which aimed at averting a planned strike by the workers following delaying the payment of the arrears. The PS failed to assure the workers as to when they would be paid, upon which the workers shouted him down.

·

 

We’re having it very rough say residents moved from Geita mine [Pg 4] – More than 250 residents from 86 wards now occupied by Geita Gold Mine in Mwanza Region, have complained about the hard life they face after being relocated from their previous land, which is now being used for mining activities. They aired their complaints at a news conference in Dar es Salaam on Wednesday. They claimed that currently were accommodated in tents supplier by the Christian Council of Tanzania and clergymen. Speaking on behalf of other evictees, Johna Saidi said they were evicted at midnight under the supervision of Local Government authorities and the police.

·

 

Poland closes embassy in Dar without notifying Govt [Pg 4] – Poland has secretly closed down its mission in Tanzania for reasons which are yet to be known. The embassy closed its doors since last month without any notice to the public, thus causing inconvenience to both Tanzanians and Polish nationals who needed consular services. According to a Foreign Affairs and International Cooperation official who preferred anonymity, quiet closure of missions was not quite new.

Lindi RC calls on farmers to increase crop production [Pg 4] – A call has been made to farmers from the southern regions of Lindi and Mtwara to fully utilize the Dar es Salaam Lindi road by increasing production of both cash and food crops. Lindi Regional Commissioner, Saidi Mecky Sadiki, made the call recently in Lindi shortly after Infrastructure Development Permanent Secretary, Omar Chambo, had inspected various infrastructure projects in the southern regions.

Dar is still committed to EA integration with care [Pg i] – In recent times, it has transpired in some economic and political circles that Tanzania was dragging its feet in the ongoing planned East African Common Market. In an authoritative article published in the ‘Daily National of 29
th August by a prominent journalist and one time editor of ‘the standard’ Tim Mshindi titled “as Tanzania dithers, EA intergrading must roll on” there is every reason to believe our partners want to go it alone. Tom mshindi says in his article ‘it is regrettable but hardly surprising that Burundi, Kenya, Rwanda and Uganda must now proceed with the East African integration project without Tanzania.
·

Local coal effectively tested for home and industry uses [Pg i] – The African Mining Network [AMN] has successfully tested the use of local coal briquettes. The testing was accomplished in partnership with the Kali Power Company limited, which has now together developed clean and cheaper coal briquettes. Speaking to ‘the Guardian’ after the testing ceremony held recently in Dar es Salaam, AMN chairperson Luhimbo Charles said their aim was to support government’s effort to conserve the environment through the use of coal in home and industries. “We want people to stop felling trees recklessly for the pretext of getting fuel-wood. Coal briquettes will do in place of charcoal and firewood. 

Local coal effectively tested for home and industry uses [Pg i] – The African Mining Network [AMN] has successfully tested the use of local coal briquettes. The testing was accomplished in partnership with the Kali Power Company limited, which has now together developed clean and cheaper coal briquettes. Speaking to ‘the Guardian’ after the testing ceremony held recently in Dar es Salaam, AMN chairperson Luhimbo Charles said their aim was to support government’s effort to conserve the environment through the use of coal in home and industries. “We want people to stop felling trees recklessly for the pretext of getting fuel-wood. Coal briquettes will do in place of charcoal and firewood.

 

August 18, 2008

Raza, NRA ndio wakereketwa zaidi wa utaifa wa Zanzibar?

Filed under: habari — tarishi @ 6:11 am
Bendera ya 'Taifa' la Zanzibar

Bendera ya 'Taifa' la Zanzibar

Raza, NRA ndio wakereketwa zaidi wa utaifa wa Zanzibar?
Na Theodatus Muchunguzi  MOJA ya matukio makubwa ya kisiasa yaliyotawala nchini ni shinikizo la maandamano tuliyoelezwa kuwa yaliandaliwa na Chama cha National Reconstruction Alliance (NRA) Zanzibar kwa ajili ya kupinga kauli iliyotolewa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuwa Zanzibar si nchi, bali sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Maandamano hayo awali yaliruhusiwa na polisi, lakini baadaye yalizuiliwa na kusababisha malalamiko kutoka kwa viongozi wa NRA Zanzibar, makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), akiwamo mfanyabiashara maarufu, Mohamed Raza, ambaye ni Mshauri wa zamani wa Rais wa Zanzibar, Dk Salmin Amour, kuhusu mambo ya Michezo pomoja na Wazanzibari wengine.

Inasemekana malalamiko dhidi ya Jeshi la Polisi yalitokana na hasara ambayo waandaaji wa maandamano hayo waliipata. Hasara hizo ni pamoja na kuandaliwa kwa fulana zilizokuwa zimeandikwa maneno ya kudai Zanzibar.

Kuna mambo yanayopaswa kuhojiwa kuhusu nani hasa aliyekuwa nyuma ya maandalizi ya maandamano hayo. Nasema hivyo kwa sababu itakumbukwa kuwa NRA ni miongoni mwa vyama vichanga; nikimaanisha kwamba nguvu yake katika siasa za Tanzania bara na Visiwani si kubwa.

Chama hicho hakina hata kiti cha ubunge Tanzania Bara na hakijawahi kufanya vizuri katika chaguzi zote za mwaka 1995, 2000 na 2005. Safu ya uongozi na mtandao wa wanachama na wafuasi wa chama hicho ni mambo ambayo hayaeleweki vizuri.

Kwa Zanzibar, NRA hakina ngome yoyote kwa kuwa siasa za Zanzibar hakuna asiyezifahamu kwamba ni vyama viwili tu vya CCM na Chama cha wananchi (CUF) vyenye mitandao na ngome za wanachama na wafuasi, viti vya ubunge na uwakilishi pamoja na safu za uongozi madhubuti na zinazoeleweka vizuri.

Ujasiri wa NRA wa kuandaa maandamano ya Wazanzibari eti kudai nchi haukuhojiwa na mtu yeyote vikiwemo vyombo vya habari, lakini lilikuwa ni suala muhimu kulihoji kwa kuzingatia kuwa chama kichanga kama hicho, tena huko Zanzibar kuwa na ubavu wa kuandaa maandamano ya kitaifa ya kudai Zanzibar.

Baadhi ya maswali ni je, NRA ambacho ni miongoni mwa vyama vya siasa 18 nchini vyenye usajili wa kudumu lakini hakipokei ruzuku yoyote kutoka serikalini kutokana na kutokuwa na viti vya ubunge kilipata wapi fedha za kuandaa maandamano hayo ya kudai Zanzibar?

Kitu kingine ambacho kinashangaza na kinahitaji majibu ni je, baadhi ya wanachama na makada wa chama tawala CCM walijihusishaje na maandamano hayo, achilia mbali kauli zao za kupingana na Pinda kuhusiana na suala la hadhi ya Zanzibar?

Raza, ambaye katika siku za karibuni amekuwa mstari wa mbele kutoa kauli mbalimbali za kupingana na kauli ya Pinda kuhusiana na hadhi ya Zanzibar, baada ya maandamano hayo yanayoitwa ya NRA kufutwa na Jeshi la Polisi, aliitisha mkutano wa waandishi wa habari siku hiyo Jumapili na kutoa kauli za kuchochea kuvunjika kwa Muungano, akidai kuwa Zanzibar inamezwa katika Muungano huo.

Raza alikaririwa na vyombo vya habari akiwataka Wabunge wa kutoka Zanzibar warejee makwao kwa madai kuwa hawaiwakilishi Zanzibar kama nchi. Pia aliwataka wafanyakazi wa taasisi za Muungano zilizopo Tanzania Bara wakiiwakilisha Zanzibar katika serikali ya Muungano kuwa wanapaswa kurudi kwao kwa kuwa Zanzibar sio nchi.

Alikwenda mbali zaidi kwa kudai kuwa Wazanzibari wote kwa sasa ni wahaini na wataendelea kuwa wahaini hadi suala hili litakapopatiwa ufumbuzi; akiwa na maana kuwa mtu anayesema Zanzibar ni nchi anachukuliwa kuwa ni mhaini. Raza pia alidai kwamba, vikao vilivyokaa kuidhinisha kwamba Zanzibar si nchi havikuwa halali kwa kuwa havikupata ridhaa ya Wazanzibari!

Kauli hizo za Raza zinazua maswali mengi. Moja, ni kuwa ilikuwaje Raza akajitokeza kulishambulia Jeshi la polisi kwa kuyapiga marufuku maandamano hayo? Pili, ni kwa nini Raza alijitokeza siku hiyo hiyo ambayo maandamano hayo yalikuwa yamepangwa kufanyika?

Baadhi ya wasomaji walionitumia ujumbe mfupi wa simu wakidai kuwa baadhi ya makada wa CCM na vyama vingine vya siasa walikuwa nyuma ya maandalizi ya maandamano hayo ya NRA. Wengine walikwenda mbali kwa kudai kuwa ajenda kuhusu suala la hadhi ya Zanzibar imewaunganisha Wazanzibari wote bila kujali itikadi zao za kisiasa.

Wakati mjadala kuhusu hadhi ya Zanzibar ulipoanza baada ya kauli ya Pinda bungeni mjini Dodoma, serikali ya Jamhuri ya Muungano na CCM zilijiweka pembeni kukwepa malumbano na ilifikia wakati vyombo vya habari na wanasiasa kuhoji sababu za ukimya huo wa kushindwa kulitolea tamko kama chama au kauli ya rais Jakaya Kikwete.

Muda mchache kabla ya Jumapili ambayo maandamano hayo yalipangwa kufanyika, mwanasiasa mmoja mkongwe nchini kutoka CCM aliniambia kuwa: ”Kama serikali itaruhusu maandamano ya kudai Zanzibar yakafanyika, hizo zitakuwa dalili tosha za kuthibitisha kuwa mwisho wa Muungamo umefika”.

Baadaye niliposikia habari za kupigwa marufuku kwa maandamano hayo, nilipata hisia kuwa pengine watu wenye busara wamewashauri viongozi wetu kuchukua hatua hiyo, ambayo kwa wenye uwezo wa kupima mambo na kuyatafakari watakubaliana nami kuwa ingeleta athari.

Kila mtu ana haki ya kuelezea hisia na kutoa maoni yake, lakini maandamano hayo tunayoambiwa kuwa yaliandaliwa na NRA kwa ajili ya Wazanzibari kudai nchi yao yaliandaliwa bila kusubiri ahadi iliyotolewa na serikali kwamba wataalamu wa sheria wa pande zote wangekaa na kupitia mambo, zikiwemo tafsiri za kisheria zinayoonekana kusababisha utata katika suala zima la Muungano.

Ni kweli kabisa kwamba kwa kiwango kikubwa serikali zote mbili zilichelewa sana kukaa pamoja kubainisha na kujadili baadhi ya kasoro za msingi, ambazo kwa zaidi ya miaka 40 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zimekuwa zikizua utata.

Huu ndio wakati ambao agizo la Rais Jakaya Kikwete linapaswa kuwataka Waziri Mkuu na Waziri Kingozi wa Zanzibar kukutana na kujadili namna ya kumaliza kasoro zilizoko katika Muungano. Aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa na waziri Kiongozi, Shamsi Vuai Nahodha, walijitahidi kuanza mchakato huo lakini matunda yake hayakuonekana.

Kwa kuwa Rais Kikwete hivi karibuni alipounda upya Baraza la Mawaziri alimpa Makamu wa Rais, Dk Ali Mohamed Shein kusimamia mchakato huo, kuna matumaini makubwa ya kuondoa kasoro hizo ili kuepukana na uwezekano wa upande mmoja kukosa uvumilifu na kuona njia ya mkato ni kudai nchi kwa maandamano, ingawa hatua hiyo tafsiri yake ni uhaini.

Kauli za Raza za kuwataka Wazanzibari kuususia muungano hazijengi taifa bali zinachochea kulibomoa kwa kuwa leo hii Wazanzibari wakijitoa katika Muungano, kesho Wapemba watadai Pemba yao. Mashambulizi ya wiki iliyopita ya Russia dhidi ya Georgia iliyojitoa katika muungano wa Urusi ya zamani lakini baadaye jimbo la Ossetia nalo likajitoa Georgia ni fundisho tosha kwetu.

Kero za muungano zinawaathiri Watanzania wote na siyo upande mmoja. Kwa hiyo inashangaza sana kuona Raza na NRA wakijifanya kuwa ndiyo wakereketwa wakubwa wa hadhi na utaifa wa Zanzibar kuliko raia wengine.

Baruapepe: theodatusm@yahoo.com

Simu: 0737-038475

Kipi kitaanza, Zanzibar kujitoa Muungano au Pemba kujitenga na Unguja?

Filed under: habari — tarishi @ 6:05 am

Na Makene Tumaini

MWANAMUZIKI nguli wa muziki wa reggae kutoka Afrika Kusini, Lucky Dube, alipata kuimba katika moja ya nyimbo zake kuwa, ‘If you follow politician, you will never come far,’ kwamba ukiwasikiliza na kuwafuata wanasiasa hautafika mbali. Watakuacha solemba tu. Kwa maana ya kwamba wanasiasa si watu wa kuaminika sana, wakati wote.

Kwa mfuatiliaji wa masuala ya siasa, sehemu yoyote hapa duniani, achilia mbali Tanzania, anaweza kuwa na mifano mingi tu, kuweza kuelezea na kulithibitisha hili. Wazo hili linaweza kuungwa mkono na hoja nyingine kwamba katika siasa hakuna rafiki wala adui wa kudumu.

Adui yako mkubwa leo anaweza kuwa rafiki yako mkubwa kesho na kinyume chake. Ndiyo maana mtu hapaswi kushangaa leo Wamarekani wakimsaka rafiki na kipenzi chao hapo zamani – Osama Bin Laden. Haishangazi kusikia kuwa Jonas Savimbi aliuawa baada tu ya waliokuwa wakimpa kiburi, kumsaliti kwa serikali ya Angola, si wengine nao ni hao hao Marekani.

Mlolongo unaweza kuwa mrefu, usishangae pia unapomuona ghafla, Muammar Gaddafi, rais aliyekuwa akihesabika kuwa mmoja wa adui wa nchi ya Marekani na washirika wake wa Ulaya, sasa ni mtu wao wa karibu.

Hiyo ndiyo siasa. Lakini pia hayo ni ya Musa (ughaibuni), ya Firauni (hapa nyumbani), pia yanaweza kukumbukwa na kuonekana. Wapo akina Leo Lekamwa na Augustine Mrema. Tunaweza kuwakumbuka watu kama Masumbuko Lamwai na Tambwe Hiza, tukiwataja kwa uchache tu. Historia inaonesha hivyo, haijafutika.

Halafu kuna hili na Zanzibar kuwa ni nchi au la, nalo limetufikisha katika uhalisia wa wanasiasa wetu na siasa kwa jumla. Suala limezua suala, kila mwenye uwezo wa kusema ameshasema na kunukuliwa na vyombo vya habari.

Mara nyingi kwa watu wafuatiliaji wa ‘mtifuko’ wa kisiasa Tanzania, hasa unapohusisha masuala ya Muungano kuna watu ambao hawawezi kujiuzia kulisema.

Haliwezi kupita jambo la nafasi ya Zanzibar katika Tanzania usiwasikie watu kama akina Raza, Maalim Seif Sharif Hamad na wengine (kwa siku za hivi karibuni wanavuma pia akina Shamuhuna.

Wote waliotarajiwa kupaza sauti zao katika suala hilo, ambalo chimbuko lake ni kauli ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakati akitoa hotuba ya majumuisho ya Ofisi yake, wameshafanya hivyo.

Hilo limesababisha kuwa na ‘Muungano usio rasmi’ kati ya mahasimu wakubwa wa siasa za Zanzibar – CCM na CUF. Hiyo ndio siasa.

Jamaa sasa wanaonekana kuwa ni kitu kimoja, mtu akihisi kuwa kwa sasa hawa jamaa wanaweza hata wakakutana kwa siri na kupanga mikakati ya kuibuka na hoja za pamoja, hata kama wasipotaka kuonesha hivyo hadharani, atakuwa hakosei.

Kwamba wahafidhina na wanamageuzi wanaweza kukaa meza moja kwa suala hili na mwisho wa siku wakaongea lugha moja, ni suala ambalo linaweza kusubiri muda tu kwa jinsi wanasiasa wetu wanavyoendesha mambo kwa kubahatisha, bila kuwa na mpangilio.

Halafu, wanasiasa walivyo watu wa ajabu wenye kutaka kulazimisha kidole cha shahada kiwe sawa na cha kati kwa urefu na ukubwa. Katika hili la Zanzibar yameingizwa mambo mengi ambayo hapo awali hayakufikiriwa.

Wahusika (wanasiasa) wote wanaorusha hoja zao, vijembe vyao, jeuri yao na kupima mbavu zao katika ulingo wa siasa, hasa wakijaribu kupinga hoja ya Pinda, kwa hoja za nguvu (badala ya nguvu ya hoja). Hawataki kuwaeleza wasikilizaji wao kuwa kati ya dola, nchi, taifa kipi hasa kinagomba hapa.

Mwanasiasa yeyote makini hasa kutoka chama makini chenye kuwa na washauri wa masuala ya sheria na katiba, bila shaka angelitazamiwa kuja na hoja iliyotokana na tafakuri jadidi.

Angechambua hoja, kupitia misingi yote na hatimaye kufikia hitimisho murua, lenye mantiki na linaloeleweka akiwaacha watu wakiwa wameelewa.

Kama mtu wa kawaida hawaelezwi masuala ya namna hii kwa ufasaha bila kuangalia mtaji wa kisiasa, tunaweza kuwa na uhakika kabisa hata tuliowasikia majuzi wakiwa wamehamasika (au kuhamasishwa?) kuandamana eti kumpinga Waziri Mkuu, wakiulizwa mmoja mmoja nini hasa kilichowafanya kutaka kubeba mabango, wachache mno watakaoweza kukuambia kitu chenye mantiki kuonesha kuwa wanajua wanachokitaka.

Wanasiasa kama akina Raza, Maalim Seif au Shamuhuna (kuwataja kwa uchache), ndio wenye kuweza kuwafikia kwa urahisi zaidi wananchi wao, kuliko akina Profesa Shivji, Haroub Athuman au Mwesiga Baregu na wataalamu wengine ambao wamekuwa wakijaribu kuzielezea zana zote hizo za taifa, nchi au dola.

Wengine wanasema kuwa wanapanga kuzunguka kote visiwani eti kuzidi kuwahamasisha Wazanzibari waendelee kusimama kidete kutetea ‘nchi’ yao.

Lakini hamadi ni iliyo kibindoni, wanatafuta kuungwa mkono katika upande ambao tayari wameshachukua msimamo bila kujali kama utakuwa na maslahi kwa wananchi wote.

Unapomsikia kiongozi wa serikali, akiwa pia na kofia ya uanasiasa, anatoa kauli kumjibu mkubwa wake kuwa hizi si zama za kutishana na kubembelezana kuhusu Muungano, anafaa kutazamwa kwa macho makini.

Kwani wakati Pinda akiibua hoja ile alimtisha mtu? Mbona alipata kurudia kwa masikitiko akisema alimaanisha nini. Lakini hawa tunaowasikia wakitema cheche, hata hawafafanui msingi na maana hasa ya madai yao, tujichunge nao.

Wanaompinga Pinda, iwe vibarazani, mikutanoni, maofisini na hata katika kumbi kubwa za kuheshimika kama Baraza la Wawakilishi, wangesubiri wanasheria wafanye kazi zao kama Waziri Mkuu alivyoelekeza, wangeonekana wanabembeleza?

Maneno yasiyokuwa na mpangilio baadhi yao yamewabubujika. Badala ya kueleza suala, wanaishia ‘kutukana’, kukejeli, kurusha vijembe, kukebehi na hata kutumia ujuzi wa maneno ya Kiswahili yasiyokuwa na tija yoyote katika ujenzi wa hoja ya suala zima.

Shamuhuna amewahi kukaririwa akiibua hoja tata wakati watu walipokuwa wakisema suluhisho la mpasuko wa kisiasa Zanzibar ni serikali ya mseto. Ilibidi CCM watoe kauli kuwa hayo yalikuwa ni maoni yake binafsi. Lakini kwa hili la sasa, hatujasikia ikisemwa hivyo na chama hicho.

Kutokana na ukimya wa sasa hasa kutoka kwa watu tuliotarajia wawakemee na kuzisukumizia mbali kauli za akina Shamuhuna, tunashawishika kuamini kuwa safari hii kauli hii si ya kwake binafsi, inasukumwa au anasukumwa na wengine wengi nyuma yake.

Na kwa kuwa Shamuhuna si mtu mdogo katika CCM na serikali ya Mapinduzi Zanzibar, ukiachilia mbali Raza ambaye hatujui alitumia nguvu inayotokana na wadhifa upi kumbeza Tambwe, ukiongeza na ukimya wa ‘mabosi’, tunashindwa pia kujizuia kuamini kuwa huo ndio msimamo atakaokwenda nao katika meza ya majadiliano, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar.

Maalim Seif nafikiri katika hili atapaswa kuwaeleza vizuri Watanzania. Kwa sababu mbali na kushangilia hukumu ile kesi ya uhaini ya akina Machano na wenzake mwaka 2000, hivi majuzi kanukuliwa akimsihi Rais Karume atangaze mgogoro wa kikatiba katika Muungano.

Katika mkutano huo wa Kibanda Maiti, kama alivyonukuliwa, Maalim Seif alitumia muda wake akimsifia Mzee Karume, kuwa alikuwa imara asiyepata kuyumbishwa.

Kwa kauli ya namna hiyo tunaweza kusema kuwa Maalim Seif alikuwa akimkubali Karume baba. Lakini wa sasa, hajawahi kutamka hivyo.

Lakini ni Maalim Seif huyo huyo ambaye hajapata kumtambua Karume kama rais wa Zanzibar, kwa misingi ya kwamba alimnyang’anya tonge mdomoni.

Katika hili, ni vyema vyama vyote vinavyosema kuwa vinalilia ‘haki’ au ‘hadhi’ ya Zanzibar viwe na msimamo madhubuti katika makabrasha yao, kama ni katika ilani au katiba zao.

Lakini ili kuonesha kuwa wanarukia mambo, ukitazama katiba zao, itakuwa ni bahati ya mtende kukuta ‘hadhi’ ya Zanzibar imeelezwaje, kama ni dola, nchi, taifa, mkoa, au vyovyote vile. Huko ni kubahatisha mambo.

Sasa CUF imepata changamoto kubwa kutoka kwa mmoja wa wawakilishi wake, aliyeamua kujitolea kumfunga paka kengele.

Bila kutafuna maneno kasema sasa ni muda mwafaka wa chama hicho kuitambua serikali ya Rais Karume. Hakuna haja ya kuendelea kutoitambua serikali kwa muda wote huu na wakati huo huo hali halisi ikionesha kuwa wako pamoja.

Lakini katika harakati zao za kudai nchi yao, ni vizuri baadhi yetu tukaelezwa waziwazi, kuwa ni kipi wanasiasa wetu wanataka kitangulie, kumeguka kwa Muungano au kujitenga kwa Pemba na Unguja.

Kwa sababu kumekuwapo na maneno mengi hasa baada ya kuzorota (au kukwama) kwa mazungumzo ya muafaka kuwa ni bora Pemba akajitegemea, kwani imekuwa ikitengwa katika serikali ya sasa ya Karume.

Sasa hao hao ambao tumepata kuwasikia wakipaza sauti zao wakitaka Pemba iwe na serikali yake, tunawasikia wakitaka Zanzibar isibabaishwe katika Muungano na kwamba inaweza kujitoa. Wana ajenda gani hawa? Kwamba wanajua wakifanikiwa kuuvunja Muungano itakuwa rahisi kwao kukitenganisha kisiwa cha Pemba?

makene_84@yahoo.com 0713 58 44 82

August 15, 2008

Sakata ya EPA yaelekea kuichanganya serikali

Filed under: habari — tarishi @ 12:01 pm
Na Ramadhan Semtawa 

UCHUNGUZI wa sakata la ufisadi wa zaidi ya Sh 133 bilioni katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), sasa unaichanganya serikali, huku Ikulu na wajumbe wa tume ya Rais ya Uchunguzi wa suala hilo kila mmoja akikwepa kusema lolote.

 

Hali imezidi kuwa tete kutokana na kuwapo kwa taarifa za kukanganya juu ya fedha iliyookolewa na wamiliki halisi wa kampuni 22 zilizochotewa fedha hizo ni nani.

 

Kuna utata pia kwamba, hatua zinazopendekezwa na kuchukuliwa na timu ya uchunguzi, ni ngumu kutekelezwa na huenda sasa serikali inataka kuvuta muda ili suala hilo lipoteze nguvu.

 

Tayari Timu iliyoongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johson Mwanyika, imekwishakamilisha kazi yake na kuandika ripoti zaidi ya siku 21 sasa, lakini habari zinasema kwamba, bado hawajapata muda wa kuiwasilisha kwa Rais Ikulu.

 

Si Ikulu ambao wako tayari kusema lolote juu ya ripoti hiyo wala wajumbe wa timu hiyo.

 

Wajumbe wengine wa timu hiyo ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hosea na Inspekta Jenerali wa Polisi, Said Mwema.

 

Taarifa kutoka vyanzo huru vya habari ndani ya serikali, zinasema hadi sasa, Rais Jakaya Kikwete, anafikiria matokeo ya maamuzi ambayo atachukua baada ya ripoti ya timu aliyounda kutolewa.

 

Kwa mujibu wa taarifa hizo, Rais ana mambo mawili makubwa anayoangalia, moja ni kuona namna gani matokeo ya maamuzi atakayochukua yatakubalika kwa wafadhili ambao wanasubiri kwa hamu kabla ya kuruhusu kutolewa kwa fedha za kusaidia bajeti ya serikali ya mwaka wa fedha 2008/09 walizoahidi.

 

Wafadhili walitoa ahadi ya fedha hizo kiasi cha asilimia 40 cha bajeti ya Sh7.2 trilioni kwa mwaka huu wa fedha, kwa masharti kwamba, fedha halisi zitatolewa kutegemeana na jinsi serikali itakavyoshughulikia mafisadi waliotajwa kwenye ripoti ya Ukaguzi wa EPA iliyofanywa na Kampuni ya Ernst & Young. Msaada huo wa fedha ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

 

Kundi jingine lenye matarajio kama wafadhili, ni wananchi ambao tangu taarifa za ufisadi wa EPA zifichuliwe wamekuwa wakisubiri kwa hamu hatua zitakazochukuliwa hasa baada ya Rais Kikwete mwenyewe kusema kupitia Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo kwamba, walioiba fedha hizo ni lazima wazirejeshe na ikibidi watafilisiwa.

 

Rais Kikwete akitafakari cha kufanya juu ya makundi hayo mawili, yaani wafadhili wanaompa fedha na wananchi ambao walimpa kura zaidi ya asilimia 80 wakionyesha imani kubwa kwake, makundi haya yakifanana kwa matumaini, kwani wanataka mafisadi waadhibiwe, kuna kundi la tatu ambalo ni watu wanaohusika na EPA, wengi wao wakielezwa kuwa karibu ama na watendaji serikalini au chama tawala.

 

Utata mkubwa zaidi wa EPA umeendelea kutanda hasa kutokana na taarifa kwamba, akaunti ya siri ya fedha za EPA ndani ya BoT bado imebaki na fedha kidogo zisizozidi Sh64 bilioni, kiasi ambacho ni chini ya nusu ya fedha zote zilizochotwa kifisadi ambazo ni Sh133 bilioni.

 

Luhanjo alipoulizwa kulikoni hadi sasa serikali imeota matende kuhusu ripoti ya EPA, hakuonekana kufurahishwa na maswali hayo na alitaka Ikulu kutokuulizwa swali hilo, badala yake alisema, suala hilo liko kwa timu ya Rais ambayo mwenyekiti wake ni Mwanyika.

 

Katibu Mkuu Kiongozi Luhanjo, alipoulizwa zaidi kwamba, kumekuwa na taarifa tata kutoka Ikulu, ambayo moja ni ile ya Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu kusema kwamba, muda wa timu hiyo umeongezwa, alijibu: “Hunielewi, leo siwezi kuzungumza na wewe kuhusu EPA, uliza timu.”

 

Kwa upande wake Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndulu, alipoulizwa jijini Dar es Salaam jana, alisema hadi sasa akaunti ya EPA ni siri.

 

Profesa Ndulu alisema, BoT haiwezi kutangaza siri za mteja wake na kuongeza pia kwamba, suala la EPA lipo chini ya timu maalumu, hivyo benki hiyo isingeweza kusema lolote.

 

“Nafikiri subiri timu iseme, sisi tuna akaunti nyingi za serikali, sasa kutaja ipi ni EPA ni kiasi gani cha fedha si sahihi, ni siri, nafikiri subiri timu ifanye kazi kisha itatoa taarifa,” alisema Profesa Ndulu.

 

Hata hivyo, Mwanyika wiki moja iliyopita aliliambia gazeti hili mjini Dodoma kwamba, kwa sasa asingeweza kusema chochote kuhusu EPA.

 

IGP Mwema alipopigiwa simu jana alielezwa kuwa katika mkutano huku simu ya Dk Hosea ikiwa haipatikani.

 

Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, wiki iliyopita wakati akizungumza na mwandishi wa habari hii akiwa bungeni, alisema uchunguzi wa EPA ulikuwa ukiendelea vizuri, lakini akamtaka mwandishi awasiliane na Mwanyika.

 

Wakati kukiwa na mkanganyiko huo, taarifa hizo kutoka duru za serikali zinaeleza kwamba, Rais anaweza kukabidhiwa ripoti hiyo wakati wowote.

 

Hata hivyo, changamoto kubwa kwa Rais Kikwete kwa sasa juu ya EPA ni jinsi ya kuchukua maamuzi, kwani anachelea kama asipowakuna wafadhili na wananchi, serikali yake inaweza kujikuta katika wakati mgumu.

 

Kwa mujibu wa taarifa hizo, Rais pia anafikiria matokeo ya maamuzi ambayo yanaweza kuwa mazito kwa wahusika, ambao baadhi ni watu wake wa karibu na walisaidia kuchangia kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005.

 

Timu ya kuchunguza ufisadi wa zaidi ya Sh 133 uliofanywa na makampuni 22, ilitangazwa na Ikulu kupitia Luhanjo, hapo Januari tisa na kuelezwa kwamba, ilipewa miezi sita, iwe imerejesha fedha hizo taslim au kukamata mali, hata hivyo, hadi sasa hakuna taarifa zozote rasmi kutoka serikalini kuhusu matokeo ya uchunguzi huo.

 

Timu hiyo ilipata kuzungumza na waandishi wa habari mara moja tu, na tangu wakati huo imekuwa ikiendesha uchunguzi wake kwa siri, licha ya Rais alipoiteua kuitaka kutoa taarifa kwa umma mara kwa mara. Haijulikani kama baadaye Rais alibadili mfumo wake wa utendaji kazi kuwa wazi hadi wa siri.

Next Page »

Blog at WordPress.com.